Absolute
JF-Expert Member
- Jan 19, 2007
- 333
- 62
Walowezi wanaoishi katika ardhi zilizoghusubiwa za Palestina wamefanya maandamano wakipinga ubaguzi wa rangi na wa kizazi ndani ya utawala wa Kizayuni wa Israel. Ripoti zinasema kuwa maandamano hayo yaliwahusisha zaidi Waethiopia waliohamishiwa katika ardhi za Palestina wakipinga ubaguzi wa rangi na wa kimbari wanaokabiliana nao huko Israel.
Zaidi ya Waethiopia elfu tano walioshiriki katika maandamano hayo mbele ya bunge la Israel wametoa wito wa kufutwa sheria za kibaguzi na kupewa haki sawa za kijamii. Waandamanaji hao walikuwa wakipiga nara za kulaani ubaguzi wa rangi wanaofanyiwa na utawala ghasibu wa Israel kutokana na rangi ya ngozi yao. Waandamanaji wa Kiethiopia pia walikusanyika mbele ya nyumba ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu na kutoa maneno yanayolaani siasa za kibaguzi za Israel.
SOURCE: Maandamano dhidi ya ubaguzi huko Israel