whizkid
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 357
- 240
Pua ndefu kama Pinocchio ni ishara ya uongo uliopindukia. Tumeshuhudia mambo mengi ya kisanii yakiendelea hasa katika ulingo wa siasa za Chama Cha Mapua-ndizi. Yameongelewa mengi na viongozi wa chama hicho kishika dola, mikutano ikafanyika mpaka ikafikia hatua ya chama kujivua magamba yake ya kijani. Green mamba wa kibisa?
Leo hii, ni dhahiri kwamba magamba yaliyoongelewa si yaliyovuliwa. Maamuzi "magumu" yaliyotolewa kwenye vikao yameshindikana kufanyiwa kazi. Najiuliza. Nahoji. Serikali inayoshikiliwa na chama kinachoendeshwa na viongozi waliojifananisha na nyoka na kuajiri panya wa majaribio (Nape na vijana wake), inaposhindwa kuyafanyia kazi maamuzi yoyote "magumu" ya kutatua matatizo ya chama chake, itaweza vipi kufanya maamuzi magumu kulinusuru Taifa letu? Huu sio utapeli wa kisiasa? Wanachama na wakereketwa hili hawalioni kama linakereketa?
Tunaongelea kila siku jinsi Rais wa nchi asivyoijali nchi na watu wake, Rais ambaye amewekwa na nyoka wanaokimbizana na panya kwenye mifereji ya siasa zisizokuwa na tija kwa Taifa bali kwa wakamata nyoka (Mafisadi). Rais ambaye hajui kwanini wananchi wake ni maskini, na anashangaa tu kisha anapanda ndege na kwenda kusalimia au kutafuta familia na/au marafiki zake nje ya nchi! Kiongozi kama huyu ambaye inaonekana wazi kuwa hasomi hata mikataba na majalada yanayomfunga (na kututesa wananchi), ana uwezo gani wa kutoa maamuzi "magumu"?
Unapotumia akili zako za kawaida (common sense), ukiwa kama Mtanzania na unatambua jinsi maisha yako ya kila siku yanavyoathiriwa na kuporwa na utapeli wa watu wachache, upo tayari kuendelea kutumika kama panya wa majaribio katika banda la nyoka? Kwanini tunaendekeza ushabiki badala ya kudai haki zetu za msingi?
Wakati unajiandaa kuchangia hoja, tafakari tena picha hiyo hapo juu. Hebu waangalie na hawa jamaa hapa chini: