Maajabu kumi ya tango kiafya

Maajabu kumi ya tango kiafya

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
1966723_10154499497490198_1543281209090995045_n.jpg


ASALAAM ALAYKUM Waislam na Wasiokuwa Waislam Amani ya Mungu iwe nanyi.

Maajabu kumi ya tango kiafya

Ngozi yako inahitaji tango kutoa seli zilizokufa na makunyanzi. Weka au sugulia vipande vya tango usoni au sehemu iliyoathirika na utaona maajabu baada ya siku chache.

Hawakukosea wale waliosema kuwa mboga za majani na matunda ni kinga kwa afya yako. Matunda mengi yana manufaa lakini tango tunasema limetia fora.

Kwanza linasifika kwa kuwa na vitamin zote unazohitaji kwa siku. Tango moja lina vitamin B1, B2, B3, B4 na B6, madini ya chuma, potasium na zinc.

Pili, unapojisikia kuchoka mchana, kula tango moja ambalo linaweza kukupa nguvu kwa saa kadhaa.

Tatu, ngozi yako inahitaji tango kutoa seli zilizokufa na makunyanzi. Weka au sugulia vipande vya tango usoni au sehemu iliyoathirika na utaona maajabu baada ya siku chache.

Nne, unataka kuondoa ?hangover? au maumivu makali ya kichwa, kula tango ambalo lina sukari ya kutosha na vitamin zitakazoweka mambo sawa mwilini.

Tano, umechelewa kwenda kwenye usaili, viatu ni vichafu, chukua vipande vya tango na sugulia katika viatu. Vitang?aa.

Sita, umemaliza kula, unahisi una harufu mbaya mdomoni nyakati za mchana. Tafuna vipande vya tango na utapata harufu nzuri ya mdomo.

Saba, midomo imekauka na inauma? Chukua kipande cha tango na sugulia mdomoni, utaona mabadiliko katika midomo.

Nane, umekosa muda wa kula mchana, kula tango moja bila kumenya maganda na litaweza kukaa tumboni kwa saa zaidi ya nane.

Tisa, umekosea kuandika katika ubao au ukuta, chukua maganda ya tango na usugulie taratibu, wino au rangi hiyo itafutika kabisa.

Kumi, pia, tango lina uwezo mzuri wa kusafisha vioo ambavyo vimefubaa kwa uchafu au maji ya chumvi.

Ukiwa na Swali lolote linalokukera au tatizo lolote lile wasiliana na mimi kwa bonyeza hapa.
Mawasiliano

 

Attachments

  • Tango.jpg
    Tango.jpg
    10.9 KB · Views: 1,595
Tango ni kitu cha ajabu sana, kuna mda niliamua kunywa juisi yake grasi kama 5 hivi usiku nilipata shida sana, kila nikishtuka nilikuwa nakuta nimelowa chapa chapa kama vile nimetoka mtoni. Mwanzo sikuelewa lakini nikagundua hii hari ilikuwa inatokea kila nilipkuwa nikitumia ile juisi ..nahisi inafanya kazi kubwa sana mwilini.
 
Tango ni kitu cha ajabu sana, kuna mda niliamua kunywa juisi yake grasi kama 5 hivi usiku nilipata shida sana, kila nikishtuka nilikuwa nakuta nimelowa chapa chapa kama vile nimetoka mtoni. Mwanzo sikuelewa lakini nikagundua hii hari ilikuwa inatokea kila nilipkuwa nikitumia ile juisi ..nahisi inafanya kazi kubwa sana mwilini.

Unaposema kuloa sijaelewa kivipi yani,jasho au, na juice yenyewe tupu au unachanganya na maji, nifahamishe mkuu
 
big up tango
mimi hutumia kusafisha kifua ninapokuwa nimepita au kukaa sehemu ya vumbi sasa kifua huwa kizito husaidia sana
hta nikitoka kuumwa malelia nkakosa hamu ya kula tngo usaidia kunipa nguvu na kuleta hamu ya kula
 
Kwa kuwa haliongezi nguvu za kiume sio tunda maarufu kwa vijana. Maana vijana wa siku hizi hata ukiwaambia kula mavi kutaongeza nguvu za kiume basi watabugia bila ya kinyaa
 
Kwa kuwa haliongezi nguvu za kiume sio tunda maarufu kwa vijana. Maana vijana wa siku hizi hata ukiwaambia kula mavi kutaongeza nguvu za kiume basi watabugia bila ya kinyaa

Haaaaa yamekua hayo tena hahahahaaaa
 
nasikia na nimesikia zaidi ya mara 4 kuwa ukila tango na kulamba asali unakufa.
je hii imekaaje wataalam ufafanuzi plz nn huwa sumu na kwanini??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom