Ukistaajabu ya musa utaona ya filauni hapa muhas first year ni wa ajabu sana eti wameweka classes kati ya shule zenye majina nchini na kayumba schools. Kwa mfano, discusion groups za wa2 wa mzumbe na marian hawataki wa2 wa shule nyingine na ukiomba discusion utaambiwa kama hujui kingereza sepa mapema. Yan wanajiskia sana wanaona wao ndio vinara wa chuo kwa first year.
Endelezeni mbwembwe tu,mkimaliza chuo ndiyo mtatubu,serikali imeshasema haina fedha za kuwaongezea mishahara.Pia kumbukeni kuwa usome iliboru au migombani shule ya sekondari,ukija kuwa daktari unachezea vidonda vile vile tu.
We waache tu, 2005 nilipoanza 1st yr ilikuwa hivyo, walipofika second year wengine wamepigwa sup za anatomy na biochemistry wenyewe second yr wakaanza kujibalaguza hasa mademu haka tukaanza kujipigia kama tunalia vile. We acha tu hawajapigika hawa.
Hao hawajaijua vizuri medical school...
Ngoja kwanza wakutane na gross anatomy ambayo ni nyepesi wakaribishwe kabla ya kuanza mambo magumu. Wakikutana na majina kama "musculus levator labii superioris alaeque nasi" ndipo watajua kuwa kuna zaidi ya kiingereza huko
Hao wangeenda SUA kusoma veterinary medicine miaka kama 10-15 iliyopita na attitude hiyo ninaamini christmas ingekuta wameshahamia chuo kingine bila kufukuzwa. Ngoja tuwasubirie hapo MUHAS tuone itakuwaje
Aanze tu kuirudia rudia,hususan General Chemistry,Inorganic Chemistry na Organic Chemistry...hili ndio huwa tatizo kubwa kwa inservices na mwalimu hakubali excuse yoyote