Maandalizi ya mazishi ya Dkt. Philemon Ndesamburo

Maandalizi ya mazishi ya Dkt. Philemon Ndesamburo

Ilikuwa mwaka 2004 kuelekea uchaguzi wa mwaka 2005, nikiwa kijana mdogo na mwororo (sekondari) hayati Ndesamburo alitua na chopa yake wilayani kwetu.

Sikuwa naijua CHADEMA zaidi ya CCM na wapinzani wao UDP kwa wakati huo hapo jimboni kwetu.

Nilijongea kumsikiliza; Alikuwa mzee wa makamo aliyebeba makabrasha aliyoyatumia kutueleza UFISADI wa serikali ya CCM. Ujengaji hoja wake, charisma na namna alivyoongea kwa passion kubwa vilinifanya kuipenda CHADEMA tangu siku hiyo. Nikawa chachu ya mabadiliko ya kifikra kwa vijana wenzangu shuleni..!

Yote haya alisababisha hayati Ndesamburo. Ile siku bado iko kichwani mwangu hata leo hii.

Pumzika kwa Amani Comrade Ndesamburo.

Mungu ibariki Tanzania,

Mungu ibariki CHADEMA.
Aisee mkuu na mm nakumbuka huo mwaka nilikuwa moshi mjini pale wakichuana na Mama Minde wa CCM...aisee ule uchanguzi ulisaidia sana shule mana tulitewa sattelite dish tukachana na kaantena kale ka "V" na kuna siku ulipikwa msosi wa hatari pale skuli tukala kuku kwa mara ya kwanza aisee .Halafu siku chache kabla ya uchaguzi headmaster akawa anatuambia kuhusu ule msosi kwamba ni kwa hisani ya ....japokuwa hakusema moja kwa moja na alikuwa anazungukazunguka sana..Ila mwisho wa siku CCM waligaragazwa vibaya pale kituo cha shuleni.
 
Back
Top Bottom