Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amewaambia wafuasi wao kwamba wataendelea kudai ushindi wa chama chao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Maalim Seif aliondoka nchini jana kwenda Marekani na kesho atazungumzia kilichojiri kwenye Uchaguzi Mkuu na kusababisha chama chake kususia uchaguzi wa marudio wa Rais wa Zanzibar ulioipa CCM ushindi.
Mwanasiasa huyo anatarajiwa kutoa mhadhara katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Elimu ya Kimkakati na Kimataifa cha Marekani (CSIS) na utafanyika makao makuu ya taasisi hiyo mjini Washington DC kuanzia saa nne asubuhi.
Mkwamo wa kisiasa Zanzibar uangaliwe kwa jicho la ziada, vinginevyo utachukuwa sura ya mgogoro wa Kimataifa.
Mataifa mengi makubwa huchangamkia mianya kama hii ya migogoro kwenye siasa za mataifa machanga kujipenyeza wao na ajenda zao za kibepari.
Source: Mwananchi