barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Wakati Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) ikisema mafuta yaliyoagizwa bila ya kushindanisha zabuni ndiyo yanayosabababisha bei ya soko la ndani isishuke kadri inavyotakiwa, Waziri George Simbachawene amesema alichukua uamuzi huo kutokana na wasiwasi wa usalama wa nchi baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.
Gazeti la Mwananchi linasema licha ya bei kushuka ktk soko la dunia lkn Tanzania mafuta yameendelea kuwa bei juu,hii ni kwasababu Waziri Simbacahwene wakati akiwa Waziri wa Nishati alitoa tenda ya kununua mafuta hayo bila kufuata sheria ya manunuzi ya umma na kanuni za EWURA za uagizaji wa mafuta.
Aliagiza kununuliwa kwa mafuta hayo ambayo ni shilingi bilioni 40 zaidi kwa sababu tu hakushindanisha zabuni zilizokuwa tayari mezani,mafuta hayo yalikuwa ni kwa mwezi Septemba,October na November na anadaiwa kufanya hivyo bila kufuata usahuri wa EWURA. Hatua hiyo ndio imesababisha kutokushuka kwa bei ya mafuta licha ya bei ya pipa kuporomoka kwa kiasi kikubwa katika soko la dunia.
Hadi jana bei la pipa katika soko la dunia ilikuwa dola 30.77 za kimarekani(sawa ni Tsh 61,500) wakati bei ya petrol vituoni DSM ilikuwa ni Shilingi 1,842 na dizeli shilingi 1,600.
EWURA wao wanasema kwa namna ilivyokuwa,mafuta hayakutakiwa kuja bila ya tenda,kwa kuleta mafuta bila tenda iliongezeka bilioni 40 zaidi,kitu ambacho kisingekuwepo kama kungekuwa na kushindanishwa kwa tenda,EWURA wanasema mafuta yalinunuliwa kwa bei ya juu kutokana na ghlama za usafirishaji,bima na faida ya mtu anayenunua,ilipanda zaidi ya dola milioni 20 ambazo ni kama shilingi bilioni 40. Wao kama EWURA walitoa ushauri,kama haukutekelezwa au la,suala linakuwa mikononi kwa waziri.
SImabachawene alipotafutwa,yeye akajitetea kuwa alifanya hivyo sbb kwanza sheria inamruhusu,lkn pia wakati huo wa uchaguzi kulikuwa na tishio la machafuko ndani ya nchi mara baada ya uchaguzi,na mabalozi wengi walionya kuwepo kwa maandamano na machafuko mara baada ya uchaguzi,na yeye kama Waziri akajiuliza kama kukitokea fujo na nchi haina mafuta,basi kunaweza kuhatarisha usalama wa nchi.
Simbachawene pia anasema alikuwa hana uhakika na huyo atakayeshinda kama anaweza kuleta mafuta,anaweza akawa ameshinda na kufanya njama za kutokuleta mafuta ndani ya nchi,kwa hali hiyo wakaamua kumpa kazi hiyo mtu aliyekuwa na uzoefu wa kuleta mafuta bila kufuata tender