1. Mjinga ni mtu asiefahamu jambo fulani. Kwamba hana knowledge kuhusu jambo fulani. Mjinga akielimishwa anabadilika na kuwa mwerevu.
Literally kama hujui kuhusu mambo ya uchumi, wewe ni mjinga kwenye uchumi. Kwa lugha ya malkia wanasema 'ignorant' / 'illiterate'.
2. Mpumbavu ni mtu ambaye akili yake hata aleweshwe vipi hawezi kuelewa. Tofauti yake na mjinga ni kuwa, mjinga akieleweshwa anaelimika ila mpumbavu habadiliki chochote.
Mpumbavu literally ni mtu asiweza kuelewa simple logic, hana cognitive ability n.k.. Yani huyu kikiingia sikio moja kinatokea la pili. Kwa lugha ya malkia wanamwita 'fool'