Maana ya ushindi wa NASSARI JOSHUA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maana ya ushindi wa NASSARI JOSHUA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FortJeasus, Apr 4, 2012.

 1. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Tarehe 18 March 2012,wiki moja baada ya kuanza rasmi kampeni za uchaguzi wa Arumeru Mashariki,na baada kuangalia mwenendo wa kampeni hizo,nilisukumwa na dhamira yangu kuanzisha ,hapa JF, thread yenye kichwa kisemacho:'Kwa nini naamini CHADEMA itashinda Arumeru' .Ninayo furaha kubwa kuwa, jana , bwana Nassari (CHADEMA) ametangazwa kuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki.Kufuatia ushindi wa jana ,nimesukumwa kuleta kwenu maeneo makuu saba, ambayo naamini daima yatabaki kama taathira ya ushindi huo:
  1 Haki ya mtu haipotei.
  Nassari aliamini kuwa alishinda uchaguzi wa ubunge mwaka 2010 kwa kupata kura 27,000, na kumshinda marehemu Jeremiah Sumari.Anasema kuanzia saa 12 jioni ya siku ya uchaguzi, matokeo yalionyesha kuwa alikuwa ni Mbunge halali wa Arumeru Mashariki,lakini ,katika hali ya kushangaza,ilipofika saa sita usiku ,wenye mamlaka ,kwa sababu wanazozijua wao,wakamnyang'anya ushindi wake kwa kubadili matokeo.Kama alivyosema mwenyewe, wakati anazindua kampeni,na jana wakati akiwashukuru wananchi pale Leganga ,hakwenda mahakamani kupinga matokeo, bali aliamua kukaa kimya na kumwachia Mungu ,akiamini kuwa itafika wakati atapata haki yake iliyoporwa.Watawala wafahamu kuwa wanalazimika kutenda kwa haki ,vinginevyo haki hizi zinaweza kudaiwa kwa nguvu inapobidi.
  2.Kampeni zenye hoja huamua mshindi.
  Wakati wote wa kampeni ,Nassari,pamoja na wanakampeni wake, walizungumza matatizo ya Wana Arumeru kwa kina,huku ajenda kuu ikiwa ni ardhi na maji na kuonyesha kwa nini yeye na chama chake ndiye mtu sahihi katika kuleta utatuzi wa matatizo hayo.Kwa kuwa kwa muda sasa, CHADEMA imekuwa ikisimamia dhana ya resource nationalisism,(usimamizi na utumiaji wa rasilimali mbalimbali kwa manufaa ya wananchi) ,haikuwa vigumu hoja za ardhi na maji kukubaliwa na wapiga kura.CCM,wakitambua udhaifu wao katika kusimamia rasilimali za taifa,kwa mfano uamuzi wake wa kubinafsisha mashirika ya umma na uuzaji wa nyumba za umma,walitumia mbinu dhaifu ya kushambulia waleta hoja badala ya kuzikabili hoja zilizoletwa.Hali hii ilileta athari kubwa kwa upande wa CCM baada ya kulazimika kutunga uongo mara kwa mara,ambao wao wanauita propaganda,ambao hata hivyo ulikanushwa kwa hoja na wahusika mara moja.Maana ya ushindi wa Nassari ni kuwa uongo , wa jina lolote lile, hawauwezi kamwe kushinda dhidi ya ukweli.
  3.Wapiga kura ndio waamuzi wa matokeo ya uchaguzi.
  Matokeo ya Arumeru yanatukumbusha somo muhimu, katika demokrasia, kuwa vyama vya siasa vinapoingia katika uchaguzi,vyote huwa na nafasi sawa ya kushinda ama kushindwa na kinachoamua mshindi si ukongwe wa chama ,si idadi ya wabunge chama kilichonacho, wala sera za chama gani zinatekelezwa.Arumeru Mashariki wamefanya uchaguzi ambao matokeo yake yamekiondoa chama tawala na ishara kuwa panapokuwa na utashi wa kisiasa-political will- miongoni mwa wenye mamlaka ,bila kujali vikwazo vya kitaasisi na kisheria -institutional & legal constraints- upo uwezekano wa mshindi kupatikana kupitia sanduku la kura na sio kwa hila wala wizi wa kura .Pamoja na kuwa nilipata taarifa kutoka kwa Afisa mmoja wa CHADEMA pale kambini Leganga, USA RIVER ,usiku wa saa 6, kuwa kwa kuzingatia mwelekeo wa zoezi la kuhesabu kura ,hesabu na makisio yalikuwa yanaelekeza kuwa Nassari atashinda kwa tofauti ya kura kati ya 6000 hadi 9000 (na ndicho kilichotokea), bado nilimwona msimamizi wa uchaguzi kama mtu pekee aliyeshikilia turufu ya mshindi wa uchaguzi ule, maana uzoefu umeonyesha kuwa wasimamizi wa chaguzi zetu,katika maeneo mbalimbali, wanao uwezo wa kubadilisha matokeo kwa maslahi ya watawala.Tunamshukuru Mungu Msimamizi wa Uchaguzi alitangaza ushindi kwa mtu aliyestahili.
  5.Mungu yupo upande wa wanyonge,watumwa , walioonewa na waliokandamizwa.
  Kwa miaka kadhaa,Wana Arumeu wamejikuta wakiwa watumwa katika ardhi yao,wakikosa raslimali ardhi ambayo ni muhimu kwa kuendesha maisha yao.Kama Joshua wa kwenye Biblia ,aliyechaguliwa na Mungu kuwaongoza wana wa Israeli kwenda Kanani, baada ya Musa kushindwa kufanya hivyo,ndivyo Mungu alivyomchagua Joshua Nassari kuwaondoa Wameru kutoka katika minyonyoo ya umaskini ,ufungwa na unyonge wao.Hii ni kazi ambayo wabunge waliopita wa CCM hawakuweza kuifanya.Kadhalika,ni mgombea pekee katika uchaguzi wa Arumeru aliyetambua ukuu wa nguvu za Mungu kwa kuomba maombi kutoka kwa watu mbalimbali ili Mungu amlinde dhidi ya hila na hujuma zilizoelekezwa kwake na washindani wake hasa kutoka CCM, ikiwemo uwezekano wa kuibiwa kura.Ni dhahiri kuwa Joshua, kwa kuzaliwa katika familia inayomcha Mungu, wazazi wake wakiwa wachungaji katika kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT), naye akiwa ni muumini wa kanisa hilo, imechangia kwa kiasi kikubwa kuamua fikra,mtazamo, kauli na matendo yake wakati wa kampeni na hivyo kuweza kuvutia kura kutoka kwa wapiga kura.Paragrafu hii inatuleta katika point nyingine muhimu hapa chini:
  6.Nafasi ya Imani katika maisha yetu.
  Wakati akizungumza na umamti uliojitokeza jana kumlaki na kumsikiliza,alieleza kuwa baada ya kupata vision ya kuwa Mbunge na kuamua kuwashirikisha baadhi ya watu maono hayo,wengi wao walicheka na kudhani huenda amechanganyikiwa,lakini yeye,kwa kujua alichokuwa anakitafuta, hakukubali kuvunjika moyo.Kama vile Barack Obama alivyoeleza katika kitabu chake cha Audacity of Hope,Mungu anapotaka kutenda jambo fulani huzungumza na mtu mmoja mahususi aliyekusudiwa na halazimiki kuzungumza na watu wengine ili kuthibitisha uhalisia ama ukweli wa mpango wake.Kwa mfano,Mungu alizungumza na Ibrahimu ili amtoe Isaka sadaka naye alitii.Ni dhahiri kuwa, iwapo Ibrahimu angewashirikisha watu waliokuwa wanamzunguka kusudio lake hilo ,wapo ambao wangemwona kama mtu aliyechanganyikiwa na yawezekana kabisa wangepiga ripoti kwa vyombo vya dola kutaka Ibrahimu akamatwe kwa 'kosa la jinai' alilokuwa amekusudia kulitenda.Kile ambacho Nassari aliamini anastahili ndicho alichopata.Aidha,kwa kuzingatia ukweli kuwa mara kwa mara,tena kwa makusudi, watu walioonekana kama wastahili heshima kwa kuzingatia majina,ukongwe wao, na vyeo vyao, wametamka maneno yasiyostahili dhidi Nassari ,CHADEMA na vingozi wake, Nassari amekuwa akitamka wazi,tangu wakati wa kampeni na jana wakati akiwashukuru wananchi,kuwa amewasemehe wale wote ambao walijipanga kuharibu taswira yake kwa jamii.
  7.Siasa za Tanzania hazitabaki kama zilivyokuwa.
  Baada ya kutangazwa matokeo,siasa za CHADEMA ,siasa za CCM na siasa za kibunge na zile za kitaifa hazitabaki kama zilivyokuwa kabla ya uchaguzi huo.CHADEMA wanamaliza uchaguzi wakiwa na mafanikio makubwa na hoja zake wakati wa kampeni zimesikika masikioni mwa Watanzania wengi nchini,wamepata wameongeza mzungumzaji mwingine mahiri bungeni.Hali kadhalika hoja na matusi yaliyotoka upande wa CCM yamesikika ,na bila shaka wananchi wamepata fursa ya kuwaelewa watawala wao.CCM ,ili kulinda heshima kidogo iliyobakiwa nayo,sasa haina budi kujichunguza kwa ndani, iwapo bado inataka kuendelea kuwa chama cha kisiasa achilia mbali kuendelea kushika dola.
  7.Nguvu ya vijana kidemografia.
  Vijana ,ambao Takwimu za Tume ya Taifa Uchaguzi zinaonyesha wanaunda asilimia 60 ya wapiga kura, wanaweza kubadili hatma ya siasa za nchi yetu,kwa kushiriki moja kwa moja kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ama kama wapiga kura na raia wanaowajibika (responsible citizens).Hakuna shaka yoyote kuwa, ushindi wa Nassari utachochea ari na hamu ya vijana katika kuamua mwelekeo na siasa za kitaifa na zile za maeneo.Ni ukweli ulio dhahiri kuwa,mafaniko ya chama chochote cha siasa, yatategemea uungwaji wake na vijana na hii inavilazimu kubuni namna ya kukidhi matarajio ya kundi hili, kwa kuwashirikisha katika kusanifu, kupanga,kusimamia, kutekeleza na kutathimini sera,programu mikakati na miradi mbalimbali ya maendeleo.
  Kwa unyenyekevu mkubwa naomba kuwasilisha.
   
 2. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mkuu hapo umenena.
   
 3. m

  mimdau Member

  #3
  Apr 4, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 3
  :shock:


  mkuu u r very right hapo juu
   
 4. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Yuko sawa kwa yote; lakini tujiandae kuwaelimisha vijana wa vijijini, kwao kupewa elfu 20,000/= wakauza shahada ni deal. Sasa ni kwa vipi tumejipanga kuwabadilisha vijana hao ili waweze kuvumilia japo kwa kipindi kifupi ili wafaidi matunda ya uvumilivu wao na kuyang'oa haya mafisadi yasiyokuwa na huruma na raia wa nchi hii?
  Chadema 1.jpg WANACHADEMA TOENI ELIMU KWA VIJANA WALIOKO KIJIJINI.
  ANDAA MKAKATI VIJANA TULIOKO MIJINI TUKO TAYARI KUANZISHA UELIMISHAJI IWAPO MTATUPANGIA MIKAKATI INAYOELEWEKA.
  Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika - Mungu tubariki wanachachema - Mungu wamulike wana - CCM na unafiki wao wa kusema "wape nyama wanyamaze"
   
 5. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Thanx wakuu.kila mmoja wetu pale alipo, atumie fursa mbalimbali kutoa elimu ya uraia sio tu kwa vijana, bali hata kwa makundi mengine.
  Ili kutimiza lengo hilo, kwa kuanzia ,ninakusudia kugawa handouts either kwa soft copy ama hardcopy zinazohusu advocacy na natarajia kuzigawa kwa yeyote atakayehitaji hapa JF.
   
 6. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Turudi Arumeru kutekeleza ahadi huu si wakati wa kampeni miaka miwili na nusu ni michache sana kwa Nassari. Huu ni wakati wa kumshauri kwa kila ahadi aliyotoa.
   
Loading...