maandamano mengine hayo yanakuja

howard

Senior Member
Feb 21, 2011
188
28
Wakati huo huo, Chama cha Uzalishaji na Maendeleo Tanzania (TAMADA) kimesema kutokana na serikali kuwadharau wafanyabiashara wadogo wadogo wako tayari kufanya maandamano nchi nzima kuishinikiza serikali kuwajali wananchi wake.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Abel Mwakabenga, alisema kuwa ni jambo la ajabu kwa serikali kutowajali wafanyabiashara wadogo licha ya kuwasilisha kilio chao kila kukicha.
Akizungumzia jengo la Machinga Complex, alisema kuwa wafanyabiashara wamekuwa na maisha magumu kutokana na kuwaweka katika mabanda mfano wa vibanda vya mbwa wa polisi huku wakiwa hawana mitaji ya kutosha na kodi kubwa wanayotozwa ili kuweza kufanya biashara katika mabanda hayo.
source: tanzania daima
 
Duh mambo yamekuwa mambo ,walijenga hiyo mall ya machinga complex kama mtaji wa kisiasa si kukwamua wao watu sasa inakuwa dhahiri
 
Back
Top Bottom