Nimeipenda 'facial expression' ya Maalim Seif. Wenzake yaonekana wana mawazo mengi mno. Yawezekana ni kwasababu hawana uhakika na huko mbele. Ama ni kwasababu wanawaza majukumu mazito watakayobeba huko mbele. Lakini Maalim Seif yuko at 'ease' na anauhakika mkubwa. Ni haiba yake ama ni kweli anafuraha na uhakika!!? Nimeipenda na yawezekana ni mtu wa tajuwidi (meditation).
Yaelekea hujanielewa mkuu. Kilichoni-fascinate kwenye hiyo picha ni 'facial expression' ya Maalim Seif. Kwa kipindi ambacho chama chake ama upinzani unapitia, kwa nafasi yake ni lazima angekuwa mtu mwenye mafikara mengi. Na sura ingeonyesha wazi ile hali ya kutokuwa na utulivu nafsini. Ukimuangalia Mbatia pale kulia (amefichwa kidogo na camera) yaonekana ana mawazo. Mbowe na Duni halikadhalika nao nafsi zao si shwari. Lowasa nae pia anaonekana ni mtu aliyepo kwenye mafikara. Lakini Maalim amenivutia sana. Huwa napenda watu wenye utulivu. Nadhani unajuwa faida za utulivu wa nafsi hasa wakati wa kufanya maamuzi. Huwa nawaheshimu watu wa namna hii. Si jambo rahisi kama watu wengi tunavyofikiria. Utulivu wa nafsi huchangiwa sana na tajuwidi (meditation). Mimi ni mpenzi wa tajuwidi, labda ndiyo maana nikavutiwa na Maalim na nikaamuwa kuongea. Hakuna 'political attack' yoyote kwenye uzi wangu. Hata kama ipo, ni 'fact' ndiyo inayo-attack siyo mimi.