Maana ya elimu ni ufanisi kazini

Maana ya elimu ni ufanisi kazini

RWEZAURAJOHN

Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
24
Reaction score
27
Huu ni mchango wangu kwenye kuiboresha elimu. Mfumo wa elimu ulenge ufanisi kazini badala ya kumpa mwanafunzi taarifa za mambo mengi. Kwa maana hiyo, kuanzia elimu ya msingi ya kati, wanafunzi wasomee taaluma badala ya kulundikiwa masomo mengi, yenye mlengo tofauti.

Hasa anapomaliza darasa la nne, uwezo wa mtoto unakuwa umejulikana. Baada ya hapo, apunguziwe masomo na kupewa masomo ya uwezo wake yaliyo katika mfumo wa taaluma. Masomo matatu au manne, yanatosha kumnoa mtoto kuelekea taaluma. Akienda na hayo tu, atafaulu na atakuwa na uelewa wa taaluma yake. Kuanzia kidato cha 5 na 6 uwe ni utafiti na vitendo.

By JOHN R. RWEZAURA (Entrepreneurs adviser)
 
Ushauri wako ni Mzuri sana Ndugu John.

1.Selikali si kana kwamba haijui kinacho endelea kwenye mfumo mzima wa Elimu.
ELIMU UOZO.

2.Vigogo na VIONGOZI WAKUBWA hawaruhusu watoto wao kusoma Tanzania, kata wilaya nk.

3.Lengo la kuwa na Elimu Mbovu ni kuwafanya watoto wao wanapotoka kwenye shule nzuri KUENDELEA KUTAWALA.

Mwalimu nyerere anamaliza beti kwa kusema
"Ole wake Tanzania tusipo isaidia nifanyalo nimeliweza kishauri na kuonya zaidi nifanye nini"

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.
 
Back
Top Bottom