Ila hii dunia hakuna watu wajinga kama sisi Waafrika! Ukute liganga limewadanganya na wenyewe wanaenda kubeba, wasipofanikiwa linaenda tena kuwandanganya eti utakuwa ulikosea masharti! Hakuna watu waongo kama waganga wa kienyeji! Zamani kabla sijafahamu mambo ya dini nikajidai kumfuata rafiki yangu kwenda kwa mganga bwana, wanachofanya hawa jamaa huyo atakayekupeleka anaanza kwanza anapeleka taarifa zako zote kwa mganga. Sasa ukifika jamaa anaanza kupita mlemle ulimomhadithia huyo rafiki yako! Pumbavu kabisa!