Maalim Seif: Zanzibar, Bara zipokezane urais

Maalim Seif: Zanzibar, Bara zipokezane urais

Huyu jamaa ni mroho wa madaraka maana kila anapofungua mdomo wake ni kugombea uongozi tu. Sasa kweli ikiwa tutapokezana nafasi ya Urais kuna haja gani ya kuwa na vyama vingi? Yaani kila baada ya miaka 10 vyama vilazimike kuchagua mgombea kutoka bara au visiwani akili kweli hiyo!. Kesho wataanza huko kwao mbona hatujapata rais - Mpemba!
Pumbavu kabisa,

Nafasi zote za juu kwenye serekali ya muungano wanatoka tanganyika sasa hapo nani mroho wa madaraka?au hamjui kuwa muungano ni wa nchi 2?nahisi wewe ndio pumbavu namba moja kuliko wote.
 
Duh!Kumbe vurugu yote ya kuitaka Zanzibar yetu ni URAIS wa Bongo? Yaani Tanganyika, ukishangaa majabu ya Musa utayaona ya firauni.
 
Wadau kwa kweli kwa sasa muungano wetu unapumulia mashine, ni jambo la busara sasa vyama vyote vya siasa kumsimamisha mgombea urais toka znz kwenye nafasi hiyo ili znz nayo itoe rais na muungano wetu uendeleee.

au wanasiasa wenzangu mnalionaje hili? maana mwalimu alipotoka akampa mznz, mznz akampa mbara mkapa. nashangaa kwa nini mkapa asingeshinikiza salmin awe rais maana haya malalamiko yasingekuwako.

Rais wa Zanzibar atoke bara na Rais wa Muungano atoke Zanzibar.
 
Tatizo sio idadi ya watu tumesema muungano ni wa nchi 2 huru lazima kuwe na usawa. Burundi na Ruwanda wana wajumbe sawa kwenye umoja wa EAC ambapo Tanzania ina idadi ya mil45.
Kila siku mnalinganisha EAC na JMT. EAC sio sovereign state. Hakuna uraia wa EA wala EA sio dola. Muungano ni wa nchi mbili zenye tofauti kubwa sana ya eneo na watu. Mtanganyika yeyote muulize; atakua yuko tayari kuvunjika muungano kuliko kupokezana uongozi wa taifa. Labda kama ni rais ceremonial.
 
Kama serekali 3 hazitakubalika wazanzibar wadai haki ya kugombea urais wa jamhuri wa muungano kwa kupitia CCM.Chama ambacho kitakuwa kinaishia kugombea na si zaidi ya hapo.
 
Maalim Seif Sharif
Hamad amesema kwa mfumo wa
muungano uliopo, ni vyema kila
upande ukawa unatoa rais kila baada
ya miaka 10.

Ina maana Maalim ameaafiki S2?

Mbona mumeanza kubweka? kumbe mnaona vyema sana Tanganyika ikiitawala Zanzibar miaka nenda miaka rudi kupitia mwavuli wa muungano haramau lakini mumekuwa wakali sana kauli ya maalim seif kupishana madaraka ya muungano. vumilieni tu mara hii Rais wa Muungano atoke Zanzibar. kama nyinyi hampendi madaraka mbona hii hoja aliyojenga maalim mumekuja juu sana intarahamwe..!
 
Huyu jamaa ni mroho wa madaraka maana kila anapofungua mdomo wake ni kugombea uongozi tu. Sasa kweli ikiwa tutapokezana nafasi ya Urais kuna haja gani ya kuwa na vyama vingi? Yaani kila baada ya miaka 10 vyama vilazimike kuchagua mgombea kutoka bara au visiwani akili kweli hiyo!. Kesho wataanza huko kwao mbona hatujapata rais - Mpemba!
Pumbavu kabisa,

Mbona mumeanza kubweka? kumbe mnaona vyema sana Tanganyika ikiitawala Zanzibar miaka nenda miaka rudi kupitia mwavuli wa muungano haramau lakini mumekuwa wakali sana kauli ya maalim seif kupishana madaraka ya muungano. vumilieni tu mara hii Rais wa Muungano atoke Zanzibar. kama nyinyi hampendi madaraka mbona hii hoja iliyojenga maalim mumekuja juu sana intarahamwe..!
 
Mbona mumeanza kubweka? kumbe mnaona vyema sana Tanganyika ikiitawala Zanzibar miaka nenda miaka rudi kupitia mwavuli wa muungano haramau lakini mumekuwa wakali sana kauli ya maalim seif kupishana madaraka ya muungano. vumilieni tu mara hii Rais wa Muungano atoke Zanzibar. kama nyinyi hampendi madaraka mbona hii hoja aliyojenga maalim mumekuja juu sana intarahamwe..!

Hujanielewa, issue hapa ni s3 au mamlaka kamili. Seem like Maalim amelegeza msimamo in favour of s2+rotating presidency.
 

maalim_seif.jpg

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na waandishi wa gazeti la Mwananchi walioongozwa na Mhariri Mtendaji, Frank Sanga (wa tatu kulia) walipomfanyia mahojiano maalumu kwenye Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
Picha na Edwin Mjwahuzi



Jumatano, Agosti 27 2014


Kwa ufupi
Mjumbe wa Bunge la Katiba, Profesa Abdul Sheriff alisema utaratibu huo utaleta maana iwapo kuna muundo wa serikali tatu na si wa serikali mbili.


Dar/Dodoma
Kauli ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kuhusu haja ya kupokezana nafasi ya urais kati ya Bara na Visiwani imekuwa ‘ngumu kumeza' kwa wanasiasa walio wengi.


Baadhi ya wanasiasa wakiwamo wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na wasomi wengine waliozungumza na waandishi wetu wamepinga kauli hiyo wakieleza kuwa suala hilo halitawezekana kwa sababu linaweza kusababisha mgawanyiko mkubwa katika jamii.

Mwanasiasa pekee aliyeonyesha kuiunga mkono kauli hiyo ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyesema jambo hilo linazungumzika kwa sababu huwezi kuwa na nchi mbili zilizoungana lakini nchi moja pekee ndiyo inayotoa rais mara zote.

"Miaka ya nyuma utaratibu huu ulikuwapo lakini baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka, CCM wakauondoa. Kitendo cha rais kutoka Tanzania Bara kila baada ya miaka 10, ndicho chanzo cha Zanzibar kubadili Katiba yao na kuifanya nchi hiyo kuwa na mamlaka kamili yasiyoweza kuingiliwa na rais wa Muungano," alisema Mbowe.

Hata hivyo, Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, alisema mfumo wa kubadilishana urais, utaleta mgawanyiko kwa makundi na maeneo mengine ya nchi kudai kuwa na zamu ya urais.

"Hatuwezi kwenda katika mfumo huo. Utasababisha kugawanyika kwa sababu ukishasema hivyo watatokea Waunguja nao watadai, Wakaskazini, Waislamu na Wakristo nao watadai," alisema.

Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, alisema utaratibu huo unaweza kuleta matatizo kwa vyama katika kumpata mgombea mwenye sifa.

Alitolea mfano katika uchaguzi uliopita ambao Dk Slaa alipata mgombea mwenza ambaye hatoshi upande wa Zanzibar.

Mjumbe wa Bunge la Katiba, Profesa Abdul Sheriff alisema utaratibu huo utaleta maana iwapo kuna muundo wa serikali tatu na si wa serikali mbili.

"Kwa sasa rais anachaguliwa na upande wenye watu wengi ambao ni Bara kwani wazi atashughulika na mambo ya Serikali ya Tanzania Bara na si ya Muungano," alisema.

Mwanasiasa mkongwe, Paul Kimiti alisema suala hilo ni zuri na analiunga mkono iwapo nchi inakwenda katika muundo wa serikali moja. "Kama tunataka kutekeleza chini ya mundo wa serikali mbili ni lazima tubadilishe mambo mengi kwanza," alisema.

Kimiti alisema zamani iliwezekana kwa sababu nchi ilikuwa katika mfumo wa chama kimoja cha siasa.

Mbunge wa Dole (CCM), Sylvester Mabumba alisema rais anatakiwa atokane na uwezo, sifa, uadilifu, hekima na jinsi alivyo na upendo kwa wapigakura wake, badala ya eneo anakotoka.

"Kama ni zamu ya upande Tanzania Bara na tumekosa mtu ambaye ana sifa na uwezo tunafanyaje na tumeshajiwekea utaratibu huo?" alihoji Mabumba. "Maalim Seif ni mwanasiasa mzoefu na aliyebobea na pia ni msomi katika eneo la siasa angefanya uchambuzi, vinginevyo atasababisha mgongano katika jamii," alisema.

Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM –Bara, Pius Msekwa alisema, "Sioni tatizo lolote kwa sababu uongozi huwa haubadilishwi kama mtu anavyobadilisha shati. Unajua mkiamua kupeana zamu ni dalili za kutoaminiana."

Huku akimtolea mfano Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, Msekwa alisema rais huyo alitokea Zanzibar na alipatikana kwa sababu kwa wakati huo alionekana anafaa na si kwa sababu alikuwa akitokea upande huo wa Muungano.

"Jiulizeni kama mnapotaka kubadilisha ili kila upande utoe rais kila baada ya miaka 10 mnataka kurekebisha jambo gani? Mbona kwa sasa hakuna tatizo lolote, binafsi naunga mkono utaratibu wa sasa."

"Ndani ya CCM majina ya wagombea urais hupendekezwa na hatimaye kubaki jina moja na huo utaratibu hutumika katika vyama vingine, sasa ukifanyika uchaguzi anayeamua nani awe rais ni Watanzania wenyewe bila kujali huyu wa huku na huyu wa kule," alisema.

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Agustine Mrema alisema: "Tukipitisha kisheria ya suala hili tutajiletea matatizo makubwa. Anatakiwa kutizamwa mtu mwenye vigezo kwa wakati huo kama ilivyokuwa kwa Mwinyi. Jambo hili lisiwe lazima, bali yatazamwe mahitaji ya wakati husika."

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Charles Rwechungura alisema: "Hakuna sheria inayosema nchi mbili zikiungana lazima rais atoke kila upande wa muungano kila baada ya miaka fulani. Binafsi sioni kama jambo hili ni tatizo kwa sababu nchi hizi zinaweza kukubaliana tu tena kwa mazungumzo ya kawaida kabisa."

Rwechungura alisema ingawa Zanzibar wanaweza kuhoji kuwa udogo wa nchi yao ndiyo sababu ya kutokutoa rais wa muungano, lakini hata kama wakipewa fursa hiyo haiwezi kuwa dawa ya kuondoa kero za muungano zilizopo.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Bashiru Ally alisema tatizo lililopo ni muundo wa muungano na si mzozo wa nani atoe rais na nani asitoe.

"Lazima mkubaliane muundo wa muungano na mgawanyo wa mamlaka ya serikali baina ya pande mbili za muungano. Rasimu ya Katiba ya sasa haisemi lolote juu ya jambo hili na lingeweza kujadiliwa ila kama unavyoona mchakato wa Katiba nao umeingia dosari," alisema.

CHANZO: Mwananchi
 
Maalim Seif naye pamoja na wadhifa wake binafsi huwa simuelewi. mara akaja na serikali ya MKATABA. kisha akazuka na serikali TATU, leo hii anakuja na KUPOKEZANA
 
Maalim na Karume waliwafunga paka kengele kina Sheikh Farid wa Uamsho ili kutimiza ndoto yao ya kutawala milele baada ya kuvunja Muungano, wakachagua kutumia watu wa Dini waanzishe, na ndio maana TRA ya Zanzibar ZRB ndio alikuwa mfadhili
 
Back
Top Bottom