Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,125
- 8,644
Pamoja na kuishi kwangu kwa kungaunga (sina elimu kubwa) nilijinyima shilingi 25,000/= nikanunua simu kutoka kwa mchimbaji mdogo yenye uwezo wa kutumia Facebook. Nikaunganishwa na rafiki yangu aliyekuwa anatoa huduma ya internet (internet cafe) huku kijijini kwetu mwaka 2011.
Mara nikakuta friend request kibao lkn mmoja kati ya hao ni mama mmoja wa Kisouth mwenye umri unaokaribiana na mama yangu mzazi. Tumechati kwa muda mrefu lkn kilichomfanya kuvutiwa sana na mimi ni pale nilipokuwa nachati nae hadi saa saba usiku nikiwa kwenye lindo la kulinda maduka usiku. Ukweli nilikuwa namsumbua sana kwa broken English niliyokuwa natumia kwani ilifikia hatua nikawa naogopa hata kuchati kwa kusingizia na kumwandikia "sorry am busy chat later dear" hicho tu ndicho nilikuwa naandika cha maana na nilikopi toka kwake. Baadae mwaka 2012 nilipata mkopo NMB hapo ndipo biashara yangu ikatanuka na nikawa nachati nae nikiwa safarini Mwanza (niko maeneo ya Geita). Baadae siku moja akaniuliza kama simu yangu ina uwezo wa whatsapp na kama sina basi nidownload hiyo app.
Pasipo kujua kuwa hii simu haina uwezo huo siku hiyo usiku nilikesha nadownload pasipo mafanikio ndipo kesho yake nikamwambia haina uwezo na akaniuliza kama huduma ya western union inapatikana nikasema hapa Mwanza ipo ndipo akanitumia pesa in doller yenye thamani ya laki 3 za Kitanzania. Nikachukua pesa na kwenda madukani pale kwenye duka kubwa la Vodacom unapotokea Kamanga ferry. Nikachukua Nokia Asha kwa 150,000/= pesa nyingine nikafanya mengine.
Aisee nilikuwa sijui umuhimu/kwa nini alitaka whattsapp kwani pamoja na kutumiana sms kwa njia rahisi pia tulitumiana picha mbalimbali na kubwa kabisa yeye alitaka kunicontrol ili afahamu usiku nalala na nani,niko wapi na nafanya nini. Mimi nina mke na nina watoto wawili na pia nafanya biashara. Hivyo kuepuka huo mtego nilikuwa napiga picha nyingi nikiwa nimelala Kitandani ama kitanda chenyewe wife akiwa hayupo akihitaji tu nipigie unitumie picha natuma nilizoandaa tayari baadae akaniamini na kuacha.
Baadae mwanzoni mwa mwaka jana nikaanza kufuata bidhaa Kampala kwa basi la Friends na kipindi basi la J4 halijasitisha safari. Hapo ndipo akaona kuwa namfaa na akakomaa niende kwake kusimamia biashara zake za magari. Kusafirisha abiria na gari za mizigo kuja Zambia na Mozambique. Hadi ninapoandika haya tayari nimeshamwita dada yangu ambaye atasimamia duka akiwa na wife na mdogo wangu ambaye amehitimu masomo ya ukunga Bombo Tanga ambaye kwa kweli namkubali sana (tunapendana sana).
Na tayari yule mama tumeweka mikakati kibao pindi nikifika huko. Nilimpatia no ya kijana mmoja toka huku kwetu aliyezamia huko na nashukuru alimtafuta na kumwita kwake na kumtambulisha kuwa mimi na ...........ni marafiki na nimeamua kumleta huku South Africa. Siku hiyo jamaa yangu alininishangaa sana kwa nini bado niko Tanzania kwani alinihakikishia kuwa mama huyo vizuri kimaisha ila umri nisijari sana.
Kuhusu Botswana.
Nilikutana na dada wa Kibotswana fb kipindi hicho akiwa mjamzito ila akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha BOTHO university. Alinipa story yote pasipo kunificha kuwa baada ya kupata ujauzito jamaa akasepa na kupitia pesa ya baba yake ambaye ni mfanyakazi wa mgodini huko na pesa ya chuo kikuu ya kujikimu hasumbuki lolote kwani wanalipwa kama waajiriwa. Ilikuwa ni 2013,hapo nikiwa vizuri kidogo kwa English kutokana na tuition kali ya Msouth kupitia sms.
Huyu dada katika hali iliyoniacha mdomo wazi kama wiki moja na siku kazaa kabla ya xmass aliomba anitumie pesa ili nikienda Kampala nikamnunulie nguo kwani nilikuwa namtumia picha za bidhaa za huko hadi anachanganyikiwa (ashajifungia muda mrefu tu na anamalizia masomo mwaka huu na tayari wezetu kule wanasoma huku wakijua anaenda kufanya kazi wapi na shirika gani). Aliponiomba niende karibu na ofisi za western union nilimwambia acha tu kutuma pesa nikiamini kuwa Uganda zawadi za 50,000/= ama 80,000/= ni nyingi na quality sana hususani nguo.
(Kumbuka mawazo ya kuzamia yalikuwepo tangu nikiwa form one Geita Secondary School). Nilipoenda kufuata mzigo wa Xmass huko ndiko nikaamua kutupa sadaka kwa Mbotswana kwa kumnunulia nguo jeans,vibonde vya kijanja na chupi kama nusu dazani ambapo hata 80,000/ haikuzidi.
Nilipofika nyumbani pamoja na zawadi kwa wife wangu na watoto nilizificha hadi nilipopata safari ya Mwanza na nikafika DHL karibia na bank ya posta Mwanza na kuzituma (gharama za dhl ni balaa). Wakati natuma niliumia sana moyoni kwa kutumia pesa vibaya pia niliangalia je hizi pesa kama nimewaongezea nyumbani kwa kilimo si mungu ataniongezea baraka tele!
Lakini nilikaa kimya pasipo kumwambia hata mdogo wangu kwani nilijua hiki ninachofanya ni tabia mbaya na haipaswi kuigwa hata kidogo. Ndugu zangu nilipotuma ule mzigo pale dhl nilipiga picha receipt nikamtumia!!! Hakuamini na akaniambia ashawahi kuambiwa kuhusu Watanzania na Tanzania kuwa ni watu wema sana.
Sasa huyu dada hatua tuliyofikia ni kuwa niende Botswana na kwa kuwa nina vyeti vya uzoefu wa mining kutoka kampuni ya Barrick katika mgodi wa Bulyanhulu atamtumia baba yake kunipatia kazi mgodini yeye akiwa anamalizia masomo mwaka huu huku nikiishi nae kwenye nyumba ya mama yake ambaye ashafariki (anasoma lakini anafahamu ataenda kufanya kazi ofisi za SADC hapo Botswana nchini kwao). Wiki jana alinitumia pesa ya chakula njiani kama 473,000/= kwa pesa za Tanzania. Kwani February hii inayokuja lazima nisafiri.
Nimemwambia tasafiri kwa basi hadi South Africa baada ya kumsalimia kaka yangu (yule mama) taunganisha hadi Gaborone na amekubali kwa moyo mmoja.
NB: kuna watu watafikiri namkimbia mke wangu,hilo halipo na ninachoenda kucheki huko ni fursa na wale mtakao nipa ushauri mzuri zaidi na uzoefu wa huko kama mshafika tawatafuta pindi nikiwa huko.