Maandamano makubwa Songea!

skendo

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Posts
212
Reaction score
102
Wakuu nimepigiwa simu na rafiki'angu toka Songea anasema kumekuwa na mauwaji ya kutisha kwa mda wa wiki sasa na inasemekana watu zaidi ya kumi wamesha uwawa ingawa RPC amedai wananchi wasihofu.

Pia nasikia wananchi waliandamana mpaka kwa mkuu wa Wilaya ila bado uvumbuzi haujapatikana na inasemekana wananchi waliwachoma moto watu wawili kutokana na tuhuma za kuhusika na mauwaji hayo na ndipo wauwaji wakasema sasa wataendeleza mashamulizi.

Mwenye ndugu pande hizo anaweza mpigia simu ili tuweze pata taarifa zaidi ila kuna jamaa yangu mwingine ni polisi nae ameniakikishia kuwa hali si nzuri kwa sasa.

 
Wakuu nasikia kuna mtu mwingine ameuwawa leo hii na wananchi wako kwenye harakati za kuandamana.mwenye ndugu pande izo ajaribu ulizia tujuwe ukweli wakuu
 
dunia imefikia mwisho lakini mungu hawaondolee roho mbaya binadamu. hii taarifa ni ya kweli kabisa
 
Uletaji wa taarifa wa namna hii na unataka watu wajadili sidhani kama unakubalika kwenye jukwaa makini kama hili.Wewe ndio mleta taarifa sasa unataka nani mwingine atoe taarifa? Sisi hatujui wewe ndio unajua sana unauliza kwetu ili iweje?
 
Uletaji wa taarifa wa namna hii na unataka watu wajadili sidhani kama unakubalika kwenye jukwaa makini kama hili.Wewe ndio mleta taarifa sasa unataka nani mwingine atoe taarifa? Sisi hatujui wewe ndio unajua sana unauliza kwetu ili iweje?

Kaka mbona wewe unaonekana mzoefu hapa JF ..........wewe kama hunandugu Songea tulia..........acha wenye jamaa songea wapige kisha tutajua kinachoendelea.
 
Taarifa nilizopata mda huu nikwamba polisi wanawatawanya raia kwa mabomu ya machozi.

Pia watu wanashangaa kwanini vyombo vya habari vinafumbia macho hili jambo.

Ila habari za kule saiti zinadai ni watu toka msumbiji,wengine wanadai kuna vigogo wanahusishwa ni kwa mambo ya kishirikina ila ukweli kamili bado sijaufahamu nini hasa chanzo.
 
Maandamano makubwa songea kulaani polisi kwa kutochukua hatua kudhibiti mauaji ya raia yanayofanywa karibu kila siku katika mji wa songea.Mabomu ya machozi na risasi zinarindima kuwatawanya waandamanaji.
 
Tayari hadi sasa Raia mmoja ameshafariki kwa kupigwa risasi na polisi hali ni mbaya kupindukia.FFU wamejaa mji mzima wa songea wakitoa kichapo kwa Raia wema,wasio kuwa na hatia.
 
SACGOT inakuja huko ombeni mungu sana, mtanyan'ganywa mashamba yenu yote na kupigwa risasi za mchanganyiko wa moto na baridi, sisi wameogopa kuja huku kwenye vihamba vyetu
 
Kwa mujibu wa Wananchi wa mji wa Songea walishatoa taarifa kwa RPC, kuhusu mauaji yanayo fanyika songea kila siku, RPC akasema hakuna kitu kama hicho (kama kawaida dharau), sasa leo asubuhi kuna raia mwingine tena mmoja amefariki kwa kupigwa risasi, wananchi baada ya kuona hali hiyo wakaanza kuandamana kuelekea ofisi ya mkuu wa wilaya, Ndipo wale jamaa wasio kuwa na kazi ya kufanya (FFU) walipopigiwa simu na kuja kutoa kichapo kwa raia ambao wanakufa kama wanyama.
 
Niliona juzi kwenye taarifa ya habari kuhusu hayo mauaji na yule RPC akitema p.umba.
 
Hali inadhidi kuwa tete,wanafunzi wanalia,wengine wanakimbia,wametoka madarasani,mji mzima umejaa polisi,hali ni mbaya sana sana,hakuna maelewano kwa sasa,kijana alipigwa risasi kwa sasa amekimbizwa hospitali ya mkoa anatokea sehemu moja naitwa matarawe.
 
Jamani nimepata habari kuwa songea hali sio nzuri, kuna vita kubwa katika ya FFU na Bodaboda chanjo kuuwawa kwa dereva mmoja wa bodaboda. Aliekaribu atujuze jaman.

Nawakilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…