Zanzibar 2020 Maalim Seif: ACT-Wazalendo kimelenga kutoa kipaumbele kwa Wanawake wasibaki kuwa wasindikizaji katika Uongozi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad (pichani), amesema wanawake ni jeshi kubwa linalotegemewa kushiriki katika uchaguzi mkuu na kuleta ushindi.

Maalim Seif alisema hayo wakati akizinduwa timu ya ushindi ya uhamasishaji kwa wanawake kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020.

Seif alisema chama cha ACT-Wazalendo kikiingia madarakani kimelenga kutoa kipaumbele kwa wanawakewasibaki kuwa wasindikizaji katika uongozi.

“ACT-Wazalendo tumejipanga vizuri tukishinda uchaguzi mkuu nafasi nyingi za uongozi kuanzia uwaziri, katibu mkuu na ukurugenzi tutahakikisha zinashikiliwa na wanawake,” alisema.

Mmoja wa viongozi wa timu ya uhamasishaji wanawake wa ACT Wazalendo, Janet Fussi, aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kukihakikishia chama hicho ushindi.

Alisema huu si wakati wa wanawake kubaki nyuma na kwamba, matarajio yake makubwa ni kuona ACT-Wazalendo ikiingia madarakani, wanawake wanashika nafasi katika nyanja mbalimbali za uongozi.

“Wanawake wenzangu naomba tusibaki nyuma katika kazi za uhamasishaji wa chama ikiwemo kuhudhuria mikutano ya hadhara ya kampeni ili kukipa hamasa chama,” alisema.

Naye Zahra Hamadi aliwapongeza wanawake wa chama hicho kwa kushiriki katika mikutano ya kampeni zinazofanyika nchini kote huku akiwasisitiza kukiunga mkono chama hicho.

“Tunawapongeza kwa dhati wanawake wa chama cha ACTWazalendo kwa sababu hawakubabaika katika kipindi chote cha misukosuko iliyopita katika chama,” alisema.

Chama cha ACT-Wazalendo tayari kimezindua timu ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu ikiongozwa na Nassor Mazrui na kimewahakikishia wanachama na wafuasi wake kujitayarisha kwa ushindi licha ya kuchelewa kuzindua ilani ya uchaguzi.
 
Mbona ACT ngazi za juu za chama wamejaa wanaume wengi zaidi ya hao wakinamama,kwanini wasengeanza sasa kuonyesha mfano ndani ya chama chake?
 
Back
Top Bottom