Maajabu ya Tanzania yangu

Shukurani.

Wanaposema "hizi ni nafasi za Ajira mpya" wanamaanisha sharti hili ni kwa kazi mpya (newly created jobs) au nafasi zilizotangazwa tu kwa mfano kazi ipo siku nyingi ila mtu kastaafu inatangazwa vacancy mpya kwa kazi ambayo ipo siku nyingi?
Naaam,
Naamini ni kazi ambazo zipo siku nyingi.Lakini mkuu ukifuatilia vzr utaona kuwa utumishi kazi nyingi wanasema kabisa kuwa husiombe km ww ni mtumishi wa umma tayari.Hiyo nimepick randomly km risiti ili nikuoneshe km ulivoomba.
 
Vema sana
Sasa mimi siongelei kuhama ila naongelea ajira mpya yan it doesn't sound to me kuwa una ajira ila unataka tena na wale wasio na ajira je? Otherwise kufanyike utaratibu kuwa wao wasiopapenda uko wahame ila awa wasio na ajira ambazo zimechukuliwa na wenye ajira basi wao wapangiwe uko ili kuwe na uwiano sawia.Lengo ni kila mmoja apate na sio watu flan flan tu wapate keki ya taifa.
 
Unalaumu bure ndugu. Angalia waasisi wa hilo ni wanasiasa. Subiri oktoba utaona ma-RC, ma-RAS, DAS, DED, RC, Wakurugenzi na maafisa wa serikali wakiomba ubunge majimboni. Kwa nini wasiwaachie jobless waombe hizo nafasi???

Huu ndio mfumo wa kibepari, ukiwa dhaifu hauna chako. Nashauri jobless wenzangu wapambane tu kwenye usaili wawe best candidates. Hata hivyo kati nafasi 1500 za ajira za TRA kumbe hao wenye kazi hata 200 hawafiki. Unaona jinsi jobless zaidi ya 1300 wametoboa. Kulalamika hakusaidii.

Naibu Spika wa bunge aliomba Uspika wa bunge. Mifano ipo mingi. Naishia hapo Restless Hustler
 
 
Reactions: fox
Ahaa kinachokuumkza wewe ni kitendo cha mtu mwenye ajira kuomba ajira nyingine wakati kuna watu hawana kabisa. Sheria bado ni ileile kijana wangu, ukiwa ndani ya system ni rahisi kuhama na kuifikia nafasi flani kuliko ukiwa nje ya system. Pia kuna mdau amekujibu hapo juu kuwa, mwajiri hatangazi ajira ili kukuokoa wewe nawe upate ajira, anatangaza ajir ili kupata mtu sahihi wa kuifanya kazi iliyopo. Kama mtu sahihi tayari ana ajira nyingine, hio haimuondolei sifa na haki ya kuomba kazi yenye maslahi zaidi ya ile aliyonayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…