VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Siasa ina vituko vyake. Katibu Mkuu wa CUF,mpiganaji wa siku nyingi na mwanasiasa mkongwe, amenaswa na mtego wa CCM. Amemezwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar lakini mikono mitupu. Yeye ni Makamu wa Kwanza wa Rais lakini asiye na mamlaka yeyote-hata kukaimu Urais hawezi. Hateuwi,haondoi,haonyi,haagizi wala hakatazi. Mamlaka yote yako kwa Rais Shein na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd. Afadhali hata Mawaziri watokao CUF. Kimsingi,Maalim Seif amebahatika kupata ving'ora tu. Hongera zake!