Maandamano ya UKAWA kushinikiza utekelezaji wa maazimio ya Bunge...

Nomile

Member
Dec 5, 2012
99
125
VIONGOZI UKAWA

Napenda kuleta pendekezo la kuandaa Maandamano (wakilishi) yaani yenye kushilikisha wadau kutoka kada mbali mbali na katika umoja wa ukawa,na taasisi za kiraia tupeleke ujumbe wetu kwa Mkiti wa Mabalozi wahisani MAMA Antila ujumbe uelezee kwa ufasaha jinsi Serikali inavokataa kuchukua hatua dhidi ya wale wote waliohusika na Mchezo Wa ESCROW.Na ujumbe utafsiri waziwazi kwamba serikali inakwepa kujichukulia hatua yenyewe maana viongozi wetu wanahusika hivyo wametusaliti

Ujumbe uambatane na mapendekezo yafatayo

1.Wale wote waliohusika katika mchezo huo wasiruhusiwe kuingia katika nchi wahisani
2.Wadau wote wa maendeleo waweke wapitishe Azimio la kutoshirikiana na watu hawa katika jambo lolote la kiserikali
3.Waendelee kubana misaada

Ujumbe huo upelekwe mapema, hatuwezi kuchezewa na wezi wachache tukae kimya HAPANA wananchi sisi ni wengi na wao ni wachache.tuchukue hatua
 

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,250
mimi kwa kweli nashangaa ukawa kuwa kimya kwenye suala hili lililokuwa wazi kama hili jk anasubiri maandamani ili awafukuze kazi wausika. ukawa mmefanya kazi safi bungeni sasa nendeni mkamalizie suala ili kwa wananchi kukaa kwenu kimya mkitegemea kikwete afanye maamuzi bila shinikizo hana record ya kufanya kazi bila shinikizo kuanzia kuwafukuza wakina ngeleja, kuwasilikiliza madokta, suala la katiba na mabadiliko ya katiba, kukutana na ukawa kuzungumzia hatima ya katiba kote huko ilikuwa ni shinikizo.

kuna mtu mmoja anaitwa Prosper mbena huyu ndiye anayefanya kazi za rais ikulu ni mtu mkubwa sana na katika issue ya escrow huyu ndiye aliyesaini kutoka ikulu kubariki escrow na amefanya hivyo kwa ruhusa ya rais bila hivyo angefukuzwa kazi.

ukawa please kama tusipoingia kwenda maandamano kwenye suala hili ambalo ni jepesi kulielewa ukilinganisha na katiba je tutaingia mtaani kwa issue gani?? Rais mzuri lazima uwe tayari kufanya maamuzi ambayo ni magumu na yanaumiza kichwa kitu ambacho jk hawezi anachukia vitu controversial anapenda vitu rahisi kama kufungua barabara na kufanya teuzi huku akiwa tembo mzito ametanda ikulu lakini anaekti kama vile hamuoni kwahiyo kazi yetu ni kumshinikiza ili adili na tembo aliyejaa tele ikulu
 

Mutakyamirwa

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
4,945
1,500
Bado tunaendelea na uchunguzi wa akili za watanzania waliowengi kuhusu maandamano. Yamkini si njia sahihi wanayoihitaji kuleta mabadiriko. Yameitishwa maandamano mengi na bado si ajabu waleta mada hamjawai husika hata siku moja.

Ili turazimu siku moja kuchapana viboko hapo udsm kuwaodoa vijana akili mgando kwenye vimbwete kuona umhimu wa kwa nini tulihitaji kupinga udharimu wa serikali kipindi hicho. Zoezi lilifanikiwa kiasi chake....ila sijajua kama kanuni hii ndo itumike uraiani. Hata ukiwanyima umeme na maji mwezi mzima dar hakuna atakaye andamana....sembuse escrow inayotetewa na kumfubiwa macho na rais wao 'kipenzi na serikali yake sikivu'

Kuna tatizo,tena kubwa ktk nchi hii.....litatoka baada ya shida na mateso makali ya kimageuzi si miaka mingi inayokuja. Watanzania wanasubili kujifunza kutokana na SHIDA si SHULE
 

kilambalambila

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
8,822
2,000
Ukawa inazidi kupungua makali, 2015 nina wasiwasi kama itakuwa na nguvu kupambana na ma ccm
 

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,008
2,000
Badala ya kutafuta pesa zenu mnakaa kuandamana kwa ajili ya pesa za IPTL. Mitambo yao mmeitumia ila kwenye malipo mnaleta zengwe eti watu waandamane kupinga Escrow. Kama pesa hazikuwa za IPTL Tanesco ilikuwa inalipa za nini? Kama kiwango cha malipo kimezidi mbona hamsemi kimezidi kiasi gani? Kama kosa ni usajili wa PAP kuwa fake mbona Brela na Wizara ya viwanda na madini haijaguswa? Kama kosa ni kutokukusanya kodi mbona TRA na Wizara ya Fedha haijaguswa?
 

Hijja Madava

JF-Expert Member
May 14, 2014
3,167
2,000
Badala ya kutafuta pesa zenu mnakaa kuandamana kwa ajili ya pesa za IPTL. Mitambo yao mmeitumia ila kwenye malipo mnaleta zengwe eti watu waandamane kupinga Escrow. Kama pesa hazikuwa za IPTL Tanesco ilikuwa inalipa za nini? Kama kiwango cha malipo kimezidi mbona hamsemi kimezidi kiasi gani? Kama kosa ni usajili wa PAP kuwa fake mbona Brela na Wizara ya viwanda na madini haijaguswa? Kama kosa ni kutokukusanya kodi mbona TRA na Wizara ya Fedha haijaguswa?
masikini we wa watu sijui kua hata sh 10 uliiona
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom