GE2025 Maandamano ya Amani ya Watanzania Wanaoishi Marekani kufanyika Leo Oktoba 17, 2025

GE2025 Maandamano ya Amani ya Watanzania Wanaoishi Marekani kufanyika Leo Oktoba 17, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Its Tesha

Senior Member
Joined
Oct 6, 2025
Posts
168
Reaction score
604
Mapema leo nchini Marekani kunatarajiwa kuwa na maandamano ya amani ambayo yatafanywa na watanzania waishio Marekani wakihitaji mambo kadhaa ambayo pia yanaendana na mahitaji ya ya maandamano ya Oktoba 29, 2025.

Kesho tutafanya maandamano ya amani mjini Washington DC kwa ajili ya:
  • Demokrasia ya kweli nchini Tanzania
  • Kukomesha vitendo vya utekaji na kutoweka kwa watu, na kudai kujua hatima ya waliopotea akiwemo Soka, Mh. Polepole, Mdude na wengine wengi
  • Kuheshimu uhuru wa kujieleza
  • Kumuachia huru Tundu Lissu
  • Kudai mageuzi na uchaguzi huru na wa haki
===
Watanzania waliopo Marekani hivi karibuni walikusanyika nje ya Ubalozi wa Tanzania mjini Washington, D.C., kuonyesha hasira zao kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania. Maandamano hayo yalifanyika kwa amani na yalijumuisha wanaharakati, wanazuoni, na wanajamii kutoka sehemu mbalimbali za Marekani.

Waandamanaji walikuwa na mabango yenye picha za Rais Samia Suluhu Hassan na ujumbe unaotaka haki kwa waathirika wa mateso, kutoweka kwa watu, na ukandamizaji wa kisiasa. Waliitaka serikali ya Tanzania kuchukua hatua za dharura ili kumaliza vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu na kuhakikisha usalama wa raia wake.

Katika tukio la kipekee, baadhi ya waandamanaji walidai kwamba maafisa wa ubalozi walijihusisha na vitendo vya rushwa kwa kulipa watu wasio raia ili kuonyesha upinzani dhidi ya maandamano hayo. Hata hivyo, ubalozi haukutoa tamko rasmi kuhusu tuhuma hizo.

Maandamano haya ni sehemu ya msukumo mkubwa kutoka kwa Watanzania waishio nje ya nchi wanaotaka mabadiliko ya kisiasa na kisheria nyumbani. Wanasisitiza umuhimu wa demokrasia, utawala bora, na haki za binadamu kama misingi ya maendeleo ya taifa.

1760686656726.jpeg

1760686705347.jpeg
 
Wapande ndege waje waandamane Tz
 
Mapema leo nchini Marekani kunatarajiwa kuwa na maandamano ya amani ambayo yatafanywa na watanzania waishio Marekani wakihitaji mambo kadhaa ambayo pia yanaendana na mahitaji ya ya maandamano ya Oktoba 29, 2025.

Kesho tutafanya maandamano ya amani mjini Washington DC kwa ajili ya:
  • Demokrasia ya kweli nchini Tanzania
  • Kukomesha vitendo vya utekaji na kutoweka kwa watu, na kudai kujua hatima ya waliopotea akiwemo Soka, Mh. Polepole, Mdude na wengine wengi
  • Kuheshimu uhuru wa kujieleza
  • Kumuachia huru Tundu Lissu
  • Kudai mageuzi na uchaguzi huru na wa haki

Kuuza sura au kuandamana?😂

Cc: Mimi Wewe Yule
 
Back
Top Bottom