Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,948
Katika siasa za Kilaghai, nachelea kusema bila shaka Chama chetu pendwa kinaweza kuwa kinaongoza kama siyo katika Dunia basi ni katika Afrika.
Chama chetu kilifanikiwa kwa ukamilifu kuisambaratisha CUF kwa nguvu za ndani na nje. Nje kulikuwa na Mtungi wa pombe, Polisichama na Sirikali. Ndani kulikuwa na Mtatatiro.
Mbinu zilizosukwa na chama pendwa zilikuja kwa namna ambayo hakuna aliyetegemea. Zilikuwa ni mbinu za kiwango cha juu sana cha ujasusi na kilaghai. Mtatatiro alifanikiwa kujitambulisha na kuonekana yupo upande wa Maalim, na Maalim na wafuasi wake wote wakamwamini Mtatatiro.
Kwa upande wa pili Propesa alihadaiwa na kufanywa ndiye kiongozi anayetakiwa na sirikali na sirikali ikamlinda kama kiongozi wa CUF. Akaaminishwa pia Mtatatiro hapendwi kabisa na chama pendwa wala sirikali yake kumbe kiuhalisia ndiye aliyekuwa karibu zaidi na chama chetu kuliko hata yeye Propesa.
Ukisikia siasa za kijasusi na kilaghai ndiyo hizo. Ni pale unapowafanya mahasimu wako, wagombane wenyewe kwa wenyewe, na yule msaliti wao mkuu wamwamini kwa kiwango cha juu. Mtatatiro kaifanya kazi kiweledi hasa, na sasa yupo kivulini.
Vyama pinzani vimekosa intelijensia ya kuweza kutambua nani ni mwenzao na nani ndiye msaliti wao mkuu.