Maalim Seif ajitosa tena urais Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maalim Seif ajitosa tena urais Zanzibar

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, May 10, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Maalim Seif ajitosa tena urais Zanzibar

  SIKU moja baada ya mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kutangaza nia yake ya kugombea urais wa Muungano, katibu wake, Maalim Seif Sharif Hamad ametangaza rasmi nia ya kugombea urais wa Zanzibar.

  Maalim Seif, ambaye aliwahi kuwa Waziri Kiongozi wakati wa utawala wa Aboud Jumbe, atakuwa akiwania urais wa Zanzibar kwa mara ya nne tangu mfumo wa siasa za vyama vingi urejeshwe.

  Maalim Seif, ambaye alikuwa akitarajiwa kugombea tena na ambaye hatarajiwi kuwa na mpinzani, amesema anasubiri muda wa kuchukua fomu utangazwe kwa mujibu wa chama chake ili achukue.

  “Mimi nadhani kuna haja ya kuvunja ukimya. Ni kweli kabisa mimi ambaye ni mwanachama halali wa CUF nakusudia kugombea urais wa Zanzibar kwa mara nyingine,” alisema Maalim Seif.

  Maalim Seif alisema anachoomba ni afya njema na kwamba hivi sasa yuko ngangari kuingia katika mapambano hayo ya urais wa Zanzibar.

  “Wakati wowote muda wa kuchukua fomu ukitangazwa nitachukua fomu na kusubiri ridhaa ya wanachama katika mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni mwaka huu,” alisema Maalim Seif.

  Kwa mara zote tatu ambazo amegombea urais wa Zanzibar maalim Seif amekuwa akishindwa kwa ushindi mwembamba na wapinzani wake kutoka CCM, matokeo ambayo yamekuwa yakipingwa na CUF na kufanya hali ya kisiasa visiwani humo kuwa tete kwa muda mrefu.

  Awali akisoma maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la CUF kilichomalizika juzi usiku, Profesa Lipumba alisema kikao kiimepitisha ratiba ya mchakato wa kura za maoni za kuwapata wagombea wa nafasi za urais, ubunge, uwakilishi na udiwani Tanzania Bara na Zanzibar.

  “Baraza linatoa wito kwa wanachama wote wa CUF kuheshimu na kufuata matakwa ya katiba ya chama na kanuni za uchaguzi wakati wa zoezi zima la kupiga kura ya maoni na hivyo kuhakikisha kuwa demokrasia ya ndani ya chama inaimarika,” alisema Profesa Lipumba.

  Alisema baraza limeridhika na maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa CUF uliopangwa kufanyika mwezi Juni mwaka huu, kwa ajili ya uteuzi wa wagombea wa urais wa CUF.

  “Baraza pia limeridhia uamuzi wa mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuwa miongoni mwa wanachama watakaogombea nafasi ya urais wa Muungano katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

  “Lengo kuu ni kuwapatia Watanzania uongozi makini chini ya chama mbadala CUF na makini hapa nchini.

  Baraza linatoa wito kwa wanachama wengine wa CUF wenye sifa na uwezo kujitokeza kutangaza nia zao na kuchukua fomu za kugombea nafasi ya urais wa Muungano na Zanzibar,” alisema Lipumba.

  Lipumba alimvaa Rais Jakaya Kikwete, akimtaka kutoingia mitini katika mijadala ya moja kwa moja ya wagombea urais kupitia vyombo vya habari.

  “Tunataka mwaka huu Rais Kikwete asiingie mitini... aje tukutane katika mijadala ya televisheni baina ya wagombea kama wanavyofanya Wamarekani na Uingereza na sio aende pekee katika TV,” alisema Profesa Lipumba.

  “Tunataka Watanzania wajue ubovu wa rais wao ili waweze kufanya maamuzi mazito katika uchaguzi huu kwa kuking’oa chama tawala,” alisema Lpumba.

  Profesa Lipumba alisema CUF inaunga mkono madai ya msingi ya wafanyakazi yaliyotolewa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) na kuitaka serikali kuboresha maslahi yao.

  “Baraza kuu limesikitishwa sana na kauli za vitisho, aibu na kufitinisha wafanyakazi na wananchi kwa serikali kutoa habari na taarifa zisizo na ukweli kamili ili kuwapaka matope viongozi wa Tucta,” alisema profesa Lipumba.

  “Mheshimiwa rais amepewa dhamana kubwa na wananchi ya kuwaongoza na kuwatatulia matatizo yao pale yanapojitokeza, lakini kwa kitendo chake cha kukurupuka na kuwahukumu hadharani viongozi wa Tucta si cha kuwatendea haki hata kidogo Watanzania hasa ikizingatiwa dhamana kubwa waliyompa.”

  Lipumba alisema baraza kuu la CUF limeona haikuwa busara kwa mheshimiwa rais kutumia jukwaa la wazee wa vijiweni wa CCM, ambao si wafanyakazi, kuelezea matatizo ya wafanyakazi.

  “Baraza linalaani vitisho alivyovitoa rais kwa wananchi na wafanyakazi nchini na vinaonyesha namna serikali ya CCM inavyokosa uvumilivu na uchungu kwa watu wake na kushindwa kuheshimu uhuru wa wananchi kutoa sauti zao,” alisema Lipumba.

  “Vitisho vya aina yoyote katika zama hizi za demokrasia havikubaliki hata kidogo na vinapaswa kulaaniwa na kupigwa vita na wapenda amani na haki wote nchini, kwani vikiachwa vinaweza kuipeleka nchi yetu pabaya.”

  Alisema baraza linawaomba wafanyakazi na wananchi kwa ujumla nchini wavumilie vitisho na kashfa walizofanyiwa na Rais Kikwete, badala yake wavigeuze kuwa changamoto kwao kwa kuweka nguvu zaidi za kudai haki zao bila ya kuchoka.

  Lipumba alisema katika kufikia hatima njema ya maridhiano ya CUF na CCM Zanzibar baraza kuu linaitaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kurekebisha mapungufu makubwa yaliyojitokeza katika zoezi la uandikishaji visiwani humo.

  “Hadi sasa, katika majimbo yaliyokusanywa takwimu tu, zaidi ya Wazanzibari 15,000 wenye haki ya kuandikishwa katika daftari la wapigakura wamenyimwa haki hiyo ya kikatiba,” alisema Profesa.

  Source: Nipashe
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  mwaka huu atachukua, hakuna mpinzani kule visiwani, ninachohofia tu akishachukua, ni muungano...hapo ndo utakaposambaratika....
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.  Uamuzi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, kugombea urais Zanzibar kwa mara ya nne, umeungwa mkono na wananchi wengi visiwani hapa.
  Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti katika Manispaa ya Zanzibar, baadhi ya wananchi walisema uamuzi wa Maalim Seif kugombea nafasi hiyo ni mwafaka.
  Walisema tangu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi Zanzibar, hakujawahi kuwa na uchaguzi huru na wa haki ndio maana Maalim Seif amekuwa hatosheki kugombea nafasi hiyo.
  Aidha, walisema Maalim Seif anaonekana bado ana mvuto wa kisiasa kwa wapiga kura na moyo wa subira licha ya kutofikia malengo ya kisiasa katika chaguzi zote Zanzibar.
  Mfanyabiashara Mohammed Kombo Mussa alisema kitendo cha Maalim Seif kugombea tena siyo vibaya kwa vile bado anauzika katika ‘soko la wapigakura’.
  Alisema pamoja na CUF kuwa na viongozi wengi, bado hajapatikana kiongozi mwenye uwezo wa kisiasa wa kuwaunganisha Wazanzibari wa Unguja na Pemba kutokana na muelekeo wa siasa za Zanzibar.
  Alieleza Maalim Seif amepita katika hatua nyingi za kisiasa nchini ndiyo maana hadi sasa bado ana mvuto wa kisiasa akilinganishwa na viongozi wengine ndani ya chama hicho.
  “Hakuna kiongozi mwenye uwezo wa kuunganisha watu wa Unguja na Pemba zaidi ya Hamad na Juma Duni ni kiongozi kijana, lakini Pemba hawezi kukubalika hata kama atachukua fomu ya kuomba kugombea urais,”alisema Ramadhani Shabani mkazi wa Mbweni.
  Naye Asha Said Mohammed mkazi wa Kilimani, alisema kutokana na mazingira ya uchaguzi wa Zanzibar unavyofanyika, ndiyo maana viongozi wa vyama wamekuwa wakigombea zaidi ya mara moja kwa kuamini uchaguzi haukuwa huru na wa haki.
  Alisema Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, umekuwa haufanyiki kwenye mazingira ya uwazi, badala yake umekuwa ukitawaliwa na vitisho vya majeshi, jambo ambalo halileti sura nzuri katika misingi ya kidemokrasia.
  Hata hivyo, mfanyabiashara katika Soko Kuu la Darajani ,alisema haikuwa muafaka Maalim Seif kutangaza kugombea tena kwa mara ya nne wakati kwenye CUF kuna viongozi vijana, ambao wameshakomaa kisiasa.
  Aidha alisema Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), inapaswa kuweka mazingira mazuri ya uchaguzi ili uwe huru na wa haki na kuondoa malalamiko ya viongozi wa vyama vya siasa kwamba hawatendewi haki katika uchaguzi.
  Mfanyabiashara Burhani Said Rashid, alisema maridhiano yaliyofikiwa kati ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Maalim Seif, bado ni msingi mzuri utakaosaidia Zanzibar kufanyika uchaguzi huru na wa haki iwapo yatatekelezwa kwa nia njema katika uchaguzi ujao.
  Alisema tangu kufikiwa kwa maridhiano, hali ya utulivu na amani, vimetawala Zanzibar na kuwataka viongozi watakaosimamishwa na vyama vyao kugombea urais visiwani hapa kudumisha umoja na mshikamano uliopatikana tangu kufikiwa kwa maridhiano. Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano na Umma wa CUF, Salim Bimani, alisema kujitokeza kwa viongozi hao kugombea kwa mara ya nne urais, hakuwazui wanachama wengine kujitokeza kuwania nafasi hizo.
  Aidha, alisema CUF inaheshimu demokrasia na inatoa wito kwa wanachama wake wenye nia ya kuwania nafasi za urais kujitokeza kabla ya uteuzi wa chama kufanyika.
  Tayari Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Maalim Seif wametangaza nia ya kugombea tena urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31, mwaka huu.
  CHANZO: NIPASHE
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kwanini Seif asiutake Urais Muungano, halafu Lipumba awe mgombea Mwenza?
   
 5. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa ndo nachokaga na upinzani. Hawa nafikiri ndo wanaua ladha ya upinzani. wananchi wanataka mabadiliko lakini upinzani wanaleta watu wale wale kila mwaka.
  Inaashiria nini mtu ashindwe mara tatu bado mnamleta huyo huyo. vyama ni vyao au hakuna watu wengine wenye uwezo.
   
 6. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Tupatie ushahidi kama kashindwa kwenye uchaguzi.Mtu kama hujuwi masuala ya Zanzibar au si mzanzibari, stay out of it.
  Sisi wazanzibari tushamweka huyo mtu agombanie mara 3, na chaguzi zote zimechafuliwa ili asituongoze njia na visiwa vyetu.

  Na mara hii bado tunamtaka yeye.Sasa wewe unaetoka Mbagala umechoka vipi?
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  May 14, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Shee Yaya nimemkubali
   
 8. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  It doesnt really matter that much...its Zanzibaris or CUFs choice on this one.
  This guy is like a hero to us, so no bla bla from Mbagala....May be you should start another thread to discuss JK (President of Tanganyika)....
   
 9. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #9
  May 25, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Umri na uzoefu wa kuwa nje ya utawala umemsaidia sana Maalim. Hivi sasa hata ukimsikiliza anavyohutubia mikutano inaonyesha ni mtu aliyokomaa. Mimi siyo mwanachama wa CUF wala siyo mpenzi wa chama hicho ila ninaamini akifanikiwa kupata urais znz atakuwa rais bora sana. He is more realistic and pragmatic than ever
   
 10. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mr Frasty Umeanza
  Humu JF kila mtu anahaki ya kutoa mawazo/maoni kama aonavyo. Tunazungumzia mambo ya marekani, uingereza nk sasa iweje umdhihaki mtu wa mbagara????
  Mbona wewe huchangia kwenye mambo ambayo siyo ya muungano????? Wacha kuwa myopic and let free thinking flow because it is god given right.
   
 11. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 701
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hakuna dhihaki hapo, kweli tupu.Let Zanzibaris decide whats best for their land....I wont bother about Mbagala, as I actually dont care whats going on in that peace of land...

  Au ndio idea za ukoloni, lazima muitie mdomo Zenj 24/7....
   
 12. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Go Ahead gag your self but that wont stop others to speak about zanzibar or any other issue they see it fit.
  Pengine hii JF haikufai maana hapa anything goes sasa labda uingie kwenye blogs za wazanzibari exclussive. Hapa bro ni haki ya kila mwana JF be it mtanzania au taifa lolote lile ana haki ya kuzaliwa [siyo ya kupewa]kuongea, kutoa mawazo yake and thats it bro.
   
Loading...