Maandamano ya Chadema yatishia Serikali ya CCM madarakani

Maandamano ya Chadema yatishia Serikali ya CCM madarakani

Makamba: Wanaofikiria kumng'oa JK wahaini


na Betty Kangonga


amka2.gif
KATIBU MKUU wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba, amesema wanaofikiria kumpokonya Rais Jakaya Kikwete kiti chake cha uenyekiti wa chama hicho ni wahaini.
Makamba alitoa kauli hiyo jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari akijibu taarifa ya gazeti hili juzi kwamba kuna kikundi ndani ya CCM kinachofikiria kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti wa chama hicho tawala.
Huku akitumia maneno makali na ya kejeli, Makamba alisema Rais Kikwete ni mtaji wa kuaminika ndani ya chama hicho na kwamba alishinda uchaguzi mkuu uliopita kwa sababu ya umaarufu wake.
"Mtaji kwa kawaida haufujwi bali unakuzwa, kwa hiyo hatuwezi kumng'oa Rais Kikwete anayependwa na wananchi baada ya ushindi huu mkubwa, alisema na kuongeza:
"…kitendo chochote cha kufikiria kumng'oa katika nafasi hizo ni cha uhaini dhidi ya chama chetu na hakiwezi kukubalika," alisema Makamba.
Alisema hata Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haina uwezo wa kumng'oa mwenyekiti huyo na wala CCM haiwezi kutenganisha kofia alizonazo Rais Kikwete.
Katika gazeti hili Jumatano wiki hii iliripotiwa taarifa iliyoeleza kuwa mambo yazidi kwenda mrama ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo mkakati unasukwa kutaka kumuengua Rais Jakaya Kikwete kwenye nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho taifa.
"Sababu kubwa inayotajwa na waumini wa mkakati huo ni kwamba muundo wa sasa wa Rais kuwa na kofia mbili umesababisha dhambi za chama kubebwa na serikali na zile za serikali kubebwa na chama," ilibainika.
 
Makamba aliponda gazeti, ataka JK aheshimiwe

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 1st April 2011 @ 09:17 Imesomwa na watu: 564; Jumla ya maoni: 5








CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema Rais Jakaya Kikwete bado ni mtaji wa chama hicho na sasa wana mpango wa kuukuza na si kuufuja.

Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alisema hayo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kukanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Tanzania Daima la jana kuwa chama hicho kimepanga kumng'oa Rais Kikwete katika nafasi yake ya Uenyekiti wa chama hicho.

"Mtaji kwa kawaida haufujwi bali unakuzwa, kwa hiyo hatuwezi kumng'oa Mwenyekiti wetu na Rais anayependwa na wananchi baada ya ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi
Mkuu uliopita," alifafanua.

Aliwataka wananchi kupuuza habari hizo na kuongeza kuwa ni uzushi na upuuzi.

"Habari hizi sio za kweli ni za kufikirika, hii ni moja kati ya tabia zinazokera za gazeti hilo na mengine yanayofadhiliwa kuichafua Serikali na Chama Cha Mapinduzi kwa kuandika habari za kufikirika, za uongo na uzushi," alisema Makamba katika taarifa
hiyo.

Alisema kitendo chochote cha kufikiria kumng'oa Rais Kikwete katika nafasi yake ya Uenyekiti ni sawa na uhaini dhidi ya CCM na hakiwezi kukubalika kwa kuwa ndani ya chama
hicho wanaamini kuwa, yeye tayari amevaa ngozi mpya na ataendelea hadi atakapokabidhi kijiti.

Alisema NEC haina uwezo wa kumng'oa Mwenyekiti na wala CCM haina mpango wa kuzitenganisha kofia ya uenyekiti na urais na kwamba zitaendelea kuvaliwa na mtu mmoja
katika ngazi ya Taifa.

"Napenda watambue kuwa Mheshimiwa Jakaya Kikwete ndiye Rais wa nchi yetu anayestahili
kuheshimiwa na wananchi wote, si adabu kumchezea, kumdhalilisha na kulidhihaki jina lake, lazima uangalifu mkubwa utumike mtu anapotaka kulitumia jina lake," alisisitiza Makamba.



Jumla Maoni (5) Maoni Sawa Mjomba Makamba,
Ukweli ni kuwa kuna Gazeti moja ni la uchochezi mkubwa na limelenga kuleta machufuko nyie mmenyamaza!
Hilo Gazeti linaleta pandikizi za mambo ya Kenya na kushabikia udini fulani na hatuoni Mtu Serikalini kuchukua hatua! Maoni Hii sasa ajabu!!!. Huyo Makamba vijana wake wa UVCCM walipotamka hadharani kwamba jin la rais ajaye liko mezani kwa Rais Kikwete alikaa kimya kama maji ya mtungi. Hii habari ya gazeti la Tanzania Daima mbona ameijibu kwa haraka sana? Jamani hivi kuna nini ndani ya CCM? Anyway, "Panapofuka moshi panaficha moto." Ipo siku Makamba anakuwa kama "Hussein Mubarrak" Maoni Ningemshauri Mkamba kwanza afanye utafiti kuhakiki kama kweli JK anapendwa, na kama kweli alipata "ushindi mkubwa" katika uchaguzi uliopita.
MAkamba, kama katibu mkuu wa CCM, ni mtendaji mkubwa sana katika chama, ila inaonekana hafahamu vizuri wajibu wake. Awatafute waliomtangulia ili wamwelekeze namna ya kuunganisha chama, na si kukibomoa kama anavyofanya yeye. Maoni kama Makamba angetafakari,angeona kuwa yaliyoandikwa yana mantiki.ni kweli kofia mbili haifanyi kazi kwa sasa.Serikali ingeachiwa iendeshe nchi bila siasa zisizo na maana,na siasa kiachiwe chama.ukiangalia kuoa ukweli kwa yaliyoainishwa kwa mujibu wa gazeti hilo... Maoni mzee makamba umaarufu wa jk hauwezi kuzidi wa ccm. kusema jk ni mtaji kuliko ccm yenyewe ni kutudharau wanaccm. nionavyo mimi ccm ni muhimu kuliko mtu yeyote nchini. mzee makamba kwa heshima yako 2012 jiuzulu ukatibu vinginevyo 2015 jk unayesema ni mtaji hagombei nini hatima ya chama chetu ccm.
 
Profesa Safari aibukia Chadema Send to a friend Saturday, 02 April 2011 09:33

Geofrey Nyang'oro
MWANASHERIA maarufu nchini, Profesa Abdallah Safari, amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).Akizungumza jana mara baada ya kukabidhiwa kadi hiyo katika Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni, Dar es Salaam, Profesa Safari alisema angependa chama hicho kiyafanyie kazi mambo matatu katika harakati zake za kuchukua dola.

Aliyataja mambo hayo kuwa ni nyumba za Serikali ambazo ziliuzwa kwa watumishi wake, udini na ukanda.
Alikitaka chama hicho kushughulikia kwa uzito wa kipekee suala la uuzwaji wa nyumba hizo uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Tatu, akidai kuwa huo ulikuwa ufisadi mkubwa kuwahi kufanywa nchini.

Kwa mujibu wa Profesa Safari, kitendo hicho kilikiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 9 na kusema kwa vyovyote vile kinastahili kupingwa.

"Mambo yanayofanyika hivi sasa yalitabiriwa na Rais wa Kwanza wa Ghana, Kwame Nkrumah katika kitabu chake kwamba watatokea viongozi watakaoliuza bara hili kwa bei nafuu,"
Profesa Safari alipindekeza njia mbili za kushughulikia suala hilo. Kwanza alisema ni kwenda mahakamani au kutumia nguvu ya umma akisema hiyo ya pili ndiyo sahihi zaidi kwa mapendekezo yake.

"Suala la kwenda mahakamani kupinga uuzwaji wa nyumba za Serikali linaweza kuwa gumu kwa sababu walionunua nyumba hizo wapo na majaji. Njia ya iliyo bora ni ile ya nguvu ya umma," alisema.

Jambo jingine ambalo Profesa Safari alitaka Chadema ilifanyie kazi ni propaganda za udini na ukanda zinazoelekezwa kwa chama hicho ambazo alidai kuwa zimesukwa ili kukidhoofisha."Wakoloni walitumia mbinu ya kutugawa katika misingi ya udini, ukabila na ukanda ili waweze kututawala na leo (CCM) wanatumia mbinu hizo," alisema Safari na kuongeza:
"Walianza kwa kusema CUF ni chama cha Kiisilamu na watu wakaamini hata kufanikiwa kukidhoofisha na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakatoliki. Hizi ni propaganda."

Alitoa wito kwa wasomi na wanaharakati kuanza kutoa elimu kwa wananchi dhidi ya propaganda hizo ili jamii ielewe ukweli."Ninashukuru kwa sasa kuna vijana wengi hasa wasomi kutoka vyuo vikuu wameanza kutambua suala hilo. Wito wangu kwao ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu historia ya Taifa hili ili watu waelewe na kushiriki ukombozi wa nchi yao," alisema.

Alisema ni suala linalotakiwa watu kukaa chini na kulifanyia kazi kwa kuwa linaweza kukidhoofisha Chadema.
"Tuliliona suala hilo wakati wa uchaguzi. Watu walitumia propaganda hiyo na wengi tulishuhudia kwani wapo waliopiga kura wakitumia sifa ya Uislamu na kuacha kiongozi mwadilifu aliyekuwa tayari kutetea tunu za Taifa," alisema Safari.

Profesa Safari alitaka suala hilo lifanyiwe kazi na chama hicho ili kuelimisha Watanzania na kufuta dhana hiyo akidai hiyo itawezesha Taifa kuwapata viongozi wenye nia ya dhati ya kutetea rasilimali zake.

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wote wa Chadema akiwamo Mwenyekiti, Freeman Mbowe, Profesa Safari alikumbuka adha aliyoipata na familia yake baada ya kufukuzwa kazi katika Chuo cha Diplomasia (CFR) kinachomilikiwa na Serikali kwa sababu za kisiasa.

"Niliumia mimi na familia yangu na hasa mke wangu ambaye alinishauri nisijiunge na siasa tena. Lakini, baada ya kushauriana na kushauriwa kwa muda wa miezi mitatu, nimeamua kujiunga na Chadema," alisema Profesa Safari.
Awali, Mbowe akimkaribisha Profesa Safari, alisema Chadema imelenga kumtumia msomi huyo katika nafasi mbalimbali kadri zitakavyotokea.

"Sisi Chadema tunatambua uwezo na umakini wa Profesa Safari, tutamtumia katika vikao vyetu vyote na katika kila nafasi zitakazojitokeza na zaidi tutamtumia katika nafasi za uongozi kadiri itakavyowezekana"alisema Mbowe.
Akimzungumzia Profesa Safari, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema: "Nilifanya kazi naye Dodoma, ninafahamu uwezo wake na hiyo ndiyo sababu iliyonisukuma kumpigia simu usiku na kumshawishi kujiunga na Chadema."

Profesa Safari alikuwa mwanachama wa CUF na pia mgombea uenyekiti wa chama hicho katika uchaguzi wake mkuu uliopita akichuana na Profesa Lipumba, alijitoa Januari 16, mwaka huu.
Comments




0 #5 yusuf 2011-04-02 10:29 Hakika si masihara tena.Prof Safari mwanazuoni mtukuka,mjenzi wa hoja makini, mwanademokrasia wa kweli na mvumilivu pasipo kukata tamaa.Hongera Baba kwa uamuzi murua. Tamko la Mufti Mkuu kuhusu ushiriki wa Waislamu katika maandamano na mikutano ya CHADEMA lilinisikitisha sana.Kama ulivyosema hiyo ni janja ya CCM kutumia udini kukidhoofisha CHADEMA.Wewe ni mwanasheria uliyebobea na mwislamu safi.Mufti asituchagulie viongozi wa kuwachagua.Yeye na familia yake wanafaidika na CCM.
Quote









0 #4 MPIGA KURA 2011-04-02 10:28 Karibu sana kaka mkubwa kwenye chama letu la Ukweli na Uwazi.

Hizo propaganda za Udini na Ukabila pamoja na Ukanda ni siasa za maji taka za chama cha mafisadi (CCM)kwa sababu ni kundi la wachumia tumbo
na hayo yote yako CCM kwani tunaona jinsi wanavyo lumbana wazee na UVCCM

Karibu sana Mkuuuuuuuuuu PPOOOOOOOOOOOOZ ZZZZZ
shocked.gif

Quote









+1 #3 ay 2011-04-02 10:24 Kwahakika Safari ni mstaarabu. Wengi wanapoviwacha vyama vyao na kujiunga na vyama vingine, jambo la mwanzo ni kuvitukana vyama walivoviwacha kwa [NENO BAYA] ya nguoni, lakini mtazame huyu aliyestaaraabik a. Kanifurahisha sana kujuwa na kukemea siasa za dini na ukabila. Siasa zake zinaelekea siasa za amani na kusameheana. Tunamuombea kila la kheri na pia ajitahidi kuwadhibiti wale wanaotumia dini ambao kazi zao ni za kidini na wala asiwape mwanya katika chama chake kipya hata hali ikawa kama ile ya nchi ambazo siasa zake ni kubaguwana kidini, kwani matokeo na misiba yake tunaiona. Tanzania ni ya Watanzania na visitolewe vyeo kidini bali kutokana na uwezo.
Quote









+1 #2 Mtu kwao 2011-04-02 09:48 TUNANGOJA MFANYE KAZI NA SI MALUMBANO TUNAKUTAKIA KAZI NJEMA ILIYOTUKUKA PRO. SAFARI...PEOPLESSSSSSSSS POOOOOOOOOOOWER RRRRRR
Quote









+1 #1 paulsen shijah 2011-04-02 09:45 Karibu sana, naomba uwe na Mchango mzuri Chadema, ucwe kama Mrema, kazi yake ni kuvivuruga vyama vinavyochanua, Karibu sana Baba katika Safari ya Kuikomboa Tanzania, MUNGU Ibariki Afrika, MUNGU Ibariki Tanzania.
Quote







Refresh comments list
 
Vijana CCM wazidi kuparuana


na Hellen Ngoromera


amka2.gif
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UV CCM), umezidi kuvurugana na safari hii wasomi na makada wa umoja huo kutoka vyuo vikuu wametoa kauli yao wakiujia juu uongozi wa UVCCM taifa kwa kauli yao ya kuwaponda viongozi wakuu wa CCM na kusema hawakubaliani na malumbano hayo.
Wasomi hao wameupa wiki moja uongozi huo wa UVCCM kuomba radhi kwa viongozi hao vinginevyo wataitisha maandamano nchi nzima kuwashinikiza kujiuzulu.
Makada hao wa UVCCM waliotoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam ni Agustino Matefu ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam na Stein Kiwanga, ambaye ni mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Matefu ambaye pia ni Katibu wa UVCCM Tawi la Matokeo Kata ya Mabibo Wilaya ya Kinondoni na Mjumbe wa Shirikisho la Vijana Makada wa CCM Vyuo Vikuu, alieleza kushangazwa na hatua ya viongozi hao wa UVCCM kuacha kuzungumzia mambo ya msingi badala yake wanazungumzia siasa chafu za makundi kwa manufaa ya wachache.
"Kwa niaba ya wana UVCCM na wasomi wa vyuo vikuu ambao ni makada wa CCM, hatukubaliani kabisa na kitendo chao cha kuwalaani wazee wetu kwani tunatambua mchango wao mkubwa ulioendeleza chama kutoka TANU hadi CCM," alisema Matefu.
Alisema wanashangazwa na uongozi huo wa UVCCM ngazi ya taifa kuacha majukumu ya msingi ya kikatiba na kikanuni yaliyosababisha kuundwa kwa UVCCM taifa.
Alisema hali hiyo inatia hofu juu ya uwezo wa kiuongozi na kiutendaji kwani walitegemea mengi kutoka kwa viongozi hao baada ya kuomba ridhaa kwa wana UVCCM wenyewe lakini hadi sasa hakuna walichofanya.
"Hakuna uhusiano mzuri baina ya vyuo vikuu, ukiona dalili hizi kufikia Green Guard na Chipukizi kufa, hizi ni dalili mbaya sana na haitoi taswira nzuri ya uhai wa chama na jumuiya ya vijana ambayo ndio jeuri ya chama," alisema Matefu.
Waliongeza kuwa badala ya kuweka mipango na mikakati ya kuendeleza jumuiya na chama kama kinavyofanya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanavyofungua matawi vyuo vikuu wanabaki kuwatukana viongozi.
Wasomi hao walikwenda mbali zaidi na kusema badala ya viongozi hao kumsaidia Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuibeba kauli mbiu ya Kilimo Kwanza ili iwakwamue vijana kiuchumi kwa maslai yao binafsi wamebaki wakiendeleza ushabiki na kutumiwa na watu wachache wenye malengo yao binafsi.
 
Kishindo cha CHADEMA chawavuruga CUF, CCM
• Mtatiro wa CUF aivurumishia shutuma nzito

na Waandishi wetu


amka2.gif
MAFANIKIO ya kisiasa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yanaonekana kuzidi kuwa kero kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), Tanzania Daima limebaini.
Hali hiyo ilizidi kujidhihirisha jana, baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro kuendelea kutoa matamshi yenye mwelekeo wa chuki na husuda dhidi ya CHADEMA yaliyomfikisha hatua ya kujikuta akitumia lugha isiyo na staha inayofanana na hadhi ya chama hicho cha upinzani chenye nguvu kubwa Tanzania Visiwani.
Mtatiro ambaye tangu aingie katika kiringe cha siasa za kitaifa amekuwa akifanya juu chini kupambana na CHADEMA na viongozi wake kwa namna ile ile inavyofanywa na viongozi wengine wa chama hicho, jana alieleza kusikitishwa na hatua ya CHADEMA kuamua kuunda kambi yao ya upinzani bungeni pasipo kushirikiana na wapinzani wengine.
Mtatiro ambaye katika Uchaguzi Mkuu uliopita aligombea ubunge wa Ubungo kwa tiketi ya CUF akikataa katakata ushawishi wa vijana waliokuwa wakimtaka amwachie John Mnyika wa CHADEMA, aliibuka na kuwashambulia wapinzani wenzake hao akiwapa sifa na majina mabaya.
Mtatiro na CUF wanaonekana kukerwa na tamko la CHADEMA lililotolewa juzi na Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa aliyetangaza rasmi kuunda upinzani unaojitegemea bungeni.
Akitoa tamko lililosheheni kauli za jazba, propaganda, maneno ya mitaani na matusi, Mtatiro aliishambulia CHADEMA na viongozi wake akisema lengo lao la kukataa kushirikiana na CUF ni kutaka chama hicho kife.
"Viongozi wa CHADEMA na chama chao ndio watakaokufa na kuiacha CUF ikiimarika…CHADEMA ‘ni chama popo, ndumilakuwili na wajinga," alisema Mtatiro ambaye alikwenda mbele na kuwafananisha viongozi wa chama hicho cha upinzani na Padri aliyekiuka kiapo na kukimbilia kula raha na wachumba.
Wakati akiishambulia CHADEMA, Mtatiro alisema chama chake kitaendelea kushirikiana na CCM Zanzibar kwani kilichotokea Zanzibar ndiyo matakwa halisi ya wananchi wa visiwa hivyo na kamwe hakitawalamba miguu na CHADEMA ili kushirikiana nao.
"CUF tunaamini CHADEMA wamewadharau Wazanzibari, wanawaona hawana maana, wanadharau maamuzi yao, wanaona hawawezi kufikiri na kujiamulia mambo yao wenyewe, hilo hatunalo shaka," alisema Mtatiro.
Akiendelea kuishambulia CHADEMA alisema chama hicho kiliusaliti ushirikiano wa vyama vya upinzani katika chaguzi ndogo za Tarime, Tunduru, Busanda, Mbeya Vijijini na hatimaye kusababisha uvunjike, akidai kuwa mara zote kilitaka kisimamishe wagombea wake hata katika maeneo ambako kilikuwa hakina nguvu.
Huku akionekana kuwa naye aligombea ubunge Ubungo ilhali akijua CHADEMA na Mnyika walikuwa wamejizatiti, Mtatiro alitoa maelezo ambayo yalionekana yakiwa na mwelekeo wa wazi wa kujikanganya.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa, chanzo cha kuvunjika kwa ushirikiano huo wa upinzani, ni hatua ya Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kutoa kauli zilizoonyesha kuunga kwao mkono tuhuma za kubuni dhidi ya viongozi hao wa CHADEMA kwamba walikuwa na mkono wao katika kifo cha aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Chacha Wangwe.
Maudhui na aina ya lugha ya matusi iliyotumiwa na CUF katika tamko hilo kwa kiasi fulani vilionekana kufanana na mashambulizi yaliyofanywa na Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) hivi karibuni dhidi ya CHADEMA na Dk. Slaa ambaye wamekuwa wakimwita ‘mwendawazimu' bila kufafanua.
Katika hatua nyingine inayoashiria kuzidi kuungwa mkono kwa CHADEMA na viongozi wake, jana Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alikuwa kivutio katika sherehe ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambayo rais Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi.
Mbowe alikuwa kivutio wakati akiinuka kwenye kiti alichokaa kuelekea kwenye ngazi za Mahakama Kuu kupiga picha na viongozi mbalimbali wa serikali na mahakama ambao ni watumishi wa mahakama, mawakili na wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo.
Watumishi wa mahakama pamoja na wananchi hao walisikika wakimshangilia kwa sauti ya juu "Mbowe Mbowe, Mbowe" na kiongozi huyo kulazimika kuwapungia mkono na kutabasamu.
Akitoa hotuba yake katika sherehe hizo, Rais Kikwete aliutaka mhimili wa mahakama kushirikiana na vyombo vya habari kutoa elimu kwa umma kuhusu utendaji kazi na muundo wa mahakama ukoje kwani kwa kufanya hivyo kutamuondolea adha anayoipata hivi sasa ya wananchi kufika Ikulu na kumtaka atengue hukumu mbalimbali wakilalamika kutotendewa haki.
"Wananchi wamekuwa wakijazana pale ofisini wakitaka nitengue hukumu zilizokwishatolewa na mahakama na mimi nimekuwa nikiwaambia sina mamlaka ya kufanya hivyo… wananchi hao wamekuwa wakinijibu kama siwezi kufanya hivyo watamchagua rais anayeweza kufanya hivyo na kwamba ndiyo maana wanataka katiba mpya…lakini yote hii inasababishwa na umma kuwa na uelewa finyu wa sheria na muundo wa mahakama," alisema Kikwete na kusababisha watu kuangua vicheko.
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga juzi alilazimika kutumia salamu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuwashawishi wanafunzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST) waweze kumsikiliza.
Kitwanga alilazimika kukikubali japo kwa muda Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kutokana na hatua ya wanafunzi wa chuo hicho kuguna kila alipoitaja ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi wakati akizungumza nao kuhusu inavyotekeleza sera ya elimu.
Waziri huyo alilazimika kuwasalimia wanafunzi hao akisema "CHADEMA hoyee!!, na ukumbi mzima ulizizima kwa mayowe na vifijo vya wanafunzi waliopaza sauti zao wakimjibu "Oyeeee" huku kila mmoja akimpungia alama ya vema kwa kuonyesha vidole viwili.
Kitendo cha Waziri Kitwanga kutumia jina la CHADEMA katika kibwagizo hicho kilitokana na hatua ya wanafunzi hao kuguna pale alipoanza kujibu maswali yao kwa kusema "katika Ilani ya ya CCM….." bila kumalizia kusema alishtushwa na miguno.
 
Wasomi waishushua UVCCM
• Wafichua serikali inavyokwamisha mikopo kwa wanafunzi

na Waandishi wetu


amka2.gif
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeendelea kupingwa kwa hatua yake ya kutoa tamko linalotaka Bodi ya Mikopo (HELSB) ivunjwe bila kueleza njia mbadala ya kumaliza matatizo ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini.
Jana wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini kupitia kwa mwakilishi wao katika bodi hiyo, Chitage Edwin, walitoa rasmi msimamo wa kupinga tamko la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) la kutaka Bodi ya Mikopo (HESLB) ivunjwe na badala yake wamefichua kuwa serikali ndiyo inayopaswa kulaumiwa na kuwajibika kwa kusababisha matatizo ya mikopo kwa wanafunzi.
Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) hivi karibuni walinukuliwa wakitoa tamko lao la kutaka Bodi ya Mikopo (HESLB) ivunjwe kwa madai ya kukwamisha na kuchelewesha utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini huku wakisisitiza kuwa isipovunjwa watafanya maandamano yatakayohakikisha inavunjwa.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, mwakilishi wa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu katika bodi hiyo, Chitage Edwin, alisema wao kama wasomi fikra zao zipo tofauti kabisa na fikra potofu za UVCCM wanaotaka bodi hiyo ivunjwe wakati matatizo yote yamesababishwa na serikali yenyewe.
Alisema utaratibu mbaya wa serikali kutenga na kutoa pesa kidogo kwenda Bodi ya Mikopo (HESLB) ndio uliosababisha kwa kiasi kikubwa matatizo ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.
"Fedha inayotengwa na serikali haikidhi mahitaji, kwa sababu hiyo idadi kubwa ya wanafunzi wenye sifa ya kusoma elimu ya juu hawapati mikopo, kwa mfano wanaopata daraja la tatu hawapati mikopo isipokuwa tu wanaposoma ualimu na masomo ya sayansi.
"Hata hao wanaopata mikopo bado wanawekwa katika madaraja, kwa bahati mbaya sana hakuna mazingira yanayowezesha kufahamu kwa usahihi uwezo wa kiuchumi wa kila mwombaji.
"Pia ni utaratibu mbaya wa serikali kutoa pesa kidogo kidogo kwenda bodi ya mikopo," alisema mwakilishi huyo.
Wakipinga zaidi kile walichokiita "hatua ya vijana wa CCM kutaka kuugeuza mgogoro wa mikopo kuwa turufu yao ya kisiasa", mwakilishi huyo alisema jambo linalopaswa kufanyiwa kazi ni mfumo mzima wa utoaji wa mikopo na upungufu wake, ambao mhimili wake ni serikali kupitia Wizara ya Elimu ya Juu na Hazina.
Akiukosoa mfumo huo, alisema kukosekana kwa usimamizi na udhibiti wa ada kwa wanafunzi kumetoa mwanya kwa mamlaka ya vyuo kupandisha ada kiholela, jambo ambalo lingeweza kudhibitiwa kama serikali ingekuwa makini.
Akiwasilisha mapendekezo ya nini kifanyike ili kutatua matatizo yaliyopo, alisema: "Serikali iweke utaratibu utakaowezesha fedha za mikopo kuifikia bodi kwa haraka kwa kiasi cha kutosha, iwe na dira iliyo wazi juu ya malengo ya taifa hususan katika idara ya wataalamu katika fani mbalimbali.
"Izingatie kuongeza fedha za kujikimu sambamba na mahitaji mengine kwa sababu ya kupanda kwa gharama za maisha.
"Iweke utaratibu wa usimamizi na udhibiti katika viwango vya ada za wanafunzi, iwajumuishe wanafunzi waliopata daraja la tatu wenye sifa za kusoma chuo kikuu wapate mikopo na iache kutoa mikopo kidogo kidogo."
Wakati huo huo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga, juzi alilazimika kutumia salamu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuwashawishi wanafunzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST) waweze kumsikiliza.
Kitwanga alilazimika kukikubali japo kwa muda Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokana na hatua ya wanafunzi wa chuo hicho kuguna kila alipoitaja ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi wakati akizungumza nao kuhusu inavyotekeleza sera ya elimu.
Waziri huyo alilazimika kuwasalimia wanafunzi hao akisema: "CHADEMA hoyee!!" Na ukumbi mzima ulirindima kwa mayowe na vifijo vya wanafunzi waliopaza sauti zao wakimjibu: "Oyeeee" huku kila mmoja akimpungia alama ya vema kwa kuonyesha vidole viwili.
Kitendo cha Waziri Kitwanga kutumia jina la CHADEMA katika kibwagizo hicho kilitokana na hatua ya wanafunzi hao kuguna pale alipoanza kujibu maswali yao kwa kusema: "katika manifesto ya CCM….." bila kumalizia kusema alishtushwa na miguno.
Akionyesha wazi kuwa amezisoma nyuso za wanafunzi hao, waziri huyo alibadili mwelekeo naye na kuwasalimu kwa salamu hiyo ya CHADEMA.
Baada ya hapo aliwataka wanafunzi hao waanze kueleza kero na changamoto zinazowakabili ambapo alisimama Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi ambaye alieleza kero inayowasumbua kuwa ni pamoja na chakula kinachotolewa si kizuri na hakina usalama.
"Hapa tuna tatizo la chakula kwani tunapewa chakula ambacho hakilingani na kiwango halisi na wakati mwingine tunapewa nyama ambayo tayari imeharibika, hivyo tunashauri tuwe tunapewa fedha ili tujitafutie chakula wenyewe," alisema.
Mwanafunzi Jacob Mambo alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa maabara za taasisi hiyo zimechoka, haziendani na mfumo wa sasa, maktaba iliyopo haitoshelezi na miundombinu yake sehemu kubwa imechakaa.
"Tunashindwa kuielewa hii serikali yetu kwani tunaeleza matatizo yetu tunaambiwa serikali haina pesa, sasa hizo fedha za kuilipa Dowans zinatoka wapi?" alihoji Mambo.
Mwananfunzi mwingine, Charles Gabriel, alisema kuwa hali ya mabweni ya wanafunzi ni mbaya na kwamba wamekuwa wakilipwa fedha pungufu kwa ajili ya kwenda kwenye mazoezi ambapo mwaka jana kilitolewa kiasi cha sh 360,000 badala ya sh 444,000 tofauti na Taasisi ya Arusha ambayo wanapewa kiasi cha sh 480,000.
Akijibu kero hizo, Naibu Waziri huyo alianza kwa kusema kuwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, lakini kabla ya kuendelea kilianza kizaazaa cha wanafunzi kupaza sauti na kubeza wakisema: "Aaaaaaa!….Aaaaaaa!" Hali iliyomfanya waziri huyo ajikute akinadi salamu ya CHADEMA kwa kusema: "CHADEMA Oyee!" Ndipo wanafunzi zaidi ya 1,000 waliokuwa kwenye ukumbi huo wakaitikia kwa kupaza sauti: "Oyee!" Huku wakipiga makofi na kumpungia alama ya chama hicho ya vidole viwili.
Waziri huyo aliwataka wanafunzi hao kuwa na subira ingawa ni kweli taasisi hiyo ina tatizo la vitendea kazi.
Pia alikiri kuwa fedha zinazotolewa kwa ajili ya mahitaji ya chakula ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi na kuahidi kuwa serikali itajitahidi kuhakikisha kero hizo zinakwisha kwa wakati.
Baada ya kumaliza mkutano huo, Kitwanga alilazimika kutembelea mabweni ili kuweza kujionea hali halisi huku wanafunzi wakimzonga na kusema: "Bado huku, bado chooni." Kitendo ambacho hakusita kwenda sehemu zote alizotajiwa na wanafunzi hao.
 
Jeshi la Polisi lisitumike vibaya
ban.mtazamo.jpg


Abdallah Khamis​

amka2.gif
JESHI la Polisi ni chombo muhimu kilichowekwa kwa ajili ya kulinda usalama wa raia na mali zake.
Jeshi hilo lina wajibu wa kuhakikisha wananchi wote wanaishi kwa usalama kwa kutegemea ufanisi bora pasipo kuangalia uzito wa mtu au taasisi anayotokea.
Lakini chombo hicho kinapotumika kama ofisi ya mtu binafsi na kwa masilahi ya upande mmoja linapoteza sifa ya kuwepo kwa ajili ya usalama wa raia na mali zake.
Nasema hivyo kwa ajili ya matukio yaliyoripotiwa kutokea hivi karibuni juu ya kuvurunda kwa jeshi hilo katika wajibu wake wa usalama wa raia na mali zao.
Baada ya kuanzisha vurugu mkoani Arusha katika uchaguzi wa meya wa jiji hilo lililosababisha vifo vya watu watatu, kuna madai mengine yaliripotiwa pia kutokea jijini Mwanza.
Yalihusu askari wa jeshi hilo wa Kituo kidogo cha Mirogo jijini Mwanza kumuua mtuhumiwa kwa kipigo kwa kile kinachodaiwa kumshinikiza aseme alipoficha fedha alizoiba kwa mwajiri wake.
Nikianza na tukio la Arusha kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Thobias Andengenye, ni kwamba hata yeye alibariki tukio la kupigwa kwa mwakilishi huyo wa wananchi.
Kamanda huyo alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kwamba Mbunge Godbless Lema (CHADEMA) aliyepigwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha (OCD) alijitakia yeye mwenyewe huku akisahau kuwa hakuna mwenye mamlaka kisheria ya kuweza kumsababishia madhara mtu mwingine.
Ni aibu kwa OCD huyo ambaye binafsi naamini mpaka kufikia kupewa nafasi hiyo si bahati mbaya, ila ni uwezo wake wa kulinda na kutetea haki anapokuwa wa kwanza kuunyoosha mkono wake kwenda kumdhuru mtu mwingine.
Je, walio chini yake wajifunze nini kwake na nani atawakemea ikiwa bosi wao hawi mfano mzuri wa amani?
Nakusihi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, kuliangalia suala hilo kwa kina, kwani linakupotezea sifa ya utendaji mzuri.
Hali hiyo inaonyesha pia kwamba baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi hawajui wajibu wao.
Mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi katika eneo lake ana haki ya kuingia katika baraza la madiwani na kupiga kura, sasa anapokuja mtu kwa masilahi yake na kumkataa mwakilishi huyo halali na kumwacha asiyehusika ni tatizo la kimfumo ambalo ni lazima litiliwe shaka.
Jeshi la Polisi lilikuwa na nafasi ya kujenga heshima yake katika tukio hilo, kwani ni suala rahisi kuupima ukweli kuhusu tukio hilo kwamba ni aina gani na vurugu zipi zilizoripotiwa kwao na Mkurugenzi wa manispaa hiyo.
Napata shaka kwamba sababu ya hali hiyo ni uwepo wa mbunge huyo ndani ya ukumbi au kitendo cha mkurugenzi kutaka kumruhusu anayedaiwa kuchomekwa ili apige kura ilhali hakuwa na sifa ya eneo husika.
Hali hiyo ingesaidia kuepusha vurugu walizokuja kuzianzisha na kumfedhehesha mbunge mbele ya wapiga kura wake.
Pamoja na yote, nawapa pongezi Watanzania kwa ustaarabu wa kondoo walionao kutembea vichwa chini, vinginevyo yangekuwa yanaongelewa mengine sasa kwa masilahi ya wachache.
Tukio jingine lililotokea Mwanza kuhusu madai ya askari kumuua raia ni ushahidi tosha wa utendaji mbovu wa jeshi hilo.
Kwa mtazamo wangu, jeshi hilo halina sababu ya kukwepa lawama hizo na ni dhahiri kwamba haya ni matukio machache kati ya mengi yanayotokea kila siku.
Ifike wakati tuwaone polisi kuwa ni msaada kwa raia wote na kamwe wasitumike kwa masilahi ya kikundi fulani au kwa masilahi ya watu binafsi.
Ikiwa jeshi hilo litatekeleza hayo, itafika mahali kila mwanajamii atakuwa ni msaada kwa jeshi hilo, hivyo kulifanya kuwa rafiki wa kila mwananchi.
Natoa pole kwa walioondokewa na jamaa zao katika tukio la mauaji ya Arusha na Mwanza, pia nampa pole Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema pamoja na wapiga kura wake.
Ikiwa hali ya machafuko itaendelea nchini itasababisha usalama wa wananchi kuwa shakani.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki mioyo ya uvumilivu ya Watanzania.



h.sep3.gif

Kwa maoni andika kwa barua pepe: abdallahkhamis2009@gmail.com 0755/0655 54 91 54
 
Ya Misri, Tunisia yawe funzo kwa serikali

ban_tahariri.jpg

amka2.gif
WIMBI la maandamano kupinga ukiukwaji wa haki, matumizi mabaya ya madaraka na madaraka yasiyo na ukomo yanayobebwa na mfumo mbaya wa kikatiba na kisheria, linaonekana kushamiri kwa kasi barani Afrika.
Wimbi hilo lililotikisa nchi ya Tunisia hivi sasa linaendelea nchini Misri kwa maandamano makubwa yaliyoungwa mkono na watu takriban milioni moja nchi nzima, yakishinikiza kung'olewa kwa Rais Hosni Mubarak, aliyetawala nchi hiyo kwa kipindi kirefu.
Itiliwe maanani kuwa maandamano hayo ya Misri sasa yameingia siku ya kumi huku yakiwa yamesababisha madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na vifo vya zaidi ya watu 300.
Shughuli za maendeleo, kazi, masomo na usafiri nchi nzima hivi sasa zimesimama Misri kwa sababu ya vuguvugu hilo la maandamano ya kupinga utawala.
Kwa namna yoyote ile kilichotokea Tunisia na kinachoendelea kule Misri ni mambo ambayo hayapaswi kupita bila kujadiliwa na Watanzania na hasa viongozi walio madarakani na wanasiasa, kwani yote yanahusu mgogoro kati ya watawala na watawaliwa ambao hata hapa kwetu wapo.
Malalamiko ya hali ngumu ya maisha (ukosefu wa ajira) na ukiukwaji wa haki mbalimbali pamoja na upungufu wa kikatiba, ni masuala ambayo hapa kwetu yapo na yamekuwa yakilalamikiwa kwa muda mrefu bila hatua madhubuti kuchukuliwa.
Kwa mantiki hiyo, tukiwa chombo cha habari chenye wajibu wa kuhabarisha na kuelimisha, tunaamini kile kilichotokea na kinachoendelea kutokea katika nchi hizo kinaweza pia kutokea hapa kwetu Tanzania na madhara yake yakawa makubwa sana.
Izingatiwe kuwa baada ya madhara makubwa kutokea kule Misri na watu wengi kupoteza maisha yao, sasa Rais wa nchi hiyo, Hosni Mubarak, ndiyo ameanza kusikiliza vilio vya siku nyingi vya wananchi, kwa kuanza kuchukua hatua mbalimbali za kunusuru hali ya uchumi, kikatiba na utendaji mbovu wa serikali yake.
Kwa mujibu wa rais huyo, akihutubia taifa lake kupitia televisheni juzi, sasa hatagombea tena urais Septemba mwaka huu na ameagiza viongozi wenzake kuanza kufanya mabadiliko ya kikatiba ikiwa ni pamoja na kuweka ukomo wa kugombea urais.
Sasa ndiyo anajaribu kutuliza ghasia kwa kuahidi mabadiliko ya kisiasa na kuagiza Waziri Mkuu mpya, Ahmed Shafiq, kuharakisha mabadiliko ya kidemokrasia ili kubuni nafasi mpya za kazi.
Tukiyatilia maanani yote hayo, tunatoa rai kwa serikali kuona kuwa ina kila sababu ya kuharakisha mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya ili yasije kutufika yanayoifika Misri hivi sasa.
Tunajua Rais Kikwete ameshaonyesha nia hiyo lakini haitoshi – Serikali, Bunge, wanaharakati na wananchi wote kwa ujumla tuhakikishe mchakato wa Katiba unaanza haraka na kukamilika mapema ili kuepusha uwezekano wa nchi yetu kuingia kwenye machafuko. Tunasisitiza.
 
UVCCM wataka mafisadi wafukuzwe uanachama Send to a friend Sunday, 03 April 2011 20:43

Geofrey Nyangóro
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UV-CCM), Martine Shigela amepokea mapendekezo ya vijana wa Tawi la Matangini, Kimara jijini Dar es Salaam kwamba wtuhumiwa kwa ufisadi akiwamo waliokuwa mawaziri na wabunge wa sasa, kufukuzwa uanachama ili kurejesha imani ya chama hicho kwa wananchi.

Akizungumza baada ya kusomewa risala hiyo Shigela alisema anaungana na vijana hao kwa asilimia mia moja na kwamba viongozi wasio na maadili ni mafisadi na mwisho wao umekaribia.

Shigela alisema chama hicho hivi sasa kina mafisadi na wamekuwa wakikiuka maadili kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa na kwamba kinachofanyika sasa ni kuangalia namna ya kukisafisha chama hicho kuanzia ngazi ya chini.

Kuhusu maandamano ya Chadema alisema umoja huo haupaswi kukaa kimya na wao wana haki ya kuandaa maandamano kupinga Chadema isifanye maandamano kushinikiza uchaguzi wa Meya Arusha, urudiwe.

Awali akisoma taarifa hiyo yenye kurasa 11 katika mkutano wa tawi, uliofanyika juzi Kimara Matangini, Katibu wa UV-CCM wa tawi hilo Asenga Abubakar alisema vigogo hao wamechangia kuiweka CCM katika hali mbaya kutokana na tuhuma za ufisadi.
"Kama tunakipenda chama, lazima tuseme ukweli na chama kijivue gamba kama alivyosema Mwenyekiti Rais wetu Dk Jakaya Kikwete kwenye mkutano wa kusherehekea miaka 34 ya CCM.

"Tunashauri uchunguzi wa kina ufanyike katika ushiriki wao katika mikataba ya kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, Dowans, mkataba wa madini wa Buzwagi, ununuzi wa Rada na Ndege ya rais kwani ni aibu kubwa kwa baadhi ya watu hawa kuendelea kuwa wajumbe wa kamati kuu na ile ya maadili, achilia mbali uanachama wa CCM,"alisema.

Vijana hao walishauri chama kuunda kitengo cha uchunguzi juu ya mwenendo wa wanachama wao na vigogo na kusema kweli juu ya majibu na matatizo yanayoikabili CCM.

Alisema idadi ya watu wanaokichukia chama imezidi kuongozeka na hilo ni kutokana na wananchi kutoridhishwa na mambo yanayotokea katika uongozi wa juu wa chama hicho.

Kuhusu uongozi wa juu vijana hao waliwatupia lawama kuwa kitendo chao cha kubadili majina ya wagombea na kuwaacha wagombea wanaokubalika kwa wananchi ni chanzo cha wananchi kuichukia CCM.

Akizungumzia hali ya kisiasa Abubakari alisema ni mbaya na imevurugwa wakati wa kura za maoni.
 
Vijana CCM wazidi kuraruana


Na Mwandishi Wetu

SIKU chache baada ya Baraza la Umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Arusha kutangaza kumfukuza Mjumbe wa Baraza la Vijana Taifa, Mrisho Gambo, yeye ameibuka
jana kupinga uamuzi huo, akisema hawana mamlaka hayo.

Bw. Gumbo alivuliwa wadhifa huo kwa tuhuma za kuunga mkono vyama vya upinzani na kusababisha Jimbo la Arusha lichukuliwe na mbunge kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Hatua hiyo ilitangazwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Arusha, James Millya, kuwa uamuzi wa kumfukuza umetokana na tuhuma na taarifa zenye ushahidi kuwa Gambo amekuwa ni kiini cha kukivuruga chama na kushawishi vijana wa CCM kuchagua upinzani.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Bw. Gumbo alisema, "Ninataka kuwafahamisha Watanzania wajue kuwa UVCCM-Arusha hawana mamlaka ya kikanuni wala kikatiba kunivua madaraka, nimeona nizungumze ili historia isije kusema nilifukuzwa".

Alisema yeye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa na mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, kwa mantiki hiyo uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na ambayo kwa mujibu wa Katiba ya CCM ndiyo yenye mamlaka ya kumvua uongozi.

Mbali na tamko hilo, Bw. Gumbo alisema anaandamwa ndani ya umoja huo kutokana na kauli yake kuwa kashfa za Richmond na Dowans zimeipunguzia CCM kura katika uchaguzi mkuu uliopita.

"Kabla ya kikao cha Vijana Arusha (kilichomvua wadhfa)nilipokea simu kwamba watanimaliza kutokana na kauli yangu kuwa 'Richmond na Dowans vimeiupunguzia kura CCM' hivyo watanishughulikia," alisema.

Alisema wakati kikao hicho hakijafanyika maamuzi dhidi yake yalikuwa yameshatolewa, hivyo kilifanyika wilayani Longido kwa ufadhili wa baadhi ya wanasiasa kuyabariki.

Alifafanua kuwa kikao hicho na kiliisha saa 2 usiku lakini maazimio yake aliyapata saa 9 mchana baada ya kikao chao cha kwanza kilichofanyika katika Hoteli ya Impala, mjini Arusha.

Kijana huyo ambaye amejitokeza waziwazi kupinga kauli za karibuni za viongozi wa jumuiya hiyo dhidi ya wastaafu wanaoikosoa CCM, alisema vitendo anavyofanyiwa ni njama za kumziba mdomo ili asiseme ukweli.

"Hoja kuu eti ilikuwa sikumpigia kura Batilda (Burian) lakini wanasahau kuwa kura ni siri na hakuna mwenye mamlaka ya kuhoji. Niliposikia hoja hiyo nikawauliza wana uthibitisho gani? Maana hata mke wangu sikwenda naye hivyo wao wamejuaje?.

"Tatizo ukiwa mpiga kelele dhidi ya ufisadi basi unatafutiwa namna yoyote ya kumalizwa. Umefika wakati wa kuacha kufanya kazi za watu na kufanya kazi za umma; ningependa vijana ndani ya CCM wajue hilo, Watanzania wa sasa ni wa DOT COM, alisema.

Alitoa rai kuwa wote wanaotuhumiwa wa kashfa za Richmond na Dowans washughulikiwe, hakuna haja ya kuumauma maneno. "Ukiwa mnafiki kijana, basi utakuwa mchawi ukizeeka. Mimi nitasema ukweli daima, fitna kwangu mwiko," alisema.
 
Wabunge 'mabubu' wanyooshewa kidole


*Utafiti wabaini wako hatarini kupoteza nafasi zao

Na Tumaini Makene

UTAFITI uliofanywa juu ya utendaji kazi wa wabunge, katika bunge la tisa, umetoa tahadhari kwa wabunge wa bunge la 10 wasiochangia kukaa
mkao wa kutorudi bungeni, huku vyama vyao vikihadharishwa kuwa vitaadhibiwa kwa kuzidi kupoteza wawakilishi.

Tahadhari hiyo imetokana na utafiti huo kubaini kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, moja ya vigezo ambavyo wapiga kura walivitumia ilikuwa ni kuzingatia kiwango cha ushiriki wa wabunge katika bunge la tisa.

Kutokana na kuzingatia kiwango hicho cha kushiriki katika kuchangia mijadala, chama kilichokuwa na ushiriki mdogo bungeni, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeonekana kuadhibiwa kwa kupoteza viti vingi, ambapo chama kilichokuwa na ushiriki mkubwa bungeni (CHADEMA) kimefanikiwa kuongeza viti.

"Kidokezo kinachojitokeza katika matokeo haya kwa bunge la 10 ni kwamba vyama vya siasa vyenye nia ya kukua katika siku zijazo vitahitaji kuwahimiza wabunge wao kuwa washiriki wazuri katika shughuli za bunge," imesema sehemu ya utafiti huo uliofanywa na asasi binafsi maarufu ya Uwazi, iliyoko chini ya Twaweza.

Asasi hiyo ambayo imeshafanya tafiti mbalimbali, zilizoibua mijadala mikubwa nchini, ikiwa ni changamoto kwa wahusika, kama ule wa wahitimu wa darasa la saba kutoweza kumudu masomo ya darasa la pili, imetumia tovuti ya bunge katika kukusanya takwimu za taarifa yake hiyo.

Katika taarifa yake hiyo, ambayo Majira linayo nakala yake, Twaweza imesema kuwa zaidi ya nusu ya wabunge wa kuchaguliwa waliokuwepo katika bunge la 9 hawakurudi bungeni baada ya uchaguzi wa Oktoba 2010;

Huku pia wabunge ambao hawakuwa mawaziri au watumishi wenye nyadhifa za juu serikalini walikuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kutorudi bungeni, ambapo ni asilimia 35 pekee ya wabunge wa kawaida wamerudi katika bunge la 10.

Katika ripoti hiyo iliyopewa jina la 'Nani amerudi? Utendaji katika bunge na uwezekano wa wabunge kuchaguliwa kwa mara nyingine,' imesema kuwa chini ya nusu ya wabunge wa kuchaguliwa wamerudi tena bungeni mwaka 2010, huku wengi wao wakiwa ni waliokuwa na ushiriki mkubwa zaidi kuliko wale ambao hawakurudi.

"Muhtasari huu unaonesha kwamba nusu ya wabunge wa kuchaguliwa wamerudi tena bungeni katika mwaka 2010 na kwamba ni theluthi moja tu ya wabunge wa kuchaguliwa ambao si watumishi wenye nyadhifa za juu katika serikali waliofanikiwa kubaki na viti vyao.

"Unaonesha kwamba wabunge wa kuchaguliwa wa kawaida waliorudi bungeni ni wale waliokuwa na ushiriki mkubwa zaidi... Vile vile, muhtasari unaonesha kwamba vyama vya siasa vyenye wabunge wenye ushiriki mkubwa katika bunge vilipata viti vingi zaidi...;

"Katika uchaguzi wa Oktoba 2010 wakati chama chenye wabunge ambao hawakuwa na ushiriki mkubwa bungeni kilipoteza viti. Kwa pamoja, mambo haya yanaashiria kuwa utendaji wa wabunge ndani ya bunge una umuhimu mkubwa kwa wapiga kura," imesema sehemu ya taarifa ya utafiti huo.

Bunge la tisa, lilikuwa na wabunge wa kuchaguliwa wapatao 231, ambapo kati yao 100 ndiyo wamerudi, huku 131 (sawa na asilimia 57) hawakurudi.

Katika bunge hilo CCM kilikuwa na wabunge 186, CUF kilikuwa na wabunge 33, CHADEMA wabunge 11 na UDP mbunge mmoja. Wakati katika bunge la sasa, CCM kina wabunge 259, CHADEMA (48), CUF (36), NCCR-Mageuzi (4), UDP (1) na TLP (1).

Pia wabunge ambao ni mawaziri na watumishi wengine wenye nyadhifa za juu serikalini (kama vile spika, naibu spika, mwanasheria mkuu wa serikali na wakuu wa mikoa) walikuwa na nafasi nzuri zaidi ya kurudi bungeni kuliko wabunge wa kawaida.

"Asilimia 80 (ambao ni 35 kati ya 44) ya wabunge wa kuchaguliwa waliokuwa watumishi wenye nyadhifa za juu serikalini walichaguliwa, ambapo asilimia 35 tu (sawa na wabunge 65 kati ya 187) ya wabunge wa kawaida walirudi bungeni baada ya uchaguzi wa 2010," imesema ripoti hiyo.

Vyama vya CUF na CCM vilikuwa na asilimia kubwa zaidi ya wabunge ambao hawakurudi, ambapo asilimia 66 ya wabunge wa kawaida wa CCM hawakurudi bungeni baada ya uchaguzi, huku wabunge wa namna hiyo asilimia 67 kwa upande wa CUF nao pia hawakurudi, huku UDP na CHADEMA vikiwa na idadi ya chini zaidi katika kundi hili.

"Chama cha UDP ambacho mbunge wake pekee alirudi bungeni na CHADEMA (asilimia 40) ndivyo vilivyokuwa na asilimia za chini zaidi za wabunge wa kuchaguliwa wa kawaida ambao hawakurudi bungeni baada ya uchaguzi 2010."

Kwa mujibu wa utafiti wabunge wengi ambao hawakurudi bungeni baada ya uchaguzi mkuu walikuwa na ushiriki mdogo, ikioneshwa kuwa waliorudi walitoa wastani wa michango 92 ndani ya miaka mitano, wakati 'waliobwagwa' walichangia wastani wa michango 81.

"Kati ya wabunge wa kuchaguliwa wa kawaida 187 katika bunge la tisa, 65 wamerudi wakati 122 hawakurudi. Wastani wa michango iliyotolewa na wabunge waliorudi ilikuwa juu kidogo kuliko ile iliyotolewa na wabunge ambao hawakurudi.

Utafiti huo umekielezea CUF kuwa ndiyo chama pekee kilichorudisha bungeni wabunge wake wengi wenye ushiriki mkubwa, ambapo kwa tathmini ya ushiriki kichama iliyofanywa na Uwazi inaonesha kuwa chama hicho kimefanikiwa kurudisha wabunge wake wengi waliochangia sana.

"Iwapo mtu atathmini kiwango cha ushiriki wa wabunge waliorudi na wale ambao hawakurudi ki-chama, ataona kwamba ni CUF pekee ndiyo iliyorudisha bungeni wabunge wake wengi waliokuwa na ushiriki mkubwa. Wabunge 6 wa CUF waliorudi walichangia hoja kwa wastani wa mara 116...;

"Ambapo wabunge 12 ambao hawakurudi walichangia hoja wastani wa mara 72...CCM na CHADEMA hakuna tofauti kubwa katika idadi ya michango kati ya wabunge waliorudi na wale ambao hawakurudi. Wabunge 55 wa CCM waliorudi walichangia wastani mara 83...

"Ambapo wabunge wa CCM 108 ambao hawakurudi walichangia kwa wastani wa mara 80. Wabunge 3 wa CHADEMA waliorudi walichangia hoja kwa wastani wa mara 174, ambapo wabunge 2 ambao hawakurudi walichangia hoja mara 173.".

Chama kilichokuwa na wabunge wenye ushiriki mdogo bungeni kilipoteza viti katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ambapo utafiti huo umeonesha kuwa wabunge wa CUF na CCM kwa kiasi fulani walikuwa na ushiriki mdogo, ambapo wale wa CUF walichangia mara 87 na wabunge wa CCM walichangia kwa wastani michango 80.

Utafiti huo umesema kuwa chama kilichokuwa na wabunge wenye ushiriki mkubwa bungeni katika bunge la tisa kilifanikiwa kuongeza viti katika uchaguzi mkuu uliopita, ambapo wabunge wa kawaida wa CHADEMA, ndiyo waliochangia zaidi kwa wastani wa hoja mara 173.

"Chama kilichotoa michango mingi bungeni (CHADEMA), kiliongeza asilimia ya wabunge kwa zaidi ya mara nne, kutoka asilimia 2 mpaka 9. Kwa upande mwingine chama chenye ushiriki mdogo zaidi (CCM) kilipunguza asilimia 89 hadi 78.

"CUF chama ambacho kilikuwa na ushiriki zaidi ya ule wa wabunge wa CCM, kiliongeza kidogo asilimia yake ya wabunge kutoka asilimia 8 hadi 10. Matokeo haya yanaelekea kukubaliana na maoni kwamba wapiga kura wanazingatia kiwango cha ushiriki wa wabunge wakiwa bungeni, wakati wanapoamua chama kipi wakipigie kura."
 
PHP:
Naisubiri siku ya ukombozi, freedom is coming tomorrow:yield:

You are not alone...................
 
Zitto 'awachomea utambi' wajumbe wa bodi Send to a friend Wednesday, 06 April 2011 21:57

Midraji Ibrahim, Dodoma
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Zitto Kabwe, amesema agizo la Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuondoa wabunge kwenye bodi mbalimbali za mashirika, halijatekelezwa na serikali.

Lakini wakati Kabwe akiilaumu serikali kwa kushindwa kutekeleza agizo hilo, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, alisema hiyo ni nongwa ya wapinzani.Kabwe alisema miongoni mwa mambo yanayotatiza ufanisi katika mashirika ya umma, ni kutowajibika ipasavyo kwa bodi za wakurugenzi wa mashirika, zilizokabidhiwa jukumu la kuhakikisha kuwa utendaji unakuwa na ufanisi.

Akiwasilisha taarifa ya kamati yake bungeni jana, Kabwe alisema imebainika kuwa katika baadhi ya mashirika, wajumbe wa bodi wamekuwa hawazisimamii ipasavyo menejimenti."Sasa ni muda muafaka kwa serikali kuingia mikataba ya utendaji na wajumbe wa bodi za mashirika ili kupima utendaji wao kwenye bodi husika na pale pasipokuwa na ufanisi, waondolewe,"alisema.

Hata hivyo akichangia taarifa hiyo, Serukamba alisema wajumbe wa bodi si watendaji wa mashirika na kwa msingi huo, hawawezi kukwamisha ufanisi.

Serukamba alisema wajumbe wa bodi wakiwamo wabunge, wana utaalamu unaoweza kusaidia mashirika kuongeza ufanisi. Mbunge huyo ni mjumbe Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

"Kinachotakiwa nin kwamba hawa wajumbe wachaguliwe kwa vigezo hata kama ni Chadema ana mchango mzuri, tuondoe hii nongwa," alisema Serukamba.

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, alisema wananchi wanafungwa na kunyang'anywa mali zao kwa nguvu wakitakiwa kuchangia maendeleo, ilhali kuna fedha za serikali zisizotumika.

Lissu alisema mwaka 2009, zaidi ya Sh3 bilioni zilitakiwa kupelekwa vijijini, lakini hakuna hata senti tano iliyopelekwa huku wakurugenzi wa halmashauri wakirejesha fedha kwa kukosa kazi za kufanya.

"Wananchi wameendelea kuchangishwa kwa nguvu ilhali kuna fedha zinazotengwa kwa ajili ya maendeleo na zinarudishwa serikalini kwa kukosa matumizi," alisema Lissu.
 
well

hii iko hivi uyo pinda hayo maendeleo lazima yaweko ina maana huo ni wajibu wa serikali na kazi pia tumewachoka CCM yaani hata wakitoa ruzuku kwa wananchi hatuwataki:angry:
 
:A S 2152:who is serukamba??????

yani CCM ina mabongo lala surukamba, simba chawenu, mkulo lofa, hawa sio watendaji jamani
 
Hivi hili la Chadema kuandamana nchi nzima kudai katiba mpya shirikishi CCM isimtafute mchawi ila ikiri ya kuwa uongozi wa JK ni bomu......................katika karne ya 21 Raisi hawezi kuendelea na madaraka yale aliyoachiwa na mkoloni kupitia gavana...........yaani presidential monarchy.............................................Raisi kuwa mwanzo na mwisho wa kila kitu.......................that was yesterday.....................................na JK kukosa utashi wa siasa za vyama vingi na kuwa alilelewa ndani ya mfumo wa chama kimoja ndiyo maana hata mchakato wa katiba mpya wa Kenya haukumpa nafasi ya kujifunza lolote lile....................................How pathetic.................
Chadema kuandamana nchi nzima

Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 8th April 2011 @ 23:58 Imesomwa na watu: 48; Jumla ya maoni: 0








VIONGOZI wote wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiwemo wabunge, Aprili 16 wataungana na wafuasi wa chama hicho kuandamana nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi kuhusu namna bora ya kuendelea na mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya Tanzania.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amewaeleza waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, kuwa, wafuasi wa chama hicho wataandamana katika makao makuu ya mikoa kama Serikali itaendelea kuharakisha mchakato wa mabadiliko ya Katiba.


"Tuna haraka gani jamani?"amehoji Mbowe na kubainisha kwamba, wabunge wote wa Chadema watatawanyika nchi nzima kufanikisha maandamano hayo.


Amesema, Chadema wanakwenda kwa wananchi ili waseme wanataka muundo gani wa sheria ya mabadiliko hayo ya Katiba ya nchi.


"Sio mikutano ya Chadema, sisi tunajitolea kupata maoni ya wananchi" Amesema Mbowe baada ya kipindi cha maswali na majibu na akaongeza kuwa siku hiyo pia kutakuwa na mikutano ya hadhara katika mikoa yote Tanzania.


Kwa mujibu wa Mbowe, Chadema watatoa taarifa polisi kwa kuwa hawahitaji kuomba kibali cha kuandamana na akasema, "Na tutaiomba Serikali itulinde"

Amesema, Serikali ikiacha kuharakisha mchakato huo, Chadema hawataandamana Aprili 16, ila wanaweza kufanya hivyo kuipongeza.

Amesema, wamekuwa wakidai mabadiliko ya Katiba ya nchi kwa takribani miaka 20, hivyo kuwezi kuibadilisha kwa wiki moja.


Kiongozi huyo wa Kambi ya Upinzani bungeni, amesema , kati ya sasa hadi Bunge la Juni kuwe na utaratibu wa kupata mawazo ya wananchi, hivyo hakuna umuhimu wa kuharakisha mchakato huo wa mabadiliko ya Katiba.


Mbowe amesema, Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiendelea kushinikiza mchakato uendelea kama ilivyo sasa, na kuupitisha muswada kwa namna ulivyo, Chadema watafanya kazi za siasa nje ya Bunge.


"Hii ni mood ya taifa mzee lazima uelewe" amesema Mbowe na kuitaka CCM isome alama za nyakati na akadai kuwa, nchi ipo kwenye mashaka hivi sasa.

Mbowe amesema, Chadema wanawawakilisha wananchi, na wana hoja za msingi, zikikataliwa Bungeni watarudi kwa wananchi ili waamue.

Amesema kuna mapungufu mengi katika muswada wa mabadiliko ya Katiba, lakini Serikali inapaswa kutambua kuwa Katiba si mali yake, si mali ya Rais , si mali ya CCM, ni mali ya Watanzania.


Mbowe amesema, unahitajika muda wa kutosha ili mchakato huo uwe na manufaa kwa kuwa Serikali ina mawazo yake, vyama vya siasa vina mapendekezo yao, na wananchi wana mtazamo wao kuhusu muundo mzuri wa Katiba yao.


Kwa mujibu wa Mbowe, Chadema watashiriki katika hatua zote za mchakato wa mabadiliko ya Katiba, lakini pia itaendelea kuwaelemisha wananchi kuhusu haki zao za msingi.


Amesema, Chadema wanadai haki za msingi, Serikali isizuie uhuru wa mawazo, na pia viongozi wajifunze kukosolewa na wawaheshimu wananchi wa vyama vyote.


 
Kikwete aagiza CCM wajibu mapigo

Imeandikwa na Basil Msongo, Dodoma; Tarehe: 12th April 2011 @ 00:40 Imesomwa na watu: 267; Jumla ya maoni: 0








MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, amewaagiza wanachama wa chama hicho wajibu mapigo ya vyama vya upinzani, na hataki wamtumie ujumbe mfupi wa simu za mkononi (sms) kuwa wametukanwa.

Kikwete amewaambia wanaCCM kwamba, wapinzani hawana jipya, hivyo wakitukanwa nao wajibu, na amewaagiza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho wakatekeleze kile walichokubaliana.

"Hakuna kumtumia Rais sms kwamba jamaa wamenitukana, na wewe jibu" amesema Kikwete usiku huu mjini Dodoma wakati anafunga mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ulioanza Jumapili.

" Na tuliyokubaliana tunayajua, tumekubaliana, tukafanye vile tulivyokubaliana" amesema Kikwete na ameagiza kuwa yote waliyokubaliana wawe wameyatekeleza kabla ya mwaka 2014.

Kikwete amesema, aliona CCM inahitaji kufanya mageuzi kwa kuwa aliona kuna udhaifu, na kwamba, mkutano huo umefanya maamuzi makubwa na magumu.
"Lakini baridii kwa sababu tulijiandaa vizuri kufanya kile tulichodhamiria kukifanya" amesema Kikwete.

"Madhumuni yangu ni kwamba, tufanye mageuzi, tujenge upya chama chetu" amesema Kikwete na kuwaeleza wajumbe hao waliyokubaliana wanayajua, wakafanye walivyokubaliana.

Amewaagiza viongozi wa chama hicho waelekeze nguvu katika mashina na matawi kwa kuwa ndipo walipo wapiga kura wao.

"Tunaanza safari ya kujenga upya chama chetu, tuna safari ya kujenga CCM mpya, umoja wetu, mshikamano wetu ndiyo utakaotufikisha kwenye dhamira yetu" amesema Kikwete na amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kuwa inawezekana, kila mmoja atimize wajibu wake.

Amesema, CCM imeamua kubadili muundo hivyo watauomba Mkutano Mkuu wa chama hicho ufanye marekebisho ya Katiba ili wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wachaguliwe kutoka ngazi ya wilaya kwa kuwa wapo karibu na wananchi.

Amesema, CCM pia imeamua kuunda Baraza la Ushauri litakalojumuisha wazee wastaafu wa chama hicho ili wakitaka kushiriki katika vikao wa vya juu washiriki na wakiitwa pia waende au atumwe mwakilishi, badala ya kufanya kama sasa kwa kuwa wanaitwa kushauri katika ajenda zilizoandaliwa na chama.

Amesema, wazee katika baraza hilo wakitaka kushiriki katika mkutano wa Kamati Kuu watatoa taarifa tu na wataruhusiwa lakini pia watapaswa kuwa tayari kwenda chama kikiwahitaji.

Amesema, kuanzia sasa, chama kitapata wanachama wapya kwa mujibu wa Katiba ya CCM, ana amekiri kwamba, chama hicho kilitetereka sana wakati wa mchakato wa kura za maoni.

"Pale tuliteleza, limetuvuruga sana, unapata mkusanyiko ambao huna uhakika na uaminifu wao" amesema Kikwete na kubainisha kwamba, nguvu ya chama ni wanachama hivyo CCM inapaswa kuwa makini.

Amesema, katika mkutano huo, viongozi wa CCM wamepata fursa ya kutathimini ya uchaguzi mkuu uliopita, na wamekubaliana warekebishe makosa ili chama hicho kishinde kwa kishindo mwaka 2015.
 
Mtei: CCM inakwenda arijojo Send to a friend Friday, 22 April 2011 10:32

Fidelis Butahe
MWASISI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei amesema siku za CCM kukaa madarakani zinahesabika kwa kuwa chama hicho kimekosa usimamizi bora na hivyo kuiyumbisha nchi.

Akijibu maswali mbalimbali ya Mwananchi jana, Mtei alisema chama hicho kimeshindwa kutatua matatizo yanayowakabili Watanzania, suala ambalo litaifanya kupotea katika ramani ya utawala wa nchi.

“Siku za CCM kukaa madarakani zinahesabika, yaani natamani hata uchaguzi ufanyike kabla ya 2015,”alisema Mtei.

Mtei ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kukaririwa akisema kwamba, hatua inayofuata katika vita ya ufisadi ndani ya CCM, ni kwa viongozi wa Serikali wa ngazi zote ambao wamekuwa wakikisaliti chama hicho kwa kujifanya miungu watu.

Kwa mujibu wa Mtei, Chadema ndio chama kitakachochukua nchi baada ya CCM, kwani chama hicho tawala, kinakosa viongozi waadilifu na wanaojali matatizo ya Watanzania.

Mtei ambaye aliwahi kuwa gavana wa kwanza mzalendo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) nchini, alisema chama imara ni kile chenye sera za kutatua matatizo ya nchi na watu wake na sio "kujivua gamba".

Alisema kuwa Chadema ni chama imara kwa kuwa kina viongozi waadilifu ambao wako tayari kubuni mikakati mbalimbali kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Mtei alisema kitendo cha CCM kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi ikiwa ni pamoja na kuwapa siku 90 wanaweza kutimkia vyama vya siasa huku akisisitiza kuwa Chadema haitakuwa tayari kuwapokea.

“Chadema hakiwezi kukubali watuhumiwa wa ufisadi, yaani Watanzania wanataka wahukumiwe kwa ufisadi wao leo hii Chadema tuwapokee, hakuna kitu kama hicho, Watanzania wako wengi sana na wanaoingia Chadema wapo pia ila kwa watuhumiwa wa ufisadi hapana, haiwezekani,”alisisitiza.
 
Comments




-1 #7 thadeus mbani 2011-04-22 23:12 sijapata kuona watu wasanii kama CCM,hovyo kabisa kila kitu kipo wazi kuhusu mafisadi lakin.........??
Quote









0 #6 Kamuche 2011-04-22 21:48 Maoni ya siku hizi kama ngonjera, yamekosa uwazi na uchanganuzi wa mambo. Tuwe na upana na mawanda ya kujadili jambo. Ufinyu wa njia ya mawazo humpelekea mtoaji kutoona mbele kwa kudhani aendako ni karibu.
Quote









+1 #5 LENGAI 2011-04-22 19:13 SEREKALI INAYOMPA FISADI SIKU TISINI NA YENYEWE INAHUSIKA. SUBIRINI KAMA WATAFANYWA KITU. SIKU 90 WALIZOPEWA NI ZA KUFICHA MALI NA KUBADILI MAJINA YA MIRADI YAO.FISADI HAPEWI MDA WA KUJITETEA IKISHABAINIKA KAIBIA UMMA. KULE CHINA FISADI ANA DAKIKA TU ZA KUPUMUA AKISUBIRI KITANZI.
Quote









0 #4 FELIX 2011-04-22 18:39 CCM ilitakiwa kuwapeleka mafisadi mahakamani si kuwapa 90 days hiki(kujivua gamba) ni kiini macho maana waswahili wanasema kuzunguka mbuyu si kazi bali kuukumbatia.
Quote









+1 #3 Kishenga V. 2011-04-22 17:41 Mzee naomba usihangaike kufikiria MAFISADI waende wapi. Ni wazi kaisa, watatakiwa wafungwe jela baada ya kutaifishiwa mali zao walizotudhulumu . Tunawasubiri wajitaje ili tuwafungulie mashitaka. Hapo ndiyo tutajua serikali yetu ya sasa inasimamia wapi.
Quote









+2 #2 CAROLINE 2011-04-22 15:37 Fisadi out. CHADEMA finish them!
Quote









+1 #1 MWAYA 2011-04-22 13:20 No room for fisadi in TZ we are just counting the time to finish the game. Fisadi please come out and adress your dubious deals then regret and seek mercy! Thus all!
Quote







Refresh comments list

Add comment
 
Back
Top Bottom