Maalif Seif: TWAWEZA mngefanya utafiti wa Escrow

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,583
Reaction score
140,003
Haaah,haaa Makamu wa Rais no.1 wa Zanzibar amewakosoa Twaweza kuwa wamefanya utafiti wa kishabiki kuwapamba mafisadi,amewashangaa na kuongeza kuwa ingeleta tija kama wangefanya utafiti kuhusu Escrow na upungufu wa madawa.Ni ajabu nchi ipo kwenye bonde la uvuli wa mauti,halafu wengine wanakuja na porojo za urais.Gazeti la Majira limeripoti
 
Utafiti hufanywa kwa vitu ambavyo havijafanywa. Kwani nchi hii ni nani asiyejua kuwa ina uhaba wa madawati? Ishu ya escrow si inajulikana! .mi naona sio dhambi kwa twaweza kufanya walivyofanya maana nalo ni jambo muhimu kwa mustakabali wa kesho
 
Naona km ngekewa, eeh eeeh ngekewa!
 
Utafiti hufanywa kwa vitu ambavyo havijafanywa. Kwani nchi hii ni nani asiyejua kuwa ina uhaba wa madawati? Ishu ya escrow si inajulikana! .mi naona sio dhambi kwa twaweza kufanya walivyofanya maana nalo ni jambo muhimu kwa mustakabali wa kesho
Haha haaa mtafiti we unataka vitu vipya tu??!!
Rudia vitabuni
 
Seif aache Ubabaishaji, yeye hivi sasa ni Kiongozi jukumu lake ni kuwaambia wananchi amewaleteaje Maendeleo Zanzibar, aeleze maendeleo yapi yamepatikana kwa kuwa kwake Makamu wa Rais pamoja na MA CUF wenzie waliopata Ngekewa ya Prof Kikwete kujumuishwa kwenye Serikali.
Anajifanya hajui maana ya Reserach kwani ESCROW inahitaji Comments za wananchi ili ujue kuwa kuna Wizi au la?
 
Utafiti hufanywa kwa vitu ambavyo havijafanywa. Kwani nchi hii ni nani asiyejua kuwa ina uhaba wa madawati? Ishu ya escrow si inajulikana! .mi naona sio dhambi kwa twaweza kufanya walivyofanya maana nalo ni jambo muhimu kwa mustakabali wa kesho

Unajua maana ya utafiti wewe? Katika Escrow ni kura ya maoni gani imefanyika kuuliza wananchi kama wanakubaliana yanayoendelea Escrow na nini kifanyike? Au swali kingine lolote lingeweza kuulizwa.
 
Utafiti hufanywa kwa vitu ambavyo havijafanywa. Kwani nchi hii ni nani asiyejua kuwa ina uhaba wa madawati? Ishu ya escrow si inajulikana! .mi naona sio dhambi kwa twaweza kufanya walivyofanya maana nalo ni jambo muhimu kwa mustakabali wa kesho
Kwani nchi hii nani asiyejua kuwa wasaka tonge mafisadi nk wanatoana macho kwa ajili ya kuwania urais.
 
Utafiti hufanywa kwa vitu ambavyo havijafanywa. Kwani nchi hii ni nani asiyejua kuwa ina uhaba wa madawati? Ishu ya escrow si inajulikana! .mi naona sio dhambi kwa twaweza kufanya walivyofanya maana nalo ni jambo muhimu kwa mustakabali wa kesho

Kwani kuhusiana na issue za siasa nchini tafiti nyingi si zimekuwa zikifanywa na taasisi mbalimbali na kuwapendelea chama cha magamba kila mara kwa hiyo ninaweza kusema hata hizi tafiti za TWAWEZA tulikuwa tunajua kuwa hazitaleta jibu tofauti na kama ile iliyofanywa na REDET....

Kwa hizi taasisi za bongo zinavyoendekeza njaa nina uhakika si ajabu siku wakaamua kutuambia kuwa wamefanya utafiti mwingine na wamegundua kuwa hata CCM wakisimamisha jiwe still litamshinda mgombea kutoka UKAWA
 
Hawa jamaa walikuwa wakifanya kazi nzuri kwenye tafiti za matatizo yanayoikabili sekta ya elimu na kutoa matangazo ya kuelimisha umma kuhusu changamoto za sekta ya elimu. Sijui nani amewashawishi kuingia kwenye tafiti za kisiasa?
 
Back
Top Bottom