Maalim Seif: Jussa ni jembe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim Seif: Jussa ni jembe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgomba101, Oct 7, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema kuwa hatua ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu kujiuzulu nafasi hiyo ni pigo kubwa kwake na kwa chama hicho kwani alikuwa ‘jembe'.
  Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Maalim Seif licha ya kueleza kuumizwa na msimamo wa Jussa, alitoa siri kwamba alionesha azma ya kutaka kuachia ngazi tangu Julai mwaka huu kwa madai kuwa ana majukumu mengi.
  Mbali ya kuwa Naibu Katibu Mkuu, CUF Zanzibar, Jussa pia ni Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe.
  "Hata hivyo baada ya kunipa ujumbe huo nilimwambia kuwa ni vyema suala hilo akamwambie Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba kwa kuwa yeye ndiye mwenye dhamana ya uteuzi," alisema Maalim Seif.
  Alisema baada ya majibu hayo, Jussa alikubali, lakini Profesa Lipumba, kutokana na uzito wa suala hilo, aliamua kulipeleka katika kikao maalumu kinachowahusisha viongozi wa juu wa chama akiwemo mwenyekiti mwenyewe, Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu kwa majadiliano zaidi.
  "Kikao hicho kiliamua kujadili suala hilo kwa kina na baadaye wakamshauri asifanye maauzi hayo hadi uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu utakapomalizika kwa kuwa huenda lingeweza kuleta dosari katika kampeni, naye bila kusita alikubali ombi letu," alisema Maalim Seif.
  Maalim Seif alisema Jussa, juzi aliwasilisha barua ya kuachia ngazi na kumkubalia kwani alibaini kuwa alidhamiria kuachia nafasi hiyo.
  "Tumemkosa mtu muhimu sana asiyekuwa mbinafsi jambo linalopaswa na wengine tufuate nyayo zake kwa kuiga tabia ya kutotaka kujilimbikizia madaraka.
  "Jussa hakuhama chama ila ameamua kuwatumikia wananchi wake wa Mji Mkongwe na kutaka kuibana zaidi Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar kupitia Baraza la Wawakilishi," alisema Maalim Seif.


  My take: Jembe bila kuingizwa mpini haliwezi kulima!!
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hayo ndio matokeo ya Vision 4 change?? Jussa ameona chama hakina dira,amejitoa mnamuita "JEMBE" huu ni unafiki mkubwa.Ndoa ya CCM na CUF inaanza kufa muda si mrefu CUF atapewa talaka.Tatizo ni Maalim na profesa Lipumba wamekifanya chama kuwa mali yao.
   
 3. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #3
  Oct 7, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Unafiki wa kauli ya maalim uko hapa Ā“Tumemkosa mtu muhimu sana asiyekuwa mbinafsi jambo linalopaswa na wengine tufuate nyayo zake kwa kuiga tabia ya kutotaka kujilimbikizia madaraka". Kama alikuwa ana yajua haya toka awali kwa nini alikataa ombi la Hamad Rashid?!anajua kuwa na yeye amejilimbikizia alipaswa kuviachia na kuwapa wengine nafasi ya kikijenga chama chake! Cuf sasa hivi inakufa kwa kasi kuliko wakati wowote ule kwenye historia ya miaka 20 ya siasa za vyama vingi! Hivi ninavyo andika kwa huku Tanga hakina mwenyekiti.
   
 4. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Rip Cuf!
   
 5. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jussa ni jembe kwa ubaguzi na kudai zanzibar yake!
   
 6. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jembe kwelikeli kwa kuchochea chuki!Jusa Jembe!Kwa kuchoma makanisa Jusa jembe!!Jembe la kihindi linaloutaka usultani urudi zenji!Jembe sana hili kwa kuchochea Udini na kuwapania wakrito!!!Jusa Jembe maana limekariri hadith za mtume zote na kuzitumia kunyanyasa wenzake!!!Jusa Jembe...Mtawala ajaye wa weusi wa zanzibar,,,,...!!!???###Jusa Jembe
   
 7. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jussa ni jembe kwa kuendelea kukataa Utawala wa Kitanganyika ndani ya Zanzibar. Jussa ni jembe kwa kukataa mfumo kristo usitawale Zanzibar. Jussa ni jembe kwa kutokubali kasumba za kikoloni kuwagawa wa zanzibari. Jussa ni jembe kwa kukataa kumuabudu dikteta Nyerere...
   
 8. p

  propagandist Member

  #8
  Oct 7, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kapumzike jembe la ukweli lililoenda shule sio kama sugu.
   
 9. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 10. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Maalimu wakati anakwenda unda upnzani feki hakunagalia mbali sana na kama alingalia mbali basi alingalia zaidi malengo ya kutawaliwa na mashariki ya kati.

  Maalimu alijenga chama katk misingi iliyokuwepo ktk jamii za wazanzibar.Jamii zilizokuwa na mahubiri mengi ya kichinichini ya udini,ubaguzi wa pande, kama Unguja n pemba,zanzibar na Tanganyika.Aliona kuwa ndio njia nyepesi ya kutokea ,huku akishindwa jua gharama ya kuja reverse hii mitazamo ni kubwa sana au isiwe inalipika.

  Kwa kutumia taarifa mbalimbalia zinazoitwa "siri za muungano", "historia ya muungano","historia ya ukombozi na uhuru", ukooni toka bara, mfumo Chritu etc maalimu alikuza CUF.Vyote haivi maaalimu alikuwa akijua na kuamini kuwa mengi yamepotoshwa na mengine hayana ukweli wowote.Ila kwa jinsi alivyokuw aka enjoy support ya wafuasi wake na walichokuwa wakiamini naye akaghalifika na kujikuta naye akiaminishwa na wafuasi kuw ayupo sahihi.hapa kama ilivyo kwa wasomi wengi wa tamaduni za mashariki ya kati wanapoambiwa kuw awalichodhani kuwa si kweli ni kweli kabisa basu hujawa na moyo sana na huwa hawajiulizi sana ukweli wa mambo.

  Sasa maalimu kaacha nchi kama ilivyo,na yeye kwa umri aliofikia ndio ule kama wa mwinyi,umri wa kupenda sana dini,ni umri ambao atajikuta akijiwekea mikapa katika suala la udini.Kwani sasa ndipo atajiona kuwa kusaidia dini kuendelea ni sehemu ya jukumu lake,bila kujua alishapanda udini mbaya sana na anodhani kuwa waumini actually si waumini shaihi kifikra ni wale wabaguzi aliosaidia wapotosha.

  Hii ndio sad end ya siasa za watu kama hawa wasio mbali zaidi ya yalipo matumbo yao.Kizazi kingine cha akina Zitto,Makamba na Jussa kitaacha radicalism in another level and number
   
 11. Rapherl

  Rapherl JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 3,308
  Likes Received: 1,489
  Trophy Points: 280
  Jembe????
   
 12. s

  saliha Member

  #12
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  haha ukweli ukidhiri uongo hujificha tutaona mengi ,kuishindikiza serikali ya umoja kufanya nini vile?mama nafa
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Mie nangoja ccj ninunue kakobe aka vw
   
Loading...