Maalim Seif kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uongozi katika chama cha ACT-Wazalendo

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Ndugu Maalim Seif Sharif Hamad anatarajiwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya uongozi ndani ya ACT Wazalendo leo tarehe 30 Januari 2020. Zaidi soma taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Maalim Seif hapa chini:

.......

TAARIFA KWA UMMA

MAALIM SEIF KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA NAFASI YA UONGOZI KATIKA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO

Kama inavyofahamika, Chama cha ACT Wazalendo tayari kimetangaza rasmi kuanza kwa Uchaguzi wa Viongozi wa Kitaifa ndani ya Chama baada ya kukamilika chaguzi katika ngazi za chini. Shughuli ya kuchukua na kurejesha fomu kwa nafasi mbali mbali za uongozi katika ngazi ya Taifa imetangazwa kufanyika kuanzia tarehe 27 Januari hadi 26 Februari, 2020.

Kwa taarifa hii, tunawajulisha kuwa leo siku ya Alkhamis, tarehe 30/01/2020 saa 5.00 asubuhi Maalim Seif Sharif Hamad anatarajia kuchukua fomu ya kugombea nafasi mojawapo kati ya nafasi za uongozi zilizotangazwa kugombewa katika Chama Cha ACT Wazalendo. Shughuli hiyo itafanyika Ofisi Ndogo ya Chama iliyopo Vuga, Zanzibar.

Kwa taarifa hii, ndugu waandishi wa habari mnaalikwa rasmi kushuhudia tukio hilo la uchukuaji wa fomu. Maalim Seif pia anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu dira na mwelekeo wake juu ya nafasi ya uongozi anayokusudia kuiomba katika Chama.

Nyote mnakaribishwa.

Imetolewa na;

Ofisi ya Maalim Seif Sharif Hamad
30/01/2020

-------- UPDATE-------

Maalim Seif.jpg

EPhEF77WsAEC80q.jpg
 
Yes, naona Zitto anapumzika!! safi saana - tactical switch !!
 
Tunamtakia kila la kheri, Maalim ni kiongozi mwenye misimamo na asie tetereka na mwenye experience and education katika siasa. Ana nguvu na yupo timam. Good luck
 
Demokrasia ya kweli katika vyama imebaki ACT pekee yake
Huko kwingine ni maigizo tupu
 
Back
Top Bottom