Maajabu ya Mussa na ajali ya Igunga

Maajabu ya Mussa na ajali ya Igunga

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,061
Tunapoendelea kuomboleza na kusikitika na madhila ya ajali ile, kwa upande mwingine napo maaajabu ya Mussa na ajali ya Igunga yanaendelea.

Walitokea kina Mwigulu Nchemba kutaka sheria zikiukwe kwa madereva kukamatwa kwa makosa yasiyokuwa na adhabu hiyo. Sasa kumeibuka wanojiita wadau wanaopendekeza hadi kuwapo na madereva wawili kwenye malori na kuwa ati mtu mmoja anapaswa kuendesha masaa nane tu kwa siku. Kisichofahamika composition ya hawa wanaoitwa wadau ni kina nani hasa na uzoefu au ufahamu kiasi gani kuhusu shughuli za usafirishaji mizigo?

Pamoja na kuwa ajali ya Igunga ilisababishwa na mashimo ambayo TANROADS wamekuwa wakiyatelekeza katika barabara zilizo nyingi hapa nchini labda kwa sababu zao yaonesha bado jitihada za kumtafuta mchawi asiyekuwapo zitaendelea.

Kwa sasa Hatutadanganyika! Inafahamika na ni wazi kuwa ajali ya Igunga chanzo ni mashimo ambayo TANROADS kayatelekeza. Hizi kelele zingine labda kama mnataka kutulazimisha. Hakika kwa mwendo huu wa kujaribu kutafuta sababu za kutengenezesha mtatufikisha hata wale ambao hatukutaka kuambatana na Dada Mange April 26 kufikiria upya.

Please stop Insulting our Intelligence. Tunaowasikiliza tu binadamu danganya toto hizi sasa zinatosha na hazina tena nafasi katika Tanzania ya sasa.

Source: Ajali iliyoua 12 yawakutanisha wadau Tabora
 
TABOA Wameahidi kufanya mgomo nchi nzima hadi serikali ifanye ukarabati wa barabara
 
  • Thanks
Reactions: b20
Mnakumbuka ajali ya Majinja iliyotokea Mkoani Iringa iliyochukua maisha ya Wanachuo kadhaa? Ajali ilikua miongoni mwa ajali mbaya saaana na source ilikua mashimo hayo hayo ya Barabarani
 
  • Thanks
Reactions: b20
Hao Tanroad washenzi barabara hawakagui kipande cha mpaka inapoishia shinyanga kuingia Mwanza sipajui jina anaepajua anisaidie ila ni mpakani kina mashimo kufuru juzi alimanusura nipate ajali ilikua usiku tairi ya nyuma ili burst baada ya kukita shimo nimengi kwa MTU ambae haijui vizuri akapita spidi ni mtihani nashuru haikua ya mbele kwa maana ilikua n upepo mdogo mno...ile lami ni kubandua kabisa sio ya kuziba kama kuna MTU wa tanroad humu plz fuatilia
 
sipati picha Yale ya same mpaka moshi saivi na mvua zilivyonyesha yatakuaje,January tu yalikua ovyo ovyo sana
 
Hao Tanroad washenzi barabara hawakagui kipande cha mpaka inapoishia shinyanga kuingia Mwanza sipajui jina anaepajua anisaidie ila ni mpakani kina mashimo kufuru juzi alimanusura nipate ajali ilikua usiku tairi ya nyuma ili burst baada ya kukita shimo nimengi kwa MTU ambae haijui vizuri akapita spidi ni mtihani nashuru haikua ya mbele kwa maana ilikua n upepo mdogo mno...ile lami ni kubandua kabisa sio ya kuziba kama kuna MTU wa tanroad humu plz fuatilia
Mkuu hapo ni kati ya Nyasamba na Ilula!! Ukimaliza tu ile lami ya Msouth (Grineka) ile ya Mchina ni bure kabisa, kwanza imekuwa ya siku nyingi sana inatakiwa kubanduliwa ni ya mwaka 1996/98 mkuu sasa sijui ni miaka mingapi hiyo?
 
Hao Tanroad washenzi barabara hawakagui kipande cha mpaka inapoishia shinyanga kuingia Mwanza sipajui jina anaepajua anisaidie ila ni mpakani kina mashimo kufuru juzi alimanusura nipate ajali ilikua usiku tairi ya nyuma ili burst baada ya kukita shimo nimengi kwa MTU ambae haijui vizuri akapita spidi ni mtihani nashuru haikua ya mbele kwa maana ilikua n upepo mdogo mno...ile lami ni kubandua kabisa sio ya kuziba kama kuna MTU wa tanroad humu plz fuatilia
Nyasamba hadi Ilula
 
Mnakumbuka ajali ya Majinja iliyotokea Mkoani Iringa iliyochukua maisha ya Wanachuo kadhaa? Ajali ilikua miongoni mwa ajali mbaya saaana na source ilikua mashimo hayo hayo ya Barabarani

Ni jambo jema wakafahamu kuwa ajali kama zilivyotokea za Majinja Express na kuua ndugu zetu hazija sahaulika.

Pana haja ya kuweka rekodi sawa sawa kwa ku upload picha za mashimo barabarani popote kule yalipo.

Tuite Spade kwa jina lake. Hapana haja ya ku fabricate sababu zisizokuwapo hata kama nyie ni serikali na kwa uzembe wenu mmesababisha vifo.
 
Bongo bwana unakuta mtu anajiita mdau wa sekta ya usafirishaji wakati hajawahi hata kumiliki toyota hiace nini lori au bus la yu-tong...

Moja ya tatizo la siku nyingi la Tanzania na watanzania ni kuacha kutumia akili kwenye matatizo ya msingi na hatimaye kupata suluhu baadala yake wanajikita kwenye kupiga ramli kwa kushirikisha watu wasio na ABC ya sekta husika au hata wale wenye uelewa mdogo..

Barabara nyingi za Tanzania zipo chini ya kiwango kiasi cha kuwa mtihani kwa watumiaji, ukosefu wa taa maeneo hatari usiku, sehemu nyingi kutokuwa na chaki nyeupe ya katikati, uzibaji viraka holela, mawimbi sehemu nyingi za barabara, kuwepo kwa kona zisizohitajika, madaraja mengi kukosa au kukaa muda mrefu bila kingo, uwepo wa vichaka sehemu za hatari..uwepo wa magari mabovu barabarani bila mamlaka kuchukua hatua..

Tanroad ni wakati wa kufanya kazi kisasa mkishirikiana na jeshi la polisi, mfunge camera kwenye baadhi ya Barabara kuu, kuwe na road patrol kila mkoa za polisi na tanroad kwenye barabara kuu kila siku mara kwa mara kuangilia kinachojiri barabarani, kila mkoa uwe na breakdown zitakazofanya kazi Barabara kuu, hizi breakdown ziwe na uwezo wa kuvuta malori makubwa yakiwa na mzigo pale yanapopata breakdown sehemu hatari yavutwe na kuwekwa sehemu salama ( mwenye gari lazima alipe hii chaji)..
 
TABOA Wameahidi kufanya mgomo nchi nzima hadi serikali ifanye ukarabati wa barabara

Wakomae wakifanikisha hili litaingia kwenye historia na hakika kesho itakuwa bora kuliko leo na jana.
 
Back
Top Bottom