Maana, aina na faida za "Connection"

Maana, aina na faida za "Connection"

Simon Jilala

New Member
Joined
Jun 25, 2020
Posts
2
Reaction score
0
"CONNECTION"

Nimekosa Kiswahili fasaha labda Watalaamu mtaniambia Kiswahili cha "Connection". " "Connection" hapa namaanisha kupata urahisi kutoka kwa mtu, watu au mazingira ili kuweza kukusaidia wewe na mwisho wa siku ufanikishe kusudi ulilonalo maishani mwako/jambo unalolifanya maishani mwako.

Katika Maisha, narudia tena katika maisha kuna kitu kinaitwa "Connection". Hizi "connection" zina nguvu sana kuliko unavyodhani katika maisha yako. Kuna "connection" ambazo unazo karibu kabisa na kuna "connection" ambazo unatembea nazo kila siku na kuna "connection" ambazo unatakiwa uzitafute mwenyewe kwa kutumia mbinu zako unazozijua. Na kuna "connection" ambazo unazo katika mazingira yako kitu muhimu ni kujiongeza tu.

Msisitizo wangu kabla hatujasonga mbele kusoma andiko langu hili ni kwamba: Tumia maarifa yako yote, mbinu zako zote na ujuzi wako wote ili uwe "connected" lasivyo utawaona wale unaodhani unawazidi maarifa na ujuzi katika sehemu hiyo hiyo moja wakiwa wanazidi kufanikiwa/kufanikisha ndoto zao. Ukiona "connection" moja haikusaidii tafadhari sana usipoteze muda na miaka mingi kulaumu kuliko kutafuta "connection" zingine.

Kulalamika kamwe hakutaweza kukusaidia, tafuta "connection" kadri unavyoweza. Na wewe kama unanafasi ya kuwapa "connection" wenzako jitahidi sana kuwaunganisha ili wawe "connected" na mfumo ambao wanadhani watafanikisha kusudi walilonalo maishani mwao. Kwani, hujui kesho itakuwaje katika maisha yako. Leo unaweza kujiona umefika na yule ukamuona wa hovyo kumbe akaja kuwa msaada mkubwa maishani mwako au kwa watoto wako au ndugu zako.

Je, unadhani naongelea connection zipi?. Kwa uelewa wangu kuna "connection" ambazo nadhani ni muhimu sana kuzijua na ujue kuzitumia ipasavyo.

1. Wazazi au Walezi wako.

Kuna msemo unasema kwamba "Charity Begin At Home". Tafsiri isiyo rasimi: Huruma Huanzia Nyumbani. Wewe ni mzazi/mlezi watafutie "connection" watoto wako kadri unavyoweza. Unaweza ukawa katika sehemu nzuri sana kikazi na ukawa huna msaada kwa watoto wako kwa sababu wewe unahisi kwamba ulipata kazi bila msaada wa wazazi wako na wao wapambane. Ndugu yangu, sisemi uwaweke ulipo HAPANA. Jaribu kuwapa connection imara zaidi. Ulishawahi kujiuliza kwa nini ni rahisi sana Mtoto wa Mwanajeshi kuwa Mwanajeshi akitaka sababu kubwa ni "connection". Na pia mtoto wa Mwanasheria, Mwalimu, Daktari, Rubani, n.k ni rahisi mzazi wake kumpa "connection" Usipompa connection mtoto wako ni nani sasa utampa connection?.

Fikiri kwa kina na utafakari sana. Na mtoto naye kama amesoma anatakiwa amkumbushe mzazi wake umuhimu wa connection kwani kwa kumsaidia atakuja kumsaidia Mzazi/Mlezi wake. Hiki kitu kimewafanya watu wengi kuwa masikini. Ndugu yangu unayesoma kuanzia leo amini kwamba connection ina nguvu kuliko unavyodhani. Siongelei ubinafsi, ukabila naongelea nguvu ya connection, mwenye kuelewa ameelewa.

2. Ndugu Zako Wanaokuzunguka

Hawa nao ni muhimu sana katika kukupatia connection. Ndugu zako wanaweza kuwa Kaka, Dada, Mjomba, Mama Mdogo/Mkubwa, Shangazi, Watoto wa Mjomba, Shangazi, Mama zako n.k. Ukikuta Ndugu wako pamoja kupeana connection ni rahisi sana sana. Ukikuta ndugu wanapendana kupeana connection ni rahisi sana. Lakini, nawaaambia kwamba kuna Ndugu wengi sana kama siyo wote, wao wakifanikiwa hawataki kabisa hata ndugu zao wawasaidie au kuwapa connection mwisho wa siku umri unawatupa na wanajikuta hawama msaada kutoka pande zote kwani wakati wanashikilia connection waliona watabaki juu juu mawinguni kama anavyopenda kusema Mzee wa "Liquid" kwa wanaomfahamu.

3. Marafiki zako.

Jitahidi sana kuwa na marafiki ambao wanaweza kukupa connection za maisha kuliko marafiki wa kufanya nao sitarehe tu. Jitahidi sana kuwatumia marafiki zako katika kupata connection. Nitawapa mfano, wewe kwa mfano una rafiki yako ana mafanikio sana katika eneo hilohilo ambalo na wewe unalifanya lakini sijui sababu ni nini mkikutana yeye hataki kuongelea jambo hilo zaidi ya kukusisitiza mfanye starehe, hapa anza kujiongeza taratibu.

Unakuta una rafiki ana mafanikio sana lakini mkikutana anakuchukulia kama mfanyakazi wako hapo huna rafiki anza kujiongeza.

Nitawapa mfano mmoja wa mtu na rafiki yake kipenzi sana toka wakiwa wadogo. Mchezaji Mashuhuri wa Mpira Christian Ronaldo aliwahi kunukuliwa kwamba kuchukuliwa katika Academy ya Club ya Lisbon alipewa connection na rafiki yake. Kivipi?. Walikuja Maskauti wa Lisbon wakiwa wanatafuta wachezaji Vijana, wakaona Ronaldo na Rafiki yake wana uwezo mkubwa sana kisoka, walitaka wamachukue mmoja tu; sasa walitoa sharti kwamba katika mechi waliyokuwa wanawaangalia yule atakayefunga magori mengi watamchukua: Matokeo ya mechi ile walishinda 3-0 na walifunga goli 1-1 kila mtu na dakika za mwisho rafiki yake Ronaldo akiwa nafasi kubwa ya kufunga hakufanya hivyo na alimpatia pasi Ronaldo na kufunga goli la 3. Mpira ulipoisha Ronaldo alimfuata rafiki yake na kumwambia kwamba; kwa nini ulifanya hivyo?!. Alijibu: Wewe unasitahili kusonga mbele kwani una uwezo kuliko Mimi. Walikuwa marafiki kwelikweli na leo hii rafiki wa Ronaldo anaishi maisha mazuri kwa msaada wa rafiki yake Ronaldo kama shukrani. Huo ndo urafiki wa kweli na hizo ndizo "connection".

4. Mazingira Unayoishi.

Mazingira unayoishi yanaweza yakakunyima kabisa connection na ukashindwa kufanikisha kusudi la maisha yako. Kwa mfano, una ndoto ya kuwa Mwanamichezo kama mazingira uliyopo siyo rafiki tafuta mazingira rafiki. Kama wewe una ndoto ya kuwa mkulima wa zao fulani na unaishi katika jangwa hama na nenda katafute mazingira rafiki na ukaanze kilimo. Kama wewe unataka kuwa mfanyabiashara wa kimataifa anza kutafuta mazingira "connection" taratibu kuelekea huko unakotaka ufike lasivyo hutasogea au kufika mbali.

Kuna watu unawazidi maarifa na uwezo katika kila nyanja na wamefanikiwa kuliko wewe katika eneo hilohilo kwa sababu ya wewe kung'ang'ania kuishi mazingira ambayo siyo rafiki kwako na kitu ukifanyacho. Ondoka hapo ulipo na katafute mazingira rafiki ili uweze kufanya jambo lako hilo. Usipoondoka mazingira hayo utabaki kulalamika tu. Mazingira yanaweza kuwa mabaya kwa sababu ya siasa za nchi husika. Kwa mfano, kwa sasa Iraq, Libya, Siria na nchi zote zilizochafuka kwa sababu ya vita siyo rafiki kibiashara na kazi zingine. Bila shaka mmenielewa.

Mwisho

Kwa kuwa na connection nzuri na ukaitumia vizuri na kwa ueledi mkubwa;

a) itakupatia kazi nzuri
b) itakusaidia kufanikisha ndoto zako
c) itakusaidia kufanikisha kusudi la maisha
d) itakusaidia kusonga mbele kiurahisi zaidi
e) itakusaidia ukipata changamoto maishani

Pia; kwa kukosa connection

a) pamoja na maarifa na ujuzi wako unaweza usipate kitu unachokitaka kwa urahisi au uwezekano wa kukikosa kabisa ni rahisi
b) kuna ugumu wa kufanikisha ndoto zako.
c) kuna ugumu wa kufanikisha kusudi la maisha yako
d) kila jambo likitokea kwako utaliona katika mfumo wa tatizo na siyo fursa kwa sababu huna connection
e) utazidi kulalamika kila siku kwa sababu huna "connection"

Tafuta "Connection"

Kama utapenda kuongeza maarifa zaidi. Soma kitabu cha MISINGI MUHIMU KATIKA MAISHA.

#SomaKitabu
#MisingiMuhimuKatikaMaisha

Kinapatikana kwa Tsh 5000// na kiko katika mfumo wa e-book na ukilipia utatumiwa kwa njia ya email au WhatsApp 0754684684.

Simon Ngusa Jilala
 
Ni mitazamo yako pia, ila unaweza jikuta ni tegemezi wa kilofa sana kutegemea connections, kwanza unapoteza dira ya kujitegemea pia unapoteza ubunifu nini ufanye mpaka usubirie connection, mfano mzuri ni mimi mzee wangu alikuaga mtu fulani serikalini lakini alipokufa sijaona support yoyote toka kwa marafiki zake, hapa nilipofika nimelijenga life langu mwenyewe,
 
Ni mitazamo yako pia, ila unaweza jikuta ni tegemezi wa kilofa sana kutegemea connections, kwanza unapoteza dira ya kujitegemea pia unapoteza ubunifu nini ufanye mpaka usubirie connection, mfano mzuri ni mimi mzee wangu alikuaga mtu fulani serikalini lakini alipokufa sijaona support yoyote toka kwa marafiki zake, hapa nilipofika nimelijenga life langu mwenyewe,
Hahahahaaa ya kwamba umelijenga life lako mwenyewe bila Wazazi/Ndugu/Marafiki/Watu wanaokuzunguka (SelfMadeBillionnaire). Mnajidanganya sana and this is the starting point of selfish...Mimi mwenyewe niko hapa lakini natambua michango ya walionizunguka, ama moja kwa moja au indirect ways.
 
Back
Top Bottom