Maalim Seif aiandikia barua ZEC, kujitoa rasmi kwenye uchaguzi wa Machi 20

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
maal seif.jpg

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ameithibitishia rasmi Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) kujiondoa kuwania wadhifa huo katika Uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20, mwaka huu.

Mbali na Maalim Seif, wagombea wote wa chama hicho wa nafasi ya Uwakilishi na Udiwani wamejiondoa kwa kuwasilisha barua rasmi kuwa hawatoshiriki uchaguzi huo wa marudio wa Zanzibar.

Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, amesema Maalim Seif amewasilisha waraka wa barua wa kujiondoa kwa Zec, Febuari 8, mwaka huu.

Amesema hatua aliyochukuwa mgombea huyo ni utekelezaji wa wa azimio la Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF kutoshiriki uchaguzi mkuu wa marudio visiwani hapa.

Shehe alisema kuwa Zec imetakiwa kutotumia jina wala picha za Maalim Seif na taarifa zozote katika karatasi za wapigakura kabla ya kufanyika uchaguzi huo.

Alisema kuwa katika Barua yake Maalim seif amesisitiza kuwa uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana ulikuwa uchaguzi huru na wa haki na Mwenyekiti wa tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Jecha salim Jecha hakuwa na mamlaka ya Kikatiba na sheria kufuta matokeo ya Uchaguzi huo.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Salum Kassim alisema jana kuwa ni mapema kueleza vyama vingapi vimekamilisha kuthibitisha wagombea wake kama wapo hai na watashiriki uchaguzi kabla ya kufanyika Machi 20, mwaka huu.

Chanzo: Mpekuzi Blog
 
Hakuna haja ya mgombea wa nafasi yeyote ile toka chama cha CUF wala umoja wa Ukawa kushiriki ktk uchaguzi huo. Hao viongozi wa vyama vingine nje ya Ukawa waache tu waendelee na harakati zao kwani hao ndio wslionunuliwa ili ionekane kama vyama vimekubali kushiriki uchaguzi huo . Pia hongela Maalim Sefu kujitoa kwani jina lako lingetumika kuhesabia kama umepata kura ngapi ili wanaemtaka ionekane ameshinda kwa kishindo
 
Amesema hatua aliyochukuwa mgombea huyo ni utekelezaji wa wa azimio la Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF kutoshiriki uchaguzi mkuu wa marudio visiwani hapa.

Baraza kuu la taifa la taifa lipi lililotoa tamko la CUF kutoshiriki? Lile lililofanyika Tanzania bara na tamko lake likasomwa na mtanzania bara? Au kuna agizo la baraza kuu la CUF la nchi ya Zanzibar ndio lililotoa tamko hilo.

Kama ni tamko lililotolewa na baraza kuu la CUF zamzibar liko sawa kisheria ni haki yao kutekeleza lakini kama ni lile lililofanyika bara ni feki wazanzibari walipuuze.Mambo ya uchaguzi wa Zanzibar hayamhusu kabisa mtanzania bara hata awe mwenyekiti wa CUF taifa sembuse mjumbe wa baraza kuu kutoka bara.

Nilimshanga Wakili TASLIMA siku ile anasoma hilo tamko analoliita la baraza kuu!!!.Lilisomwa na mtanzania bara,kwenye ardhi ya Tanzania bara mlipuuze.Endeleeni na uchaguzi.

Seif Sharrif Hamad ana roho mbaya akikosa yeye anataka na wajumbe wote wa baraza la wawakilishi wa CUF wasigombee hata kama walikuwa na uwezo wa kuchaguliwa.

Halafu SEIF sharriff Hamad dikteta alitakiwa yeye ndie atangaze kujitoa na awaachie wengine mmoja mmoja waandike barua wao wenyewe za kujitoa.Hawezi kuwasemea.
Natamani atokee mmoja aseme mimi nitagombea na nitashiriki uchaguzi kwa tiketi ya CUF na eneo aliloko wamsainie fomu zake tuone.

Naisihi ZEC waipuuze hiyo barua YA KUTOSHIRIKI.Wasubiri mgombea mmoja mmoja apeleke barua ya kujitoa.Asipopeleka barua ya kujitoa kwa sababu uchaguzi ni wa marudio wawaache kwenye karatasi wapigiwe kura.Tusiruhusu mtu mmoja kuwasemea wengine au kuwaamulia wengine.

Huu ni uchaguzi wa marudio wagombea ni wale wale watake wasitake

Tume iwatetee hao wanyonge wengine waliogombea uwakilishi kupitia CUF wasionewe na CUF
 
MKUU UNAMAANISHA NINI UNAPOSEMA "MAALIM AKIKOSA YEYE HATAKI WENGINE WAPATE"? ALIKOSA LINI? ALIKOSA NINI?
 
ALIKUWA ANASUBIRI NINI??????????

ANAPIMA MAJI YA BAHARI KWA MGUU, AYA SASA???
 
MKUU UNAMAANISHA NINI UNAPOSEMA "MAALIM AKIKOSA YEYE HATAKI WENGINE WAPATE"? ALIKOSA LINI? ALIKOSA NINI?

Alipokua CCM inaelekea kushinda aliamua kuvuruga uchaguzi kwa kukurupukuka kujitangaza mshindi kabla ya kusubiri tume itangaze.Alitaka serikali imkamate vurugu zitokee wakose wote nchi isitawalike
 
Ningeshauri aite waandishi kabisa ili dunia ijue amejitoa kwa maandishi na sababu aseme!
 
Back
Top Bottom