Maandamano ya Kitaifa Cameroon wakidai ushindi wa Kiongozi wa upinzani Issa Tchiroma utambuliwe

Maandamano ya Kitaifa Cameroon wakidai ushindi wa Kiongozi wa upinzani Issa Tchiroma utambuliwe

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Maelfu ya waandamanaji walimiminika mitaani jijini Douala, mji mkuu wa kiuchumi wa Cameroon, siku ya Jumapili Oktoba 26, 2025 wakijibu wito wa kitaifa uliotolewa na kiongozi wa upinzani, Issa Tchiroma Bakary. Waandamanaji wengi wakiwa ni vijana, walipita katika mitaa mikuu ya jiji hilo wakitaka mamlaka zitambue ushindi wa Tchiroma katika uchaguzi uliopita na zitangaze matokeo halisi, ambayo yanatarajiwa kutolewa rasmi Oktoba 27, 2025

Soma Viongozi wawili wa Upinzani Wakamatwa Cameroon, Tchiroma atoa wito Maandamano ya Kitaifa

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, maandamano hayo yalienea haraka katika mitaa kadhaa ya Douala, ikiwemo eneo lenye wakazi wengi la New Bell. Hata hivyo, hali iligeuka kuwa ya taharuki baada ya polisi na askari wa kutuliza ghasia kuripotiwa kutumia risasi za moto kuwatawanya waandamanaji. Mashuhuda wanasema watu wawili walipigwa risasi huku wengine kadhaa wakikimbizwa hospitalini, baadhi wakiwa katika hali mahututi.

Kadri taarifa za makabiliano zilivyozidi kusambaa, maandamano hayo yalivuka mipaka ya Douala na kuenea hadi katika miji mingine ikiwemo Garoua, Maroua, Meinganga, Kaélé, na Bertoua, yakigeuka kuwa kile kinachoelezwa kama “vuguvugu la kitaifa la kudai ukweli wa uchaguzi.”

Wachambuzi wameonya kuwa hali bado ni tete, huku kukiwa na hofu ya machafuko zaidi wakati tume ya uchaguzi ikijiandaa kutangaza matokeo rasmi. Wakati huo huo, wafuasi wa Issa Tchiroma Bakary wameendelea kutoa wito wa utulivu, lakini wamesisitiza kuwa madai yao ya uwazi na haki lazima yasikike

1761544780036.png



 
Back
Top Bottom