...Mawazo yangu, wapiganaji wa ufisadi, waandae maandamano ya amani kuitaka serikali ishugulikie swala la mafisadi kwa haraka zaidi. Tunahitaji kesi hizi zisikilizwe ndani ya miezi 6, na suluhu zake zipatikane kabla ya 2009 haijaisha....
If we talk the talk, lets do the walk.
Naunga mkono wazo ila ngoja wait....
Kama gazeti la Mwanahalisi lililoandika habari za kuwanufaisha wao (watwana) likaishiwa kufungiwa. je sisi ambao tukiamua kuandamana si itakuwa yale yale ya wanyasa kuitwa wamalawi?
Haki haijawahi kuja kirahisi rahisi, kwahiyo nauhakika hata haya maandamano hayatakuwa marahisi. Siwezi kusema watakaoamua kushiriki kwa udi na uvumba, jinamizi la ukandamizaji halitawasogelea. Najua lazima litatufuata tu! Lakini hiyo ndio hali halisi ya upambanaji kujitoa muhanga, ila kama waandaaji wa mapambano inabidi kufikiria ni jinsi gani tutapunguza hizo athari.
Njia moja wapo ni kuhakikisha wanaongoza haya maandamano ni watu wanaojulikana katika jamii na mashirika ya kijamii na vyombo vya wanafunzi, hata kama serikali itakyereka vipi hawezi kuvifunga kirahisi.
Hapa tunapigania maslahi na heshima ya nchi kimya kimya ila mawazo yetu ndo yanapiga kelele kukemea uozo na uzandiki wa watawala kupitia forums kama hizi.
Nadhani kwanza tunapaswa kuwachechemiza wanaozimiliki sheria (polisi) kwa kuwaelimisha ili wabadilike kwanza kisha ndo mtaona mfululizo wa maandamano ya HAKI ukirindima. Nchi hii huchelei kuitwa HAINI kisa tu unadai chako
kuna rafiki yangu mmoja kutoka ng'ambo ya bahari, huwa anawahamasisha sana washkaji zake kuandamana kule ng'ambo ila inapotokea dalili ya majiwasha huwa haonekanagi ktk kilinge hata kushiriki, yeye huchagua aina ya maandamano ya yeye kuandamana nao.
Sina nia mbaya ila kwanza lazima kuelimishana kuondoa ukungu wa sheria na haki kutoka kwa wabeba bunduki wetu kisha hata wakiamua kututandika shaba iwe wanajua wanafanya nini maana sasa wanajua kuwa wana kazi moja tu kuwalinda watawala hata kama hao watawala wameoza vipi.
umenipata hapo?
Vita dhidi ya Mafisadi inahitaji nguvu ya wananchi sasa. Maana mpaka sasa wananchi wamekuwa wasikilizaji na watazamaji tu. Umefika wakati ambapo tunahitaji kutambua kama hii vita ya mafisadi inawagusa kweli wananchi, na pia serikali itambue inahitaji njia za haraka kudhibiti ufisadi!
Sidhani kama tunataka viporo kwa uongozi ujao, tunataka ufisadi ushugulikiwe ndani ya awamu ya kwanza ya kikwete, na asiposhughulikia kipindi hichi basi ndio ajue itakuwa swali lake kubwa katika uchaguzi ujao.
Mawazo yangu, wapiganaji wa ufisadi, waandae maandamano ya amani kuitaka serikali ishugulikie swala la mafisadi kwa haraka zaidi. Tunahitaji kesi hizi zisikilizwe ndani ya miezi 6, na suluhu zake zipatikane kabla ya 2009 haijaisha.
Maandamano yawe katika mikoa mitatu tofauti, na Zanzibar, katika siku zinazofuatana ndani ya wiki mbili. Kwa mfano maandamano yazinduliwe tarehe 9 may, Dar, tarehe 10 yapelekwe Kilimanjaro, halafu tarehe 16 yaende mwanza na 17 yafungiwe Zanzibar.
Napendekeza mengi, kupitia ujasiri wake wa kuwataja mafisadi na vyombo vyake vya habari, awe kinara wa maandamano hayo, mzee mwanakijiji ashugulikie agenda za maandamano hayo, NGOs zihamasishwe kushiriki, hasaFEMACT imekuwa mstari wa mbele kupinga ufisadi. Kitila Mkumbo uhamasishe watu wa vyuoni hasa vyombo vya wanafunzi kushiriki katika maandamano haya. Na watu wengine wenye michango mbalimbali katika harakati, ambao siwafahumu wajitolea kuhamasisha na kupanga maandamano haya.
Umefika wakati wa kujiondoa katika magazeti na kujipima kupitia wananchi kama kweli ni agenda yetu sote.
If we talk the talk, lets do the walk.
BWT....!Je, unafikiri serikali itashtuka kwa maandamano hayo, kwani kina Dr. Slaa si walishaandamana na kutaja a list of shame...what happened thereafter? Je, serikali yetu inajua implications za wananchi kuandamana? kwani inawauma kusikia wananchi wanaandamana? mimi siamini kabisa kama eti kuandamana kwa siku moja tu kutawakosesha serikali usingizi...!
Labda sema tujipange mitaani hadi ikulu, tukiimba nyimbo za ukombozi na taifa......non stop mpaka watoe tamko rasmi la hatua madhubuti za kuwachukulia hatua mafisadi au mpaka waresign! Hili lisiwe zoezi la siku moja ...no, iwe ni non stop...hapo nafikiri hawa watastuka!
Alternatively, labda tuandae ushahidi wa kutosha kuwashtaki mafisadi wote then petition iandaliwe na isainiwe na wananchi wote wanaokereketwa na ufisadi, then tutafute Advocates watusaidie kuwafungulia kesi mahakamani tukishirikiana na wanaharakati mbalimbali! Mimi nipo tayari kuisupport hii morally and materially tukishajipanga vizuri!
Wazo zuri Petu Hapa.
Wanajamvi tunaweza kuandaa maadamano nchi nzima kuishinikiza serekali ichukue hatua za kisheria dhidi ya mafisadi.
Ni wazo zuri sana. Daima nguvu ya umma hushinda. Kwa kuwa JF si jukwaa la kisiasa ni vema wanaharakati wakashirikishwa.
Maandamano ya kugawanyika hawayaogopi, lakini maandamano ya pamoja bila kujali itikadi wanayaogapa ila wanauhakika hayawezi kutokea
Unajua kwa nini wanauhakika huo, reason mmoja wapo ni kwamba watz ni mbumbu wa kutupwa, wana njaa, ni maskini, ni wanafiki, ni waroho, hawana misimamo like Kenyans, Zambians, South Africans, Madascans etc....so is very easy to paly around with them! Usione watu hapa JF wamehamasika, embu nenda mitaani uliza maswali vijana wakawaida, wape idea ya kuandamana mitaani kuhusu ufisadi.....then rudi utupe jibu! Kifupi tunahitaji kutoa elimu sana kwa watanzania kuelewa elimu ya uraia na haki zao za msingi!
Amini nakwambia, serikali ikiona zaidi ya watu elfu 6000 barabara moyo utaenda mbio tu.
Naomba Mungu ndoto hizi zije zitokee nikiwa bado naishi.....one day yes!
Tatizo maandamano mengi yanayoendelea ni tumejigawa sana, ngo's kivyao, waislamu kivyao, vyuo vikuu kivyaoo, kafuu kivyao, sekondari kivyao. Sasa tukivuja hiyo kivyao vyao, na kuwa sisi! Serikali itacheza dede!
Migawanyiko inatokea kwa sababu ya mambo niliyoorodhesha hapo juu!
Lakini swali la msingi pia, ambalo wataalamu wa maswala ya siasa na serikali watuambie - haya maandamano lengo lake liwe nini na tumshinikize nani, halafu tutajua wapi tutaelekea na tujipange vipi
Tunaishinikiza serikali mkuu....Rais+ Cabinet..& Co!
This is not an alternative it should be a second stage of citizens action toward mafisadi. Maandamano yaanze, stage two petition.
Kama hilo hapo juu haliwezekani kwa msingi wa umbumbumbu wa watz walio wengi, basi sisi wenye mwanga kidogo na haki za watanzania basi tuact on their behalf tukitumia option ya pili na tuifanye ya kwanza!
Unajua kwa nini wanauhakika huo, reason mmoja wapo ni kwamba watz ni mbumbu wa kutupwa, wana njaa, ni maskini, ni wanafiki, ni waroho, hawana misimamo like Kenyans, Zambians, South Africans, Madascans etc....so is very easy to paly around with them! Usione watu hapa JF wamehamasika, embu nenda mitaani uliza maswali vijana wakawaida, wape idea ya kuandamana mitaani kuhusu ufisadi.....then rudi utupe jibu! Kifupi tunahitaji kutoa elimu sana kwa watanzania kuelewa elimu ya uraia na haki zao za msingi!
Unajua Serikali yetu is smart more than us. Lakini sisi ndio hatutaki kuwelewa. Serikali kwa kiasi kikubwa anafanya kiburi kwa kuwa inahakika asilimia kubwa ya wananchi hawana nguvu ya kuweka katika mapambano. Inawezekana kabisa kwa sababu binafsi lakini kwa kiasi kikubwa na sisi watu wakati kushidwa kuonyesha njia.
Natambua hamasa ya JF sio ambayo iko mtaani, lakini ninaimani kabisa wananchi wanakyerwa na upupu unaoendelea. Naamini watu wa DECI DECI ni wengi. Naamini Cost Sharing Vyuoni inawakerya wengi! Naamni ardhi zimegawanya bila mpango maeneo mengi! Naamini wamachinga wanapigwa na jua sana. Kwa ujumla, wananchi wamefinyika, na wapo tayari kupambana iwapo watu wenye maono mapana watakuwa jasiri kuonyesha njia.
Ni woga wetu sisi watu wakati, hesabu tunazipiga nyingi, elimu yetu hajatufanywa tuwe jasiri ila imetufanywa tuwe woga wa kusema wazi tunachofiri. Tunajali zaidi kazi zetu kuliko maisha ya badaye ya watoto wetu! Tumefungwa macho na vijisenti vidogo bila kugundua we can create new employment if change!
The whole problem is about us, and not the people in the streets!
Watamwaga FFU, polisi na hata jeshi ili kuhakikisha maandamano hayo hayafanyaki. Si mnajua CCM ni chama cha mafisadi!? Kwanini waruhusu maandamano ya Watanzania waliochoka na ufisadi na hali chama hicho si wawakilishi tena wa wakulima na wafanyakazi?
Nadhani tukipata documentary chache ya maisha halisi ya watanzania na kusikia kutoka kwa watu waliochoka kama Mengi alivyofanya then swala la kuingia barabarani litakua automatic.