Maajabu mbalimbali duniani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maajabu mbalimbali duniani!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 7, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Sunday, July 05, 2009 11:43 PM
  Mwanaume mmoja nchini China ambaye alizaliwa akiwa na uume mwingine wa ziada ameukata uume wake mmoja baada ya mpenzi wake kumwambia achague moja, aukate uume wake mmoja wa huo wa ziada au wavunje uhusiano wao. Ang Qiang mkazi wa mji wa Guangzhou nchini China alizaliwa akiwa na uume mmoja wa ziada lakini baada ya mpenzi wake kuchukizwa na hali yake hiyo na kutishia kumkimbia, Qiang aliamua kuukata uume mmoja.

  "Wakati tulipoanza uhusiano wetu, mpenzi wangu alishtushwa na hali yangu lakini baada ya muda alianza kuogopa" alisema Qiang.

  Mpenzi wake alimwambia kuwa aidha aukate uume wake mmoja wa ziada au itabidi wauvunje uhusiano wao kwani hawezi kuendelea naye akiwa katika hali hiyo.

  Qiang mwenye umri wa miaka 23 aliamua kuukata uume wake wa ziada ili kulinda mapenzi yake na mpenzi wake.

  Qiang anaamini kuwa kwa kuuondoa uume wa ziada aliokuwa nao atakuwa amemridhisha mpenzi wake na mapenzi yao yataendelea vizuri kama awali.

  Hali aliyo nayo Qiang inajulikana kitaalamu kama "Diphallus" na humtokea mwanaume mmoja kati ya wanaume milioni 5.5.

  Nchini Italia mfanyabiashara mmoja marufu wa nchini humo ambaye naye alizaliwa akiwa katika hali kama hiyo na yeye aliukata uume wake wa ziada.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2403254&&Cat=7
   
  Last edited by a moderator: Jul 7, 2009
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  MAHAKAMA ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara imemhukumu mwalimu wa Shule ya Sekondari Basstu aitwae Renatus Massy [29] kifungo cha maisha jela kwa kupatikana na kosa la kulawiti mtoto wa miaka nane. Mahakama hiyo ilimhukumu mwalimu huyo kwa kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na bila kuwa na shaka na ushahidi huo.

  Katika kesi hiyo upande wa mashitaka ulikuwa ukiongozwa na mwendesha mashitaka, Athumani Mkilindi huku ikisikilizwa na kutolewa hukumu na Hakimu Joseph Kimaro wa Mahakama hiyo.

  Hakimu Kimaro kabla ya kutoa hukumu hiyo alimtaka mshitakiwa kujitetea ili asipewe adhabu kali na mshitakiwa alijitetea kuwa: “Naomba nipunguziwe adhabu kwa kuwa hili ni kosa langu la kwanza na nina familia kubwa inayonitegemea hakimu naomba nipewe adhabu ndogo sitarudia tena” alijitetea hivyo mwalimu huyo mbele ya hakimu Kimaro.

  Hakimu Kimaro hakuridhika na utetezi wake na kumuamuru akatumikie adhabu ya kifungo hicho cha maisha ili iwe fundisho kwa wengine wenye tamaa za kijinga kama zake.

  Awali ilidaiwa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Mei 25, mwaka jana, majira ya saa 10 jioni, nyumbani kwa shangazi yake mshitakiwa alikokwenda huko Wilayani Hanang.

  Ilidaiwa kuwa mshitakiwa alipokwenda hapo alimkuta mtoto huyo [jina kapuni] akicheza na wenzake nje ya nyumba hiyo na kumchukua kuingia nae chumbani na kumbana pumzi na kuanza kumlawiti bila hata chembe ya huruma.

  Baada ya kutimiza azma yake hiyo mshitakiwa alikimbia na kumuacha mtoto huyo akipiga kelele kali na watu kukimbilia na kumkuta amefanyiwa kitendo hicho cha kinyama.

  Mtoto huyo alikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu na mshitakiwa alikamatwa siku hiyo hiyo akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2426390&&Cat=1
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Ria akiwa na wanyama wake jikoni Sunday, June 28, 2009 8:37 AM
  Mwanamke mmoja wa Afrika Kusini anawashangaza watu wengi kwa jinsi anavyolala kitanda kimoja na kukaa nyumba moja na wanyama hatari 11 wakiwemo simba watano, chui wawili na duma wanne. Picha za mwanamke huyo na wanyama wake mwisho wa habari hii. Wakati watu wengi wakiogopa hata kuwasogelea wanyama hao hatari, hali ni tofauti kwa Riana Van Nieuwenhuizen wa nchini Afrika Kusini ambaye yeye hudiriki hata kulala kitanda kimoja na wanyama hao hatari.

  Riana mwenye umri wa miaka 46 akiwaongelea wanyama wake hao anaowafuga ndani ya nyumba yake alisema "Nawapenda sana wote".

  Riana alianza maisha yake na wanyama hao hatari kwa kumnunua duma mmoja mwaka 2006 baada ya kugundua kwamba wanyama hao ni miongoni mwa wanyama ambao kizazi chao kinaelekea kupotea kukiwa na duma 1000 tu barani afrika.

  Riana aliacha kazi yake ya miaka 22 kwenye kitengo cha wizara ya sheria na kufanya kazi kwa muda kwenye zoo ili aweze kumkuza duma wake.

  Riana alitimiza ndoto yake ya kuwaokoa duma baada ya muda mfupi kwa kuanzisha mfuko wa hisani wa kutunza kizazi cha duma Afrika aliouita Fiela Funds Cheetah Breeding Project.

  Wanyama wake hao wamekuwa wakiranda randa ndani ya nyumba yake kuanzia jikoni mpaka chumbani kitandani.

  Pamoja na wanyama hao wakubwa Riana pia anafuga pia mbwa wawili na paka.

  "Hufanya kitu chochote kukujulisha kuwa wana njaa, Wakati mwingine huruka ruka kwenye sakafu kukujulisha kuwa wana njaa" alisema Riana.

  Riana ameelezea kufurahia maisha yake hadi sasa na wanyama hao ambao wakiwa porini huwa nyama hazikatizi wakaziachia. GONGA HAPA KWA PICHA ZA MWANAMKE HUYO NA WANYAMA http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2353126&&Cat=7WAKE
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2353126&&Cat=7

   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mgonjwa wa Uingereza akihitimisha maisha yake katika kliniki ya Diginitas ya Uswizi Monday, June 01, 2009 12:57 PM
  Takribani waingereza 800 ambao wamechoka maisha waliyo nayo kutokana na kusumbuliwa na magonjwa mbali mbali wamejiunga kwenye foleni ya kusubiria kifo katika kliniki ya Diginitas ya nchini Uswizi. Taarifa za magazeti ya Uingereza zilisema kwamba waingereza 800 ambao wanasumbuliwa na magonjwa mbali mbali ambayo hayana tiba ambao wanataka wafariki muda wowote baada ya kuchoka maisha waliyonayo wamejiorodhesha kwenye foleni ya kusaidiwa kujiua kwenye kliniki ya Diginitas iliyopo nchini Uswizi.

  Uswizi ndio nchi pekee ya ulaya ambayo inaruhusu watu kusaidiwa kujiua pale wanapoona magonjwa yao ambayo hayana tiba yanawatesa kwa muda mrefu.

  Kliniki ya Diginitas huwasaidia watu wanaotaka kujiua kwa kuwapa dozi kubwa za madawa ambazo husimamisha mapigo yao ya moyo na kuwaua taratibu wakiwa wamelala.

  Watu wengi ambao hujiua kwenye kliniki hiyo ni wale ambao wanasumbuliwa na magonjwa yasiyotibika kama vile kansa na mengineyo ambayo huwa yamefikia hatua za mwisho mwisho.

  Ni kosa la jinai kumsaidia mtu kujiua nchini Uingereza.

  Mtu anayemsaidia mgonjwa ambaye hajiwezi na hawezi kwenda mwenyewe kutoka Uingereza hadi Uswizi bila ya msaada wa mtu mwingine huingia kwenye fungu la watu wanaosaidia watu kujiua na hukabiliwa na kifungo cha miaka mingi jela.

  Waingereza 34 ambao foleni yao imefika wako tayari kuelekea nchini Uswizi kwenye kliniki hiyo kuhitimisha maisha yao.

  Idadi ya waingereza ambao wamejioredhesha kwenye foleni ya kusaidiwa kujiua kwenye kliniki hiyo kuanzia mwaka 2002 hadi sasa imeongezeka mara kumi zaidi.

  Katika miezi 12 iliyopita Waingereza 23 walihitimisha maisha yao katika kliniki hiyo. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2137190&&Cat=7
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Thursday, June 18, 2009 6:59 PM
  Mwanamke mmoja wa nchini Israel ametia fora kwa kuzaa watoto 18 ndani ya miaka 21 ya ndoa yake na mumewe. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 40 na ushee alijifungua mtoto wake wa 18 jana.

  Pamoja na kuwa na watoto 18 mwanamke huyo na mumewe bado hawajaridhika tu na idadi ya watoto walionao na walielezea mpango wao wa kuzaa mtoto wa 19, vyombo vya habari vya Israel vimeripoti.

  Wanandoa hao wana watoto 12 wa kiume na watoto sita wa kike. Mtoto wao wa mwisho ndiye huyo aliyezaliwa jana ikiwa ni wiki moja tu baada ya mtoto wao wa kwanza kusherehekea kutimiza miaka 21.

  "Siwezi kusema jinsi ninavyojisikia kuwa na watoto wengi lakini kila mtoto amekuja na baraka zake" alisema mwanamke huyo.

  Mwanamke huyo alisema kwamba kwa jinsi alivyoenda kujifungua mara nyingi kwenye hospitali ya Kaplan iliyoko kwenye mji wa Rehovot, manesi wote wa hospitali hiyo wamemzoea sana.

  "Tumezoeana sana kiasi cha kwamba utadhani na mimi nafanya kazi hospitali hiyo" alisema mwanamke huyo.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2276970&&Cat=7
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Thursday, May 07, 2009 1:52 PM
  Mtoto mmoja nchini Urusi amewashangaza wazazi na madaktari baada ya kuanza kuzungumza dakika chache baada ya kuzaliwa. Kwa mujibu wa tovuti za nchini Urusi, mtoto huyo alianza kusema neno lake la kwanza punde baada ya kuzaliwa kwa kutamka kifasaha kwa kumuita baba yake "Baba!".

  Na katika dakika chache baadae mtoto huyo aliyepewa jina la Stephan alitamka "Mama!".

  Miujiza ya mtoto huyo haikuishia hapo kwani siku iliyofuatia wakati mama wa mtoto huyo alipomwambia mtoto huyo "Baba yako anakuja hospitali" kwa mshangao mtoto huyo alijibu "Nani?, Baba?".

  Mama wa mtoto huyo Lisa Bazheyeva, mwenye umri wa miaka 17 na baba wa mtoto wake Rodion Bejeev wanaishi katika jiji la Norilsk nchini humo.

  Madaktari waliomsaidia mama huyo wakati wa kujifungua wamethibitisha taarifa za kuongea kwa mtoto huyo.

  "Nilisikia kwa masikio yangu mtoto huyo akiongea punde tu baada ya kuzaliwa" alisema Dokta Marina Panova, na kuongeza "Sijawahi kuona kitu kama hiki katika miaka yangu 23 ya kufanya katika kliniki ya uzazi". http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=1940534&&Cat=7
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Martin Jones alivyo sasa. Saturday, July 04, 2009 6:47 AM
  Mwanaume mmoja kipofu wa nchini Uingereza ameweza kumuona mkewe kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa upasuaji wa macho ambapo jino lake la juu lilipandikizwa kwenye jicho lake. Mjenzi Martin Jones, 42, alipata upofu wa macho yake yote mawili zaidi ya miaka 10 iliyopita baada ya bomba la madini ya aluminium yaliyokuwa yamechemka kumpasukia usoni, liliripoti gazeti la Daily Mail la Uingereza.

  Lakini sasa baada ya kufanyiwa upasuaji wa macho wa aina yake ambapo jino lake lilipandikizwa kwenye jicho lake la kulia, ameweza kuona kwa mara ya kwanza baada miaka mingi sana ya upofu.

  Upasuji kama huu umefanyika mara 50 tu nchini Uingereza.

  Upasuaji huo wa macho umemwezesha Jones aweze kumuona kwa mara ya kwanza mkewe Gill ambaye alimuoa miaka minne iliyopita wakati akiwa tayari ni kipofu.

  "Madaktari waliitoa bandeji kwenye jicho langu na mara nikaanza kuona kitu mbele yangu na nilipoangalia vizuri alikuwa ni yeye mke wangu".

  "Ni mrembo sana , sikuwahi kumuona awali, ilikuwa ni miujiza kumuona kwa mara ya kwanza" alisema Martin.

  "Wakati nilipoona kuna uwezekano wa kuona kwa mara nyingine, mtu wa kwanza niliyetaka kumuona alikuwa ni mke wangu".

  Opereshereni hiyo ya masaa manane iligunduliwa na daktari mwenye makazi yake nchini Uingereza, Dr Christopher Liu.

  Upasuaji ulifanyika kwa kuchukua jino lake moja la juu la mbele kwa pembeni na jino hilo lilitengenezwa katika umbile ambalo liliweza kuwa kama nyumba ya lenzi moja ndogo iliyotengenezwa maalumu.

  Jino lake lilitumika kwa kuwa mwili wa binadamu mara nyingi hukataa kuendana na plastiki, alisema Dr Liu.

  Kipande cha ngozi yake kilichukuliwa kutoka kwenye ngozi ya mashavu yake na kupandikizwa kwenye jicho lake kwa muda wa takribani miezi miwili na kiliweza kupata uwezo wa kujisambazia damu chenyewe.

  Baadae kipande hicho kilitolewa na kuwekwa juu ya jino lake ambalo liliwekwa lenzi na kupandikizwa ndani ya jicho lake na kitobo kidogo kilitobolewa kwenye ngozi hiyo iliyowekwa juu ya jino ili kuwezesha mwanga kuingia na kumwezesha Martin kuona tena.

  Madaktari walisema kwamba upasuaji kama huu hufanyika kwa watu wenye upofu uliosababishwa na kuharibika kwa cornea na ambao macho yao hayawezi kufanyiwa upasuaji wa aina zingine wa upandikizaji wa cornea.

  [ Cornea ni eneo la juu la jicho ambalo linazunguka iris, pupil na anterior chamber. ]

  Martin hakufanyiwa upasuaji kama huu kwenye jicho lake la kushoto kwakuwa jicho hilo lilikuwa limeharibika sana na ilibidi litolewe.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2402290&&Cat=7
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wanaume nao Kutumia Sindano za Kupangilia Uzazi Tuesday, May 12, 2009 9:05 AM
  Baada ya wanawake kwa miaka mingi kuwa ndio wenye jukumu la kutumia vidonge na njia nyingine katika kupangilia uzazi, watafiti nchini China wamekamilisha utafiti wao ambao utawasaidia wanaume kuwasaidia wanawake jukumu hilo baada ya kutoa sindano kwaajili ya wanaume zitakazosimamisha uzalishaji wa mbegu za kiume kwa muda Wanasayansi nchini China wamekamilisha utafiti wao wa sindano kwaajili ya wanaume ili kusaidia kuzuia mimba zisizohitajika.

  Sindano hizo zinasimamisha kwa muda uzalishaji wa mbegu za kiume na watafiti hao walisema kwamba uzalishaji wa mbegu za kiume unaweza ukaendelezwa muda wowote ule.

  Watafiti hao waliwatoa wasiwasi wanaume kwa kusema kuwa hakuna madhara yoyote yanayotokana na matumizi ya sindano hizo.

  Kwa miaka mingi wanawake wamekuwa wakitumia vidonge na njia nyingine mbali mbali za kuzuia mimba zisizohitajika huku wanaume wakibakia na chaguo moja tu ambalo ni matumizi ya kondomu au kufunga kizazi kabisa kwa njia ya vasektomi.

  Wanaume 1,000 wa nchini China wenye umri kati ya miaka 20 na 45 ambao kila mmoja wao alikuwa tayari ana mtoto mmoja au zaidi walishirikishwa kwenye majaribio ya sindano hizo kwa kuchomwa sindano hizo kila mwezi kwa muda wa miezi 30 mfululizo.

  Majaribio hayo yalionyesha mafanikio makubwa kwani katika watu 1,000 ni mtu mmoja tu ndiye aliyefanikiwa kumpa ujauzito mpenzi wake wakati akiendelea na sindano hizo.

  Mwisho wa utafiti huo, mfumo za uzazi wa wanaume wote walioshiriki kwenye utafiti huo ulirudi katika hali yake ya kawaida isipokuwa wanaume wawili tu.

  Wanasayansi wamesema watautumia utaalamu uliotumika kujaribu kutengeneza vidonge vitakavyotumiwa na wanaume kusaidia kuzuia mimba zisizohitajika.

  Hata hivyo wanasayansi hao walikumbusha kwamba matumizi ya sindano hizo hayamaanishi kwamba ndiyo yatakuwa kinga ya magonjwa ya zinaa.

  "Tunawahimiza watu watumie kondomu ili kujikinga na magonjwa ya zinaa" walisema watafiti hao.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=1972346&&Cat=7
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Michelle na mumewe Sean Agnew wakiwa na mtoto wao Maggie Thursday, May 07, 2009 1:26 AM
  Familia moja nchini Marekani inahaha kutafuta tiba ya ugonjwa usiojulikana ambao umemfanya mtoto wao wa miezi 10 kuzidi kuwa mdogo badala ya kukua. VIDEO ya mtoto huyo mwisho wa habari hii. Michelle na mumewe Sean Agnew wakazi wa Utah nchini Marekani wanahaha kutafuta tiba ambayo hadi leo haijapatikana ya mtoto wao Maggie ambaye badala ya kukua kama watoto wengine amezidi kudhoofika na kuwa mdogo.

  Maggie mwenye umri wa miezi 10 hivi sasa anazidi kuwa mdogo kwani misuli kwenye mwili yake inayeyuka na kumwacha na nyama zinazoning'inia, anapoteza kilo kila siku pamoja na kulishwa chakula kingi sana.

  Hadi sasa madaktari hawajajua nini kinamsumbua mtoto huyo kwani uzito wake umezidi kupungua na misuli kwenye mwili wake imezidi kunywea pamoja na kwamba madaktari waliamua walimshe kwa kutumia mipira iliyounganishwa kwenye tumbo lake ambayo husukuma kalori nyingi kuliko kawaida.

  "Anapata kalori nyingi sana kutoka kwenye chakula anacholishwa lakini mwili wake hutumia kalori zote katika muda mfupi , hali ambayo imetufanya tusielewe chakula anacholishwa huwa kinaenda wapi" alisema baba wa mtoto huyo.

  Vipimo vya magonjwa yote ambayo madaktari walihisi yanaweza yakawa ndio chanzo cha hali hiyo yamefanyika lakini vipimo vyote havijathibitisha ugonjwa wowote ule.


  VIDEO yake bonyeza hapa http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=1932822&&Cat=7
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Hajnal Ban alivyo sasa Monday, May 04, 2009 9:47 PM
  'Mungu ameniumba mfupi, Madaktari wamenitengeneza nimekuwa mrefu' hivyo ndivyo anavyosema mwanasiasa mmoja mwanamke wa nchini Australia ambaye ili awe mrefu alisafiri hadi nchini Urusi na miguu yake kuvunjwa vipande vinne na kurefushwa kwa sentimeta nane Baada ya miezi tisa ya maumivu makali ya hatua za kurefusha miguu yake, Hajnal Ban, 31, diwani wa halmashauri ya jiji la Queensland, alifanikiwa kuwa na urefu wa futi 5 na inchi 4.

  "Wanawake wengi huwa hawajiamini kutokana na unene wao, matiti au pua zao, mimi nilikuwa sijiamini kwa urefu wangu" alisema diwani huyo.

  Hajnal alikuwa akitaniwa na wenzake wakati wa utoto wake kutokana na ufupi wake, hali hiyo ilimfanya ajifikirie kwamba kutokana na ufupi wake watu hawatampa uzito wowote wakati alipoanza kazi ya uanasheria na baadae kuhamia kwenye siasa.

  Hajnal alisafiri hadi Urusi na kutumia dola 25,000 za kimarekani kuwalipa madaktari wa mifupa waivunje miguu yake yote miwili katika vipande vinne ili kuviongeza urefu vipande hivyo.

  Madaktari wake waliingiza vipande vya vyuma kwenye miguu yake vilivyoitanua mifupa yake kwa milimita moja kila siku katika kipindi cha maumivu makali cha miezi tisa.

  Hajnal alirudi nchini Australia miguu yake ikiwa imerefuka kwa sentimeta nane na kutunga kitabu alichokiita "Mungu ameniumba mfupi, Madaktari wamenitengeneza nimekuwa mrefu".

  Hajnal alitoa kitabu hicho kwa kutumia jina bandia akijiita Sara Vornamen baada ya kumalizika kwa operesheni yake hiyo iliyofanyika miaka minane iliyopita.

  Kitabu chake hicho kilikuwa miongoni mwa vitabu vilivyouza sana wakati huo, lakini Hajnal alitoboa siri ya uandishi wa kitabu hicho wiki iliyopita.

  "Kutoka wakati nilipopanda ndege kwenda Urusi hadi wakati nilipoweza tena kuvaa viatu vya kuchuchumia ilikuwa ni karibia mwaka mzima, lakini katika kipindi cha miezi tisa nilikuwa katika maumivu makali sana" alisema diwani Hajnal.

  Hajnal alisema kwamba anataka watu wamchukulie kwa umakini na kumkumbuka kwa kazi zake nzuri kwa jamii badala ya kumkumbuka kwa kusema "Unamjua yule mwanamke aliyeongeza urefu wa miguu yake".

  "Sijutii kabisa uamuzi nilioufanya, ulikuwa ni uamuzi niliofikia baada ya kushauriana na familia yangu na baada ya kufanya utafiti"

  "Nina bahati sana kwakuwa matokeo ya uamuzi wangu yalikuwa yakufurahisha. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=1910650&&Cat=7
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Jengo la Hospitali ya Royal Derby Sunday, February 01, 2009 7:51 AM
  Wafanyakazi katika hospitali mpya ya kisasa katika mji wa Derby nchini Uingereza wamelalamikia kutishika kutokana na majini na mizuka inayofanya vitu vya ajabu ajabu katika hospitali hiyo. Wafanyakazi katika hospitali hiyo wamekuwa wakilalamika kuona vitu vya ajabu ajabu katika korido za hospitali ya Royal Derby ambayo ujenzi wake umegharimu mamilioni ya pound.

  Mmoja wa wafanyakazi hao alisema "Mzuka wa Mwanaume aliyevaa nguo nyeusi unachomoza na kupotea kutoka katika kuta za korido za hospitali hiyo" alisema mfanyakazi huyo na kuongeza kuwa mizuka hiyo inatokeza kwa wingi karibu na chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.

  Kutokana na hali hiyo inasemekana mchungaji mmoja ameombwa aende kwenye hospitali hiyo akafanye sala za kufukuza majini hayo.

  Uongozi wa hospitali hiyo ulisema kuwa unayachukulia malalamiko ya wafanyakazi hao kwa uangalifu zaidi na kusema haina mpango wa kufanya kafara au maombi katika hospitali hiyo.

  Mchungaji Canon Elaine Jones wa Derby amekiri kuombwa kwenda kufanya maombi ya kufukuza majini yanayozunguka katika hospitali hiyo.

  Mji wa Derby inasemekana unaongoza kwa kuwa na mizuka na majini wengi kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtafiti wa masuala hayo Lionel Fanthorpe.

  Utafiti huo ulionyesha kuwepo kwa majini na mizuka 315 katika mji huo.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=964966&&Cat=7
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ili aweze kumfurahisha mkewe Carla kitandani anachukua masomo maalumu ya mapenzi toka mwalimu mmoja wa kike. Ili kuongeza nguvu zake za kiume Sarkozy anaingia mara kadhaa kwa wiki kupata somo la mwalimu Julie Imperiali anayempa mazoezi ya kuongeza nguvu za kiume ambapo hulipa euro 160 kwa lisaa limoja.

  Akibainisha mwalimu huyo alisema "Kuwa na misuli yenye nguvu kunaongeza ufanisi katika mapenzi", "Kufika kileleni mapema kwa wanaume kunatokana na upungufu wa nguvu katika misuli ya maeneo ya siri" alisema Imperiali.

  Ili kuongeza nguvu za mapenzi za rais huyo Imperial hubaki na rais huyo mwenye umri wa miaka 53 akimpa mazoezi mbali mbali katika masomo yake.

  Katika miezi 10 iliyopita iliyopita Julie Imperiali, mcheza dansi na mwongoza mazoezi wa zamani amemsaidia rais Sarkozy kupunguza kilo 4 na kupungua saizi mbili za suruali.

  "Ili kuihisi misuli yako ya maeneo ya siri fikiria kwamba unahitaji kukojoa na wewe unajizuia kukojoa, hii ni kwa wanawake na kwa wanaume pia". alisema Imperali.

  Bi Imperiali anawachaji wateja wake kati ya euro 110 na euro 180 kwa saa.

  Miongoni mwa wateja wake ni wafanyabiashara wakubwa, wanasheria na watoto wa wafalme wa Saudi Arabia na Qatar.

  Sarkozy alipelekwa na mkewe Clara kwa mtaalamu huyo.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=879170&&Cat=7
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wednesday, June 24, 2009 8:31 AM
  Hatimaye habari nzuri kwa watu wanene, Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Japan kwa watu 50,000 kwa jumla ya miaka 12 umeonyesha kuwa watu wanene wanaishi miaka sita zaidi ya watu wembamba. Wakati watu wanene kila siku wamekuwa wakifanya kila wawezalo ili kupunguza uzito wao, utafiti uliofanywa na timu ya wizara ya afya ya Japan iliyoongozwa na Profesa Shinichi Kuriyama wa chuo kikuu cha Tohoku umeonyesha kuwa watu wanene huishi miaka mingi kulinganisha na watu wembamba.

  Utafiti huo ulifanywa kwenye mji wa Miyagi uliopo kaskazini mwa Japan ukiwashirikisha watu 50,000 wenye umri wa miaka kati ya 40 na 79.

  Matokeo ya utafiti huo yalionyesha kuwa watu wembamba huishi miaka sita pungufu ya watu wanene.

  Utafiti huo uliofanyika kwa jumla ya miaka 12 uliwashirikisha wanawake kwa wanaume wenye umri zaidi ya miaka 40.

  Utafiti huo ulifanyika kwa kuangalia vielelezo vya unene na urefu wa mtu (BMI) ambapo kipimo chake kuwa katika mfumo wa kilo kg/m2.

  Utafiti huo ulionyesha kuwa watu wenye unene wa wastani (BMI kati ya 18.5 na 25) wenye umri zaidi ya miaka 40 huishi miaka miwili pungufu ya watu wanene kidogo (BMI kati ya 25-30) wakati watu wembamba sana (BMI chini ya 18) huishi miaka sita pungufu ya watu wanene sana (BMI zaidi ya 30).

  Sababu iliyochangia watu wembamba kuwa na maisha mafupi kulinganisha na watu wanene ilisemekana kuwa ni kutokana na kwamba watu wengi wembamba hupenda kuvuta sigara na pia kutokana na kwamba watu wembamba miili yao huwa dhaifu katika kupambana na maradhi sugu.

  Hata hivyo Profesa Kuriyama alishauri watu waendelee kula vizuri na wasibweteke na kujiachia kuwa wanene, badala yake wajitahidi kuwa katika uzito wa wastani unaopendekezwa na mashirika ya afya duniani.

  Utafiti huo ulionyesha pia kuwa jinsi mtu anavyozidi kuwa mnene ndivyo gharama za matibabu yake zinavyozidi kuongezeka.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2319386&&Cat=7
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Jyoti katikati akiwa amesimama na marafiki zake. Thursday, June 18, 2009 5:22 AM
  Jyoti Amge wa nchini India ndiye msichana mfupi kuliko wote duniani pamoja na kuwa na umri wa miaka 15 ana urefu wa sentimeta 38 tu na tangia amezaliwa ameongezeka kilo nne tu na kutokana na ufupi wake hata mtoto wa mwaka mmoja anaonekana mkubwa zaidi yake. Picha zake zaidi mwisho wa habari hii. Jyoti Amge ndiye msichana mfupi kuliko wote duniani pamoja na kuwa na umri wa miaka 15 ana urefu wa sentimeta 38 tu.

  Pamoja na umri huo aliokuwa nao sasa Jyoti ameongezeka kilo 4 tu tangia alipozaliwa. Hivi sasa Jyoti ana uzito wa kilo 5.4 tu.

  Umbile lake ni dogo sana kiasi cha kwamba ndugu yake mwenye umri wa mwaka mmoja na mwezi mmoja anaonekana mkubwa zaidi yake.

  Madaktari wanasema kwamba hali ya Jyoti inatokana na ugonjwa ambao umesababisha mwili wake kushindwa kutoa homoni za ukuaji.

  Wataalamu mbali mbali waliomfanyia uchunguzi wa hali yake wamedai kwamba Jyoti hatarefuka zaidi ya hapo na atabakia na urefu aliokua nao sasa katika maisha yake yote.

  Jyoti kama wasichana wengine wa umri wake anasoma shule ya msingi na kutokana na ufupi wake ametengenezewa kidawati chake "kiduchu" maalumu kwa ajili yake ambacho kimewekwa katikati ya darasa ili kumwezesha kuona vizuri ubaoni.

  Jyoti huenda shule kwa kupewa kampani na marafiki zake ambao wamejitolea kumbeba kama mtoto mdogo. Wakati rafiki yake mmoja akijitolea kumbeba, rafiki yake mwingine hulibeba begi lake la shule ambalo humfikia Jyoti kiunoni kwa urefu.

  Ufupi wake pia unampa tabu hadi wakati wa kujisomea kwani peni na madaftari yake yanaonekana ni makubwa sana kwake.

  "Nilipokuwa na miaka mitatu nilijiona nina tofauti na watoto wengine kwani wenzangu wote niliwaona ni wakubwa sana kuliko mimi" alisema Jyoti.

  "Mimi ni mtu wa kawaida kama nyinyi, nakula kama nyinyi, naota kama nyinyi na sijihisi tofauti yoyote na watu wengine" alisema Jyoti.

  Jyoti ana ndoto ya kuwa msanii wa filamu nchini India na ndoto yake imeonyesha mwanga kidogo baada ya kushirikishwa kwenye video ya muziki ya mwimbaji mmoja maarufu nchini humo.
  picha zaidi bonyeza hapa http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2270222&&Cat=7
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wednesday, June 17, 2009 10:47 AM
  Takribani wanaume 400 wa Korea Kusini wanapigana vikumbo kujaribu bahati yao ya kumuoa mwanamke milionea wa nchini humo ambaye ametangaza kutafuta mume kwenye internet. Wanaume 394 kuanzia wanajeshi, madaktari, wanasheria, wahasibu mpaka wafanyakazi wa ngazi za juu serikalini wamejaribu bahati yao ya kumuoa mwanamke milionea wa Korea Kusini ambaye ana utajiri wa dola milioni 22 na amechoshwa na maisha ya upweke na hivi sasa anatafuta mume mtarajiwa kwenye internet.

  Kampuni ya kuwatafutia watu wachumba ambayo mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 49 ameitumia, ilisema kwamba katika wanaume wote waliojitokeza ni wanaume wanane tu kati yao watakaoingia fainali kumpa nafasi milionea huyo kumchagua ampendae.

  Tangazo la mwanamke huyo kutafuta mume mtarajiwa liliwekwa kwenye tovuti ya kampuni hiyo tangia mei 20 mwaka huu.

  "Akiwa kama mfanyabiashara ambaye yuko bize sana, ilikuwa ni sana vigumu kwake kutafuta mume kwa wakati wake mwenyewe" alisema msemaji wa kampuni hiyo.

  "Tulikuwa tumepanga tangazo hilo likae kwenye internet hadi mwishoni mwa mwezi lakini kutokana na vyombo vya habari kuonyesha kuvutiwa sana na tangazo hilo, hajafurahia hali hiyo na ametaka tangazo hilo lifikie tamati jumanne".

  Mwanamke huyo ameishachagua wanaume wanane kati yao kwaajili ya kuwafanyia mahojiano na anatajiwa kuwachagua wanaume watatu tu kati yao na baadae atatumia mwezi mmoja na kila mwanaume mmoja kati ya hao watatu kabla ya kumtangaza atakayemchagua awe mume wake.

  "Anatafuta mwanaume atakayekuwa na mapenzi ya kweli ambaye atakuwa tayari kupanda na kushuka milima ya vikwazo katika maisha" alisema msemaji wa kampuni hiyo.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2267330&&Cat=7
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Tuesday, June 09, 2009 7:57 AM
  Mfungwa wa zamani katika jela moja nchini Marekani amempandisha kizimbani nesi wa jela aliyokuwa amefungwa akidai kwamba nesi huyo alimpa dawa ambazo zilimsababishia mateso makubwa kwa kusababisha uume wake usimame kwa masaa 55 mfululizo. Dawud Yaduallah alimfungulia mashtaka nesi Judith Lovelace kwa kumpa dawa ambazo zilimsababishia aishi kwa mateso makubwa kutokana na dawa hizo kusababisha uume wake kusimama kwa masaa 55 mfululizo.

  Yaduallah, 43, alisema kwamba ilimbidi asubiri zaidi ya siku mbili kabla ya kutolewa kwenye jela hiyo iliyopo New York na kupelekwa hospitali, liliripoti gazeti la New York Post la Marekani.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, Yaduallah alisema kuwa dozi yake ya dawa za kutuliza akili na kupunguza mawazo na stress ilizidishwa kwa asilimia 25 na matokeo yake kumfanya abaki na maumivu makali kutokana na uume wake kusimama muda wote kwa zaidi ya siku mbili.

  "Dawa hizo zilimsababishia madhara makubwa kama vile uume wake kutosimama vizuri hivi sasa na kusababisha mapungufu katika uwezo wake wa kujamiiana na kuhisi maumivu wakati wa kujamiiana" nyaraka za mahakama zilinukuliwa na vyombo vya habari.

  Yaduallah pia alilamika kuwa dawa hizo zimemsababishia ndoa yake iwe kwenye mashaka makubwa ya kuvunjika.

  Yaduallah pia alimlaumu nesi Lovelace kwa kutompatia matibabu yoyote ya kumpunguzia maumivu zaidi ya kumwambia aweke barafu kwenye uume wake.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2196958&&Cat=7
   
 17. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Tumeingiliwa? WTF?
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mshale unapozama jichoni [​IMG] Mwanafunzi wa miaka 11 nchini China amenusurika kufa baada ya mshale uliorushwa na rafiki yake kuzama kichwani kwake kupitia kwenye jicho lake, aliwahishwa hospitali huku mshale huo ukiwa bado umezama kwenye kichwa chake
  Posted by: majid

  http://www.nifahamishe.com/gallery_photos.aspx?TagId=1&&P_Sec=1
   
 19. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Zawadi ya Bethidei - 'Muuweni Mke Wangu'[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]
  [​IMG]
  Jorge Victorino-Vazquez[/TD]
  [TD]Sunday, April 29, 2012 7:14 PM
  Mwanaume mmoja wa nchini Marekani amejikuta akiingia matatani baada ya kumkodisha mtu amuue mkewe ili iwe ndio zawadi yake ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]mbaroni na polisi na kufunguliwa mashtaka ya kula njama ya kuua mtu baada ya kumkodisha mtu amuue mkewe.

  Jorge aliingia matatani baada ya bila kujua kumkodisha mwanaume amuue mkewe kumbe mwanaume huyo alikuwa ni askari kanzu.

  Jorge alipanga siku ya jumatatu iwe ndio siku ya kuuliwa kwa mkewe ili iwe ndio zawadi yake bora ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake.

  Jorge alimlipa askari kanzu huyo dola 2000 ili ajifanye amevamia nyumba yao usiku, amshushie kipigo Jorge ili na yeye aonekane ameshambuliwa, aibe baadhi ya vitu na kisha amuue mkewe.

  Jorge alikutana na askari kanzu huyo tarehe 19 mwezi huu ambapo walipanga mpango mzima wa jinsi ya kumuua mkewe bila ya kusababisha polisi kushuku chochote.

  Jorge alisema kuwa anataka mkewe auliwe kwakuwa anaisaliti ndoa yao kwa kutembea na mwanaume mwingine, anatumia pesa zake, anatumia magari yake na amekuwa kila wakati akitishia kuwaita maafisa uhamiaji ili arudishwe kwao Mexico", iliripoti taarifa ya polisi.

  "Alisema kuuliwa kwa mkewe itakuwa ni zawadi yake tosha ya siku yake ya kuzaliwa", alisema msemaji wa polisi.

  Alimpa pesa askari kanzu huyo kwenye tarehe 20 na 21 na alimpa pia picha ya mkewe na ramani ya nyumba yao ili ajue wapi pa kupita wakati wa zoezi hilo la kumuua mkewe.

  Alitiwa mbaroni kabla ya zoezi hilo kufanyika na ametupwa mahabusu akisubiri kufikishwa mahakamani.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 20. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Atampata mme, japo nadhani baadae atamwacha na kutoa tangazo jingine la kutafuta mme
   
Loading...