Hemed Mzee Hemed
Senior Member
- Jun 26, 2013
- 186
- 41
Sasa nimewaelewa CHADEMA.
Nimeamua kuzunguka baadhi ya wilaya za mkoa wa Pwani na kugundua kwamba hakuna mahali popote ambapo CHADEMA imeamua kufanya maandamano bila kupeleka barua polisi. Viongozi wanakaa vikao na kupata uamuzi wa pamoja, barua inaandikwa, maandalizi ya maandamano au mikutano inaanza kufanyika. Hakuna uhuni wowote wala hila zinazowekwa mbele, bali maslahi ya taifa.
Tayari nimeweza kupita Rufiji, Mkuranga, Kisarawe, Kibaha na Bagamoyo (Mafia sitafika) Na kujionea kwamba Wilaya zote na majimbo yote yatafanya mikutano na maandamano ndani ya siku hizi saba kuanzia leo jumamosi.
Maandamano yanaanza leo Bagamoyo kukiwa na kiwingu cha polisi kupiga marufuku maandamano hayo na mikutano ya CHADEMA ingawa CCM chini ya Kinana wakiruhusiwa hata kwa taarifa ya siku hiyo hiyo.. Hii ni barua niliyoipata (Nimeandika upya, sina scanner; Zuio la polisi bado sijaliona).
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA);
Kumb Na CDM/01/07/14/10
MKUU WA POLISI (w)
BAGAMOYO.
Ndugu,
Rejea kichwa cha habari hapo juu. Uongozi wa wilaya ya Bagamoyo umeazimia kufanya maandamano na Mikutano ya hadhara hapa Bagamoyo mjini kwa siku tatu mfululizo kwa kusudi la kutoa elimu ya uraia.
Maandamano yatafanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzia siku ya jumamosi hadi jumatatu. Ratiba ya yetu ya maandamano tumeipanga kwa umakini mkubwa kuepusha muingiliano wa aina yoyote na shughuli zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi zinazofanyika Bagamoyo. Zaidi ya yote tumezingatia sheria zote za nchi ili tulinde haki yetu ya kuandamana. Ratiba yetu ni kama ifuatavyo:
1. Jumamosi 20/09/2014 – Saa 3 – 12 jioni – Kuanzia njia panda ya hospitali ya wilaya, kupitia Mangesani, Soko la Tandika, Kisutu, Saigoni, Mageti mia, Nianjema shule ya msingi, Checkpoint, Stendi ya Kongowe, Magomeni na kuishia Top top.
2. Jumapili 21/09/2014 – Saa 3 – 12 jioni Kuanzia Caravan Serai, Kupitia CRDB, Posta, Kosovo, Bong'wa, Majikosti na kuishia Kidongo chekundu.
3. Jumatatu 22/09/2014 – Saa 3 – 12 jioni kuanzia SLADS, Cosovo, Mbuyuni, Hill Side, Stendi mpya, Corner Bar hadi Soko jipya au stendi ya Zamani ambako mkutano wa hadhara utafanyika.
Maandamano hayo yataongozwa na viongozi wa CHADEMA wilaya na majimbo mawili ya wilaya ya Bagamoyo kulingana katiba yetu na taratibu za chama chetu tulizojipangia. Tunatanguliza Shukrani iwapo ofisi yako itazingatia na kulinda haki yetu ya kuandamana kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.
Nakutakia kazi njema;
……………………………………………………………..
Bi Nuru Ramadhan
[Katibu wa CHADEMA – (w) Bagamoyo]
Nakala kwa:
: Mratibu wa CHADEMA kanda
: Katibu wa CHADEMA mkoa wa Pwani;
:Katibu jimbo la Bagamoyo;
:Katibu jimbo la Chalinze.
Updates:
Polisi walipeleka CHADEMA barua ya Zuio la mikutano jana mchana (sina scanner kuiweka hapa). Viongozi wamekuwa wakipigiwa simu kushawishiwa kuahirisha maandamano. Muda huu polisi wameweka kambi ofisi za CHADEMA na mahali ambapo maandamano yataanzia. Wanachama wako jirani na eneo la tukio.
Kikao cha viongozi kimefanyika usiku, na kingine kiko jirani na eneo la tukio.
Nimeamua kuzunguka baadhi ya wilaya za mkoa wa Pwani na kugundua kwamba hakuna mahali popote ambapo CHADEMA imeamua kufanya maandamano bila kupeleka barua polisi. Viongozi wanakaa vikao na kupata uamuzi wa pamoja, barua inaandikwa, maandalizi ya maandamano au mikutano inaanza kufanyika. Hakuna uhuni wowote wala hila zinazowekwa mbele, bali maslahi ya taifa.
Tayari nimeweza kupita Rufiji, Mkuranga, Kisarawe, Kibaha na Bagamoyo (Mafia sitafika) Na kujionea kwamba Wilaya zote na majimbo yote yatafanya mikutano na maandamano ndani ya siku hizi saba kuanzia leo jumamosi.
Maandamano yanaanza leo Bagamoyo kukiwa na kiwingu cha polisi kupiga marufuku maandamano hayo na mikutano ya CHADEMA ingawa CCM chini ya Kinana wakiruhusiwa hata kwa taarifa ya siku hiyo hiyo.. Hii ni barua niliyoipata (Nimeandika upya, sina scanner; Zuio la polisi bado sijaliona).
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA);
chademabagamoyo@gmail.com
WILAYA YA BAGAMOYO.
18/09/2014
MKUU WA POLISI (w)
BAGAMOYO.
Ndugu,
YAH: RATIBA YA MAANDAMANO YA AMANI