Nguvu ya Hoja
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 276
- 125
Leo saa 10:00 alasiri katibu Mkuu wa CUF katika ziara yake jijini Dar es Salaaam, atamtembelea baba askofu Gwajima ofisini kwake katika kanisa la Ufufuo na Uzima Ubungo ili kumfariji na kumjulia hali pamoja na kuongea mambo mbalimbali yanayoendelea nchini.
Habari hizi zimetolewa na Naibu Mkurugenzi wa habari na uenezi wa CUF Bw. Mbarara Maharagande alipokuwa akitoa taarifa ya ziara ya katibu mkuu huyo inayoendelea jiini Dar.
======
UPDATES
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima amemuweka kiporo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na kuhoji kwa nini mwenyekiti huyo anaruhusiwa kukivuruga chama hicho.
Askofu Gwajima ameyahoji hayo baada ya kupokea malalamiko ya mgogoro uliopo ndani ya CUF kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad alipokwenda kumtembelea ofisini kwake, leo Ubungo jijini Dar es Salaam.
“Katika mazungumzo yetu nilitaka kujua Lipumba anafanyaje kuvuruga chama chako ili nami nijue cha kufanya, si unajua tena. Kwa nini unamruhusu kukivuruga chama?” amehoji Gwajima.
Baada ya kuhoji hayo, Gwajima amesema atayatafakari mazungumzo hayo na kwamba baada ya kutafakari atajua cha kufanya sambamba na kuueleza umma kile atakacho kuwa nacho.
“Kwa vile ameniambia mgogoro jinsi ulivyo basi nami najua cha kufanya, na nitakacho kuwa nacho nitasema baadae, ngoja nitafakari kwanza,” amesema.
'Mimi huyu ni rafiki yangu kwa hiyo nilitaka kujua Professa Lipumba anafanya nini kuvuruga CUF, hivyo nilitaka kujua Lipumba amepatwa na nini mpaka amevuruga chama chako na kiukweli mimi nilikuwa siufahamu vizuri huu mgogoro ila saizi Seif ameniambia kwa hiyo na mimi nataka nitafakari alichoniambia rafiki yangu ni 'digest' baada ya hapo nitajua nafanya nini" alisema Gwajima
Nilikuwa siufahamu vizuri mgogoro wa CUF ila sasa Seif ameniambia. Natafakari alichoniambia ni 'digest' halafu nitajua nafanya nini - Gwajima
Kwa upande wake Maalim Seif ambaye alizuru kwa Gwajima kwa ajili ya kumjulia hali na kuzungumza naye masuala mbalimbali ya nchi, amesema anamuunga mkono mchungaji huyo kwa chochote atakacho kufanya.
“Namuunga mkono aliyoyasema, sisi ni marafiki wa muda mrefu nimekuja kumjulia hali na kuzungumza naye mambo mbalimbali na kila mmoja kayaeleza yake,” amesema Maalim Seif.
Na Regina Mkonde