Maamuzi ya AU & Tumaini la Haki kwa Upinzani Afrika:U Scratch my Back, I scratch Ur's | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maamuzi ya AU & Tumaini la Haki kwa Upinzani Afrika:U Scratch my Back, I scratch Ur's

Discussion in 'International Forum' started by Elifasi, Feb 1, 2011.

 1. E

  Elifasi Senior Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AP: Umoja wa Afrika umetoa nafasi ya mwezi mmoja kutafuta mstakabali kuhusu urais wa Ivory Cost - kati ya mng'ang'ania madaraka - Gbagbo - na ALIYESHINDA KIHALALI - Alassane Ouattara..... Ukweli ni kwamba ukweli uko wazi (mshindwa nani na mshindi nani), na kama ni haki haipaswi kuombwa bali kuchukua kama tulivofanya ANJOUAN (COMORO)- hasa kwa kutumia chombo kilichopewa baraka za bara zima kama AU- Sasa:
  • Je, kuna sababu za kuendelea kukiamini chombo hiki katika kudumisha demokrasia ya africa kwa maana ya serikali ya watu iliyowekwa na watu kwa maslahi ya watu???!!!
  • Ni sawa kui-branch organization hii kama chombo cha kubebana kwa wakamia madaraka wa bara hili- you scratch mine, I scratch your's - so tukubali kushinwa (tuwe pessimistic) au tutafute otenative?
  • Tunaanzia wapi - short & long term?
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Unategemea nini kama wajumbe wa hiyo timu ya usuluhishi kuna JK na Mugabe????????
   
 3. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wanajitahidi kuuficha ukweli kwenye nafsi zao. Mwisho wa siku tutasikia eti wamewapatanisha (kana kwamba waligombana) na hivyo Mng'ang'aniaji anakuwa prezidenti na aliyeshinda kihalali anapewa u-praimu minista kama ambavyo tumeshuhudia maeneo kadhaa ya africa wezi wa demokrasia wakifanya hivyo. hii ni hatari.
   
 4. E

  Elifasi Senior Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo tunalijua, na ndo mantiki ya swali. Na swali lenyewe ni kwa wana maoinduzi... ni zipi strategy mbadala za ku-deal na hili wimbi la udikteta kwa mgongo wa demokrasia ambao nchi za kusini mwa jangwa la sahara tunaupalilia, tukikaa vitako na kupiga siasa za midomoni huku tukikaa na kudanganywa na serikali za mseto, wakati wananchi wenzetu wenye nyama na damu kama sisi wanafanya mapinduzi ya kweli hapo juu africa tu??!!
   
Loading...