Maandamano IFM

Maandamano IFM

hapa wanafunzi wa ifm wakiandamana kupinga wenzao wawili kuvamiwa na majambazi halafu wakalawitiwa. Wamekwenda ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi kupeleka malalamiko yao kuwa waliwahi kuripoti kukosa usalama katika mabweni ao ila jeshi hilo halijachukua hatua zozote.

wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha ifm wakiwa ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi nchini jijini dar es salaam leo mchana.

kiongozi wa wananfuzi ifm akimweleza kamanda wa polisi kanda maalum dar es salaam suleiman kova juu ya kadhia iliyowapata wenzao kwa kuvamiwa na majambazi wakiwa wamelala.

baada ya kuzungumza nao kamanda kova aliamua kuandamana nao mpaka zilipo hostel na kituo cha polisi walichodai waliripoti matatizo yao lakini hawakusikilizwa. Kova aliwaahidi watapanda kivuko bila malipo, tatizo wanafunzi walijaa kuliko uwezo wa kivuko. Hapa akijadiliana na askari wenzie namna ya kuwapunguza wanafunzi hao....


wanafunzi hao walivamia makao makuu ya jeshi hilo majira ya saa nne na nusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya hosteli za kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku waliyofanya kikao na jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na kubakwa hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. Majambazi hao wamekua wakidai kupewa laptop simu na fedha kama mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.


hii ndo tanzania, nchi inayoongozwa na mbululas, every time they are reactive, we need the pro active leaders, achana na ukenge wa policcm
 
Kazi ipo!sasa hapo mimi sijaelewa,ulinzi gani unatakiwa kwenye hostel hizo?au wanafunzi wanatakaje?kuwepo askari pale kwenye hostel zao au iweje?hakuna walinzi binafsi kwa ajili ya hostels zao?hao majambazi wanafahamika?kwa maana wanajulikana na polisi hawajawakamata?au ni wale wa kustukiza na kuvamia?

wanafunz wanaibiwa na kulawitiwa wewe ujui ulinz gani wanaitaji? makubwa
 
Hii nayo kali yaani polisi aje kulinda Hosteli?​
 
Ina maana uongozi wa hostel haupo na hamna ulinzi binafsi ktk hiyo jumuiya, hata mm swali langu hilohilo hapo polisi waweke sungusungu au wawe walinzi wa hostel???
 
Ina maana uongozi wa hostel haupo na hamna ulinzi binafsi ktk hiyo jumuiya, hata mm swali langu hilohilo hapo polisi waweke sungusungu au wawe walinzi wa hostel???

polisi wanawajua wahsika a majina walipelekewa sema hawajafanyia kazi n inavoonekana wanagawana hela. kwenye mapato ya mauzo ya laptop na simu hizo
 
Du hii kali kama walianza mda mrefu ina maana wanafunzi wanaokaa kigamboni wengi wao wameliwa
 
Ina maana uongozi wa hostel haupo na hamna ulinzi binafsi ktk hiyo jumuiya, hata mm swali langu hilohilo hapo polisi waweke sungusungu au wawe walinzi wa hostel???

Katiba inasema ni kazi ya Polisi kulinda raia na mali zao.
Kama wanafunzi wameona uongozi wa hostel pamoja na walinzi hewa wameshindwa, ni jukumu lao kuomba ulinzi kwa polisi.

Polisi wanapopewa taarifa za wahalifu, na watu/kikundi cha watu kuomba ulinzi, ni jukumu la polisi kutoa ulinzi.

Kama polisi hawatoi ulinzi, ni sahihi kwa vijana hao kuandamanana kudai maelezo as to why hawalindwi.

Msiwe mnaongea tu bila kuwa informed.
 
Ishu ya kulawitiwa denti wa IFM inanikumbusha msemo simba kula mtu ni habari ila mtu kula simba ni habari hatari ..sidhani kama hata hizo nchi zenue ushenzi kama afghanistan au akistani wamefikia huko
 
Duh basiii kila atakayelawitiwa akiandama au kuomba ulinzi wa polisi itakuwaje?
 
Mimi naona hawa wanafunzi wenyewe kwa wenyewe wamepigana dushelele wanasingizia majambazi
 


wanafunz wanaibiwa na kulawitiwa wewe ujui ulinz gani wanaitaji?
makubwa

Polisi wanawafahamu hao majambazi, labda hawana interest nao. Kwa mfano
ridhiwani ndo angekuwa amelawitiwa hao majambazi wangepatikana within 2
hours tu....
 
Kazi ipo!sasa hapo mimi sijaelewa,ulinzi gani unatakiwa kwenye hostel hizo?au wanafunzi wanatakaje?kuwepo askari pale kwenye hostel zao au iweje?hakuna walinzi binafsi kwa ajili ya hostels zao?hao majambazi wanafahamika?kwa maana wanajulikana na polisi hawajawakamata?au ni wale wa kustukiza na kuvamia?

nasikia wakitoa taarifa hakuna kinachoendelea zaidi ya stori za kila siku tutafuatilia ndio tatizo hapo washaiba sana laptop sasa hivi wanataka na ndogo pia..
 
Walindwe na Polisi Hostel kwani wao ni zaidi ya Raia wengine ambao tunakosa ulinzi huo huku mtaani? Kwa nini wasipambane na mmiliki wa hiyo hosteli aweke ulinzi binafsi? Polisi wenyewe wako wangapi kulinda kundi kubwa lote la Wanafunzi ambao ni wanaume wenye nguvu?.
 
Mimi naona hawa wanafunzi wenyewe kwa wenyewe wamepigana dushelele wanasingizia majambazi

Wee sio mzima kabisa yakikukuta au ukaambiwa babako kafanywa hivyo ndo utshika adabu.
Sii kila thread uchangie wehu wako. People r serious unaleta ----- hapa.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
NI vyema uongozi wa chuo , kuingia mkataba na kampuni kubwa za ulinzi zenye uwezo wa kupambana na khali kama hiyo. tatizo hapa yawezekana kampuni ya ulinzi iliyopewa jukumu la kusimamia usalama wa mali za wanafunzi na usalama wao haina uwezo. jukumu la polisi ni kutambua eneo hilo ni hatari hivyo kuweka utaratibu wa doria za mara kwa mara. vilevile hapa ile elimu ya ulinzi shirikishi inapotakiwa kutumika.
 
Mi nadhani polisi nao wanakosa busara! Kwa nini wawapige virungu? Aaaargh
 
Hawa wanafunzi waongo, dume la mbegu kamwe haliwezi kulawitiwa..! Tena unalawitiwa bwenini? Haiwezekani, hao watakuwa wanalewa mpaka wanazima halafu wengine wanawanyatia..! Sasa huu ulinzi mpaka vyubani utawezekana vipi?
 
Back
Top Bottom