Maajabu ya MV Nyerere; michango ndio iliyolipa wafiwa na wahanga, na watoa huduma kujilipa laki 4 kila mtu. Serikali haijatoa chochote mfuko wa maafa

Jamani; hebu tuone nia njema ya uongozi wetu. Watu wamefiwa, wakapewa usaidizi wote wa gharama ya mazishi. Halafu bado 1mli. Ulitaka nini tena?? Ulitaka kila mtu apewe 50mil?? Nadhani serekali imefanya vyema kujenga hizo wodi. Kwani hazitaisha kwa mwaka bali zitakaa miaka huku zikisaidia wengi.
Wazo langu; Serekali iwakumbuke watoto walio achwa na wazazi/mzazi haswa kwenye elimu yao tu. Huko nako ni matumizi mazuri ya hiyo fedha.
Je isingetokea ajali hiyo... hayo mawodi yasingejengwa???? Naomba unijibu hili swali...
 
Hapa ndipo ninapowaona baadhi ya watanzania kuwa vichaa kamili. Yaani kijiji kinakusanya rambirambi kwenye msiba wa mazee Makanya, fedha 560,000/- inayopatikana inagawanywa sehemu 3. Tsh. 140,000/- inapewa familia ya marehemu, Tsh. 180,000/- wanapewa wachangishaji kama motisha na Tsh.240,000/- zitanunua kipaza sauti cha kijiji ambacho kitatumika kwenye mikutano ya kijiji ili kuwasaidia wanakijiji wote kufuatilia mikutano kwa usahihi. HUU MGAWANYO UNASHANGILIWA NA WANAKIJIJI!!!! Tanzania ni nchi ya amani na utulivu.
...

mkuu, hapa kuna watu hawatakueleqa kabisa yani.... lakini mwenye masikio na asikie
 
Wasiponielewa Leo watanielewa siku yakiwakuta. Yaani kama nchi tunaanza kushangilia serikali kutumia matatizo yetu kujipatia kipato na sifa binafsi kwa viongozi? Hivi hili lina tofauti gani na baadhi ya NGOs Zinazotumia watanzania wenye matatizo (Mf. UKIMWI) kujipatia fedha na kujinufaisha na fedha hizo huku waathirika wakiambulia kiduchu?
 
Tanzania ni nchi ya amani na utulivu.
Aksante kwa uelewa wako mzuri. Msituchafulie amani kwa kudai msivyo vitaabikia. Hivi ukiulizwa wewe umetoa ngapi unayo risiti?? Ulishaambiwa hata ukiingia hotelini kwa mama ntilie. Dai risiti. We ulitoa ngapi?? Acheni uchochezi
 
Mna kila kitu mnaweza kufanya chochote. Lakini laana ya rambirambi haitawaacha salama ipo siku mtalipa madhara yake.
 
Je isingetokea ajali hiyo... hayo mawodi yasingejengwa???? Naomba unijibu hili swali...
Nnai ajuaye?? Hapa kinachoangaliwa ni kwamba; Tusitumie resources zetu kipumbavu. Unampa mtu 50mil na sio mmoja bali wengi tu waende wakazichezee. We waona ni uongozi bora huo?? Serekali imetumia busara zaidi hapo. Je, wangelisema kuwa fesha hiyo ikajenge flyover Gerezani darisalama si mngeua mtu nyiye. Wodi zimejengwa pale pale kijijini kwao. mbona hamulioni hilo?
 
Mliongalia taarifa ya habari, nadhani mmesikia rambirambi zinakoelekezwa...

Pia ile milioni moja moja ambayo walisema wafiwa wangepewa nayo ilikuwa from rambirambi na siyo from the government funds.

Wale wapiga vigeregere karibuni....
na watu wanaochanga ni mazoba kweli. misiba ya namna hii siku za hivi karibuni, sio ya kuchangia. hii ni Mara ya tatu sasa Pesa za rambi rambi hazitumiki Kama wachangaji wanavyodhani.
 
Mliongalia taarifa ya habari, nadhani mmesikia rambirambi zinakoelekezwa...

Pia ile milioni moja moja ambayo walisema wafiwa wangepewa nayo ilikuwa from rambirambi na siyo from the government funds.

Wale wapiga vigeregere karibuni....
Naona maafa yaidhinishwe kama chanzo cha kuaminika cha mapato ya serikali.
 
Mna kila kitu mnaweza kufanya chochote. Lakini laana ya rambirambi haitawaacha salama ipo siku mtalipa madhara yake.

Kwani hiyo hela imeenda kuliliwa Kenya au hapa hapa home. Kukitokea laana ambayo wala haitokaa tokea itakukula hata weye.
 
Nnai ajuaye?? Hapa kinachoangaliwa ni kwamba; Tusitumie resources zetu kipumbavu. Unampa mtu 50mil na sio mmoja bali wengi tu waende wakazichezee. We waona ni uongozi bora huo?? Serekali imetumia busara zaidi hapo. Je, wangelisema kuwa fesha hiyo ikajenge flyover Gerezani darisalama si mngeua mtu nyiye. Wodi zimejengwa pale pale kijijini kwao. mbona hamulioni hilo?
Hatuwezi kuua mtu, kwani mmefanya mangapi ya ovyo lakini hakuna kati yenu aliyejeruhiwa? Nimetangulia kusema "Tanzania ni nchi ya amani na utulivu". Hoja yako kwamba wadi zinazojengwa ni za pale pale Bwisya na siyo za Gerezani Dsm haina mashiko! Kwani waliokufa wote ni wakazi wa Bwisya? Kuna waliotokea nje ya Ukerewe na hata nje ya Mkoa wa Mwanza, huko pamejengwa nini?
 
Wasiponielewa Leo watanielewa siku yakiwakuta. Yaani kama nchi tunaanza kushangilia serikali kutumia matatizo yetu kujipatia kipato na sifa binafsi kwa viongozi? Hivi hili lina tofauti gani na baadhi ya NGOs Zinazotumia watanzania wenye matatizo (Mf. UKIMWI) kujipatia fedha na kujinufaisha na fedha hizo huku waathirika wakiambulia kiduchu?
So kwahyo kwa watu 200+ wangepewa pesa zote za rambirambi, na kila mtu aondoke kiroho safi? So gharama zingine zisihusike? Km mtu unajua kuhusu rambirambi vizuri unataka kuniambia kwenye msiba wa kawaida mtaani mchimba kaburi halipwi? Usafiri km mnasafirisha hawalipwi, chakula na vinywaji havinunuliwi mnapewa bure? Coroner kule mochwari mnatoa bure, km hayo yote bure mi sina kwere, ila km mnagharamikia wenye msiba kutoka kwenye rambirambi na michango sasa humu kuna tofauti gani? Ninaomba majibu sahihi yasiyo ya kishabiki!!!
 
Nnai ajuaye?? Hapa kinachoangaliwa ni kwamba; Tusitumie resources zetu kipumbavu. Unampa mtu 50mil na sio mmoja bali wengi tu waende wakazichezee. We waona ni uongozi bora huo?? Serekali imetumia busara zaidi hapo. Je, wangelisema kuwa fesha hiyo ikajenge flyover Gerezani darisalama si mngeua mtu nyiye. Wodi zimejengwa pale pale kijijini kwao. mbona hamulioni hilo?
Watu wanabisha kishabiki sana
 
Serikali ya CCM wameiba tena hela za michango ya maafa. Mtu amepata majanga unamdhulumu. Ukiwa mwanaCCM huendi mbinguni, hata uwe mcha Mungu kiasi gani. Ukishajiambatanisha na shetani, wewe ni wa motoni tu.
Chadema mmeumbuka! Pamoja na kuhamasisha watu wasichangie ila ndo wamewapuuza,shame on you !
 
So kwahyo kwa watu 200+ wangepewa pesa zote za rambirambi, na kila mtu aondoke kiroho safi? So gharama zingine zisihusike? Km mtu unajua kuhusu rambirambi vizuri unataka kuniambia kwenye msiba wa kawaida mtaani mchimba kaburi halipwi? Usafiri km mnasafirisha hawalipwi, chakula na vinywaji havinunuliwi mnapewa bure? Coroner kule mochwari mnatoa bure, km hayo yote bure mi sina kwere, ila km mnagharamikia wenye msiba kutoka kwenye rambirambi na michango sasa humu kuna tofauti gani? Ninaomba majibu sahihi yasiyo ya kishabiki!!!
Katika matumizi hayo ni lipi lisilohusu msiba moja kwa moja? Ni wapi uliona fedha ya rambirambi inatumika kukarabati Mortuary? Si ndimo zinamohifadhiwa maiti?
 
Kwani waliokufa wote ni wakazi wa Bwisya? Kuna waliotokea nje ya Ukerewe na hata nje ya Mkoa wa Mwanza, huko pamejengwa nini?

Wote sio wakazi wa Bwisya ila walikuwa wakielekea huko. Ndo maana hakikujengwa Ukerewe main island. Tunajenga pale kama kumbu kumbu tu ambazo zitadumu kwa muda mrefu. Jamani furahieni fikra nzuri hizi
 
Siwezi kupinga maendeleo ya mahali popote nchini, lakini hii tabia ya kugeuza rambirambi kuwa fedha rasmi ya serikali ni matumizi mabaya ya utu. Hata wewe fikiria nje ya box Mkuu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom