Maandamano ya NCCR-Mageuzi, Mtwara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maandamano ya NCCR-Mageuzi, Mtwara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waridi, Mar 10, 2012.

 1. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kutoka gazeti la Mtanzania

  [h=2]NCCR- Mageuzi kuandamana Mtwara [/h]Jumamosi, 10 Machi 2012 09:23 Na Mwandishi Wetu, Newala

  CHAMA cha NCCR-Mageuzi, kinatarajia kufanya maandamano ya amani Mjini Mtwara ili kuishinikiza Serikali iwajali wakulima wa zao la korosho mkoani Mtwara.
  Akizungumza na MTANZANIA Mjini Newala jana, Katibu Mwenezi wa chama hicho, Moses Machali, alisema maandamano hayo yatafanyika kesho kuanzia saa 8 mchana.

  Pamoja na suala la zao la korosho, alisema pia maandamano hayo yatafanyika kama sehemu ya kuhitimisha ziara ya wiki moja ya viongozi wakuu wa chama hicho mkoani Mtwara.
  “Kama unavyojua, Mkoa wa Mtwara una changamoto nyingi na mojawapo ni kuhusu kudorora kwa bei ya zao la korosho ingawa pia zao la karanga nalo halina faida kwa wakulima wa mkoa huu.

  “Ni ukweli ulio wazi kuwa, Serikali imewasahau kabisa wakulima wa korosho, bei ya korosho iko chini na hata wanapoiuza wanakopwa wakati ikijulikana kuwa kuwakopa ni njia mojawapo ya kudhoofisha maisha yao.

  “Kwa kuwa tuko katika mkoa huu kuanzia Machi 4, mwaka huu, tunatarajia kuhitimisha ziara yetu kesho Jumapili kwa kufanya maandamano makubwa ya amani Mjini Mtwara ili kuishinikiza Serikali iwajali wakulima wa korosho ambao wengi wao wanaishi maisha ya shida bila sababu za msingi.

  “Sisi ni wazalendo wa kweli, hatutaki kuona Watanzania wenzetu wakinyanyasika katika nchi yao, hatutaki kuona wakulima wanalima kilimo kisichokuwa na faida, kwa hiyo, tutaitisha maandamano hayo ili kuwaamsha wakulima na wananchi wa Mtwara kwamba CCM si chama chao bali ni chama cha wachache.

  “Kwa bahati nzuri katika ziara hii yupo Mwenyekiti wetu wa Taifa, James Mbatia, sasa huyo ndiye atakayeongoza maandamano hayo na watakuwapo pia viongozi wengine wa kitaifa waliopo katika ziara yetu hii,” alisema Machali ambaye pia ni Mbunge wa Kasulu Mjini.

  Kwa mujibu wa Machali, uongozi wa NCCR- Mageuzi, Jimbo la Mtwara Mjini, umeshatoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, Wilaya ya Mtwara Mikindani kwa ajili ya kuomba ulinzi wakati wa maandamano hayo.

  “Polisi wameshapewa taarifa kama ilivyo kawaida, maandamano yataanzia eneo la Mkanaredi Magomeni kupitia mkoani, Bima, Soko Kuu, Chilindima na yataishia katika Uwanja wa Mashujaa uliopo Mtwara Mikindani.

  “Kwa maana hiyo, tunawoamba wananchi wa Mtwara wajitokeze kwa wingi katika maandamano hayo kwa sababu tutatoa tamko zito kuhusu zao la korosho linaoonekana kuwa kero kwa wananchi ingawa ni muhimu kwao,” alisema.
   
 2. H

  Han'some JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
   
 3. February

  February Member

  #3
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Inanikumbusha kitabu cha hekaheka mtoni. Tehtehteh. Kazi kwelikweli.
   
 4. Waridi

  Waridi JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,027
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Polisi Mtwara wamkwaza Mbatia


  na Mwandishi wetu, Mtwara


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amekerwa na tabia ya Jeshi la Polisi nchini kutokana na tabia ya kupenda kuzuia maandamano ya vyama vya upinzani.
  Akizungumza mjini hapa jana, Mbatia alisema kuwa jeshi hilo limekuwa na tabia ya kuvidhibiti vyama hivyo bila sababu za msingi ingawa vina haki ya kuandamana kwa kuwa vimesajiliwa kwa mujibu wa sheria.
  Akihutubia mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara yake ya wiki moja mkoani Mtwara, alilishutumu jeshi hilo kwa hatua yake ya kuzuia maandamano yaliyopangwa kufanyika kabla ya mkutano wa hadhara.
  "Kwanza kabisa polisi ni lazima wajue kwamba, sisi chama chetu siyo cha vurugu, chama chetu ni cha amani na ndiyo maana hata kwenye bendera yetu, kuna rangi nyeupe, hatutaki ugomvi na mtu.
  Pamoja na kwamba sisi ni watu wa amani, polisi wajue wakituletea longolongo, wajue tutapambana nao, hii inashangaza sana kuona wanazuia maandamano yetu, tunajua wanafanya hivyo kwa sababu wanashawishiwa na Chama cha Mapinduzi," alisema.
  Aliongeza kuwa polisi wanasahau kuwa mishahara yao na sare zao vinatokana na kodi za wananchi, hivyo inashangaza kuwazui kuandamana kwa kisingizio cha mgomo wa madaktari.
  "Kwa hiyo tunawaambia polisi kwamba muda wa kutunyanyasa umekwisha, siku nyingine wakitoa sababu nyepesinyepesi kama hizi, wajue hatutawavumulia," alisema Mbatia.
  Naye, mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali, alilishambulia jeshi hilo na kulitaka liache kuvinyanyasa vyama vya upinzani kwa kuwa Tanzania ni ya Watanzania wote.
  "Mara nyingi sisi huwa hatupendi kulumbana, huwa tunapenda kukaa mezani na kumaliza tofauti zetu, kwa watu makini kama sisi leo tunakubali kutoandamana lakini siku nyingine wajue hatutakubali," alisema.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 5. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wamevamia ngome ya mwisho ya CUF, anyways nilikuwa napita tu mtaa huu
   
Loading...