Maana ya pete katika uhusiano

Maana ya pete katika uhusiano

Rebo Tz

Senior Member
Joined
Sep 26, 2016
Posts
169
Reaction score
125
Wakuu mimi naomba kuuliza hivi mtu ukivishwa pete haijalishi ya uchumba au ndoa na mpenzi wako ni anamaanisha anakupenda sana?
 
Pete ni ujinga tu,kuna mijitu ilitaka kukonga nyoyo na mahawara zao wanavua pete eti za ndoa,kisa zimebarikiwa na kiongozi wa dini,pumbaaaavu kabisa,yaani baada ya kumuogopa mungu yanaogopa pete.
Pete ni ujinga mtupu,eti pete ya ndoa,sijui ya uchumba.
Mwenye hoja aje.
 
Asante mkuu kwa mawazo yako
 
Pete za sikuhizi ni mapambo tu,kama zilivyo hereni,bangili na cheni.
 
Pete ni ujinga tu,kuna mijitu ilitaka kukonga nyoyo na mahawara zao wanavua pete eti za ndoa,kisa zimebarikiwa na kiongozi wa dini,pumbaaaavu kabisa,yaani baada ya kumuogopa mungu yanaogopa pete.
Pete ni ujinga mtupu,eti pete ya ndoa,sijui ya uchumba.
Mwenye hoja aje.
Umechangia kwa Ukali...

Ungejenga hoja yako tu kawaida ungeeleweka
 
Pete ni ujinga tu,kuna mijitu ilitaka kukonga nyoyo na mahawara zao wanavua pete eti za ndoa,kisa zimebarikiwa na kiongozi wa dini,pumbaaaavu kabisa,yaani baada ya kumuogopa mungu yanaogopa pete.
Pete ni ujinga mtupu,eti pete ya ndoa,sijui ya uchumba.
Mwenye hoja aje.
Khaaa hasira zoote izo za nn mkuu
 
Wakuu mimi naomba kuuliza hivi mtu ukivishwa pete haijalishi ya uchumba au ndoa na mpenzi wako ni anamaanisha anakupenda sana?

Maisha hayana fomula Mkuu,Kuvishana pete yeyote ni imani ambayo Binafsi sitokaa niielewe kulingana na tukio lenyewe lilivyo.Swali langu ni hivi,Kama sina vidole ina maana nisioe kwakuwa sitovalisha/sitovalishwa pete??

Ndiyo maana vilema na vipofu wanadumu kwa muda mrefu katika mahusiano yao pamoja na kuishi muda mrefu kuliko sisi wenye vidole na pete karibu vidole vyote.

Wakati mwingine nawaza kuwa ni kujiweka katika vifungo fulani hivi ambavyo mwisho wa siku ni taabu na matatizo.

Kuvalishana pete hakuna maana kuwa ni kupenda/kupendwa sana,Ni utamaduni tu tuliourithi kwa waliotutangulia ambao wengi wetu hatuuelewi.

Hakujatofautiana sana na Kuzika watu kwa kutumia majeneza.Tuna ardhi kubwa pamoja na Mbao za kutosha hivyo ni sawa tu,Tusingekuwa na ardhi pamoja na Mbao tusingezika watu ardhini wala kutumia majeneza.Ni utamadunu fulani tu,Hauna maana rasmi.
 
Ni alama kwamba tayari ana mtu na sio single, lakini sio kwamba inamaanisha upendo
 
Kwa nini unavaa gauni na sketi na usivae suruale za kiume au mwanaume kwa nini unavaa suruale na mashati tofauti na wanawake? Lengo kubwa la vitu tuvaavyo ni kujitofautisha na makundi mengine. Halikadhalika Pete hukutofautisha na makundi mengine. Kwa hiyo mavazi yanakutofautisha tu kwamba wewe ni mwanamke ila kama tabia ni za kiume hazitabadilika. Pete itakutambulisha kwamba umeoa au kuolewa ila tabia yako itabaki pale pale.
 
Hata cheti cha ndoa ni ujinga tu mtu kama anakupenda anakupenda tu akikuchoka hata huo mkataba mliosanishana haun maana unless lengo liwe ki secure mali msije dhulumiana.
 
Mleta mada swali, kwa nini unavaa nguo? Unavaa nguo kwa kuwa umepewa akili na utashi wa kujitofautisha na wanyama. Lakini wanyama pia wanaweza kukalishwa nguo lakini hazitakuwa na maana kwao. Lakini kuvaa nguo Kwako hakukuondolei tabia ya kuwa kama mnyama kama unayo. Hivyo wenye ndoa walipata utashi wa kuvaa Pete kujitofautisha na maseja lakini hata maseja wanaweza kuvaa Pete lakini with meaningless.
 
Hata cheti cha ndoa ni ujinga tu mtu kama anakupenda anakupenda tu akikuchoka hata huo mkataba mliosanishana haun maana unless lengo liwe ki secure mali msije dhulumiana.
Upendo unajengwa na commitment na accountability. Hivyo commitment na accountability huongozwa na sheria.
 
Kwa uelewa wangu pete huvaliwa moyoni..
Ni ile nadhiri kwamba nakupenda kwa moyo wangu wote na hali zangu zote.
Kuvaa pete ya ndoa/uchumba kama hauijui thamani yake moyoni ni sawa na urembo tu.
 
Maisha hayana fomula Mkuu,Kuvishana pete yeyote ni imani ambayo Binafsi sitokaa niielewe kulingana na tukio lenyewe lilivyo.Swali langu ni hivi,Kama sina vidole ina maana nisioe kwakuwa sitovalisha/sitovalishwa pete??

Ndiyo maana vilema na vipofu wanadumu kwa muda mrefu katika mahusiano yao pamoja na kuishi muda mrefu kuliko sisi wenye vidole na pete karibu vidole vyote.

Wakati mwingine nawaza kuwa ni kujiweka katika vifungo fulani hivi ambavyo mwisho wa siku ni taabu na matatizo.

Kuvalishana pete hakuna maana kuwa ni kupenda/kupendwa sana,Ni utamaduni tu tuliourithi kwa waliotutangulia ambao wengi wetu hatuuelewi.

Hakujatofautiana sana na Kuzika watu kwa kutumia majeneza.Tuna ardhi kubwa pamoja na Mbao za kutosha hivyo ni sawa tu,Tusingekuwa na ardhi pamoja na Mbao tusingezika watu ardhini wala kutumia majeneza.Ni utamadunu fulani tu,Hauna maana rasmi.
Maana inafikia wakati wengine mpaka zinawachimba vidole hata kutoa hawataki...
 
Natafuta wa Kumvisha na ntampa na BMW 5 Series kama Mike Mkama
1475078222439.jpg
 
Pete ni biashara kubwa sana kwa masonara pia kwa wenye migodi ndio walikuja na hii mbinu ya kuvisha pete wakati wa ndoa. Pia upande mwengine inasaidia kutumika kama alama ya ndoa. Mfano ukimuona mwanaume au mwanamke amevaa pete unajua huyu Mume au Mke wa mtu.
 
Pete huwa na maana kwa wahusika lakini kwa watu wengine wanaweza wakaona kama vile ni nothing. Akikuvisha pete ya uchumba kwa dhamira ya ndani ya kukuoa basi pete hiyo itakuwa na maana kwako na kwake pia
 
Back
Top Bottom