Maajabu katika Website ya Bunge

Maajabu katika Website ya Bunge

Asante Mkuu kuliona hili jambo..
Uvivu na uchoko ulioko kwenye taasisi/idara za serikali (umma) ndo maana nchi haiendelei na tunazidi kudharaulika...

Huo ni mfano mmoja tu kuhusu taarifa muhimu kwenye kurasa za tovuti mbali mbali...
Njoo sasa kwenye mawasiliano ya e-mail (barua pepe)... Utaandika kadha wa kadha lakini kamwe hutajibiwa kitu...
Hata kwa suala la dharura wao watataka uende mwenyewe ofisini au upeleke barua kwa njia ya posta... Aibu sana!!
 
Kwani ni kawaida kwa Website za Tz Govt. kuwa updated on time?
Unaweza hata ukapiga simu ofisini fulani isipokelewe hadi uende physically...biz as usual..
 
Usishangae ya Musa kabla ya kuona ya Firauni!
 
Usistaajabu ukienda kwenye website ya ofisi ya waziri mkuu ikakwambia,Waziri mkuu ni laigwanani LOWASA.
 
Kweli ukistaajabu ya musa utayaona tu na mengine, mtu aliyekufa kuendelea kuonekana labda wanajisikia simanzi, sasa kubwa kuliko yote ni hii hapa:
Mhe. Deo Haule Filikunjombe bado anasoma shule ya msingi, kwa uthibitisho ingia website ya bunge
 
Jamani hao jamaa wanahudhulia bunge wakitokea kuzimu!!
 
Mimi huwa sishangai kwa website za serikali kukuta habari za miaka miwili nyuma ndiyo zipo kwenye front page ni kawaida sana, wale waajiliwa wa kazi hiyo sijui huwa wanakazi gani after.
ni kweli websites za serikali nyingi zina taarifa nyingi zilizopitwa na wakati na sijui hazina watu wakuhuisha maana hata website ya ikulu nayo hali ni ile ile.?
 
Mimi huwa sishangai kwa website za serikali kukuta habari za miaka miwili nyuma ndiyo zipo kwenye front page ni kawaida sana, wale waajiliwa wa kazi hiyo sijui huwa wanakazi gani after.
si watoto wa mjomba; wako bize kwenye masemina wakitoka huko wana hangOVER ya posho. ku update ni kitu cha dakika 5 kwa majina yote kwa wale wanaojua principle za IT.
 
Mkuu hapo kwenye hang OVER kicheko kimenikimbia asee..!!

si watoto wa mjomba; wako bize kwenye masemina wakitoka huko wana hangOVER ya posho. ku update ni kitu cha dakika 5 kwa majina yote kwa wale wanaojua principle za IT.
 
Kwa hapa mimi nawalaumu wale wote walioajiriwa ku-maintain website ya bunge, pamoja na watanzania wote, haswa vijana wenzangu, wenye tabia ya uvivu uliokitihiri katika utendaji kazi mara baada ya kupata ajira. Bila kujali ajira hiyo imepatikanaje, tabia ya uvivu imetujaa sana vijana wa Tanzania, sijui tutatokaje hapa ila nadhani nchi yetu inapaswa ipate rais dikteta akayachapa watu viboko.

Niliwahi kuona "joke" fulani nadhani ilikuwa katuni, ikionesha muda wa kazi katika siku moja ya mfanyakazi serikalini, ilionesha kitu kama hiki:

Saa 2 asubuhi:Kufika kazini
Saa 2:30 kukaa ofisini
3:00 Chai
4:00-5:00 kugusagusa kazi
5: Kuingia Facebook and social media nyingine bila kusahau Whatsapp
6:00 Kuanza kupiga umbea na kusimulia yale uliyoyaona kwenye social media, tv na kwingineko, hapo wote mnasubiri saa saba ifike
Saa 7:00 Lunch time bana, kwani hujui? Utakujaje ofisini saa hizi
Saa 8:00 kurejea ofisini, kama boss yupo, vinginevyo saa 8:30
Saa 8:00 kugusagusa vikazi
Saa 8:30: Dah, usingizi unasumbua sana aisee, kusinzia kidogo
Saa 9:00: Duh, muda hauendi kabisa yaani, kusoma magazeti yaliyoletwa ofisini
Saa 10:00 Stori kuhusu watu waliofika kuhudumiwa hapo ofisini, yule sister....yule anko....yule mdingi.....
Saa 11:00 Oyaa, hivi nyie hamna saa au?? Jamani napata lift kwa nani leo?

Kwa ratiba hii, website mtu atahakikisha saa ngapi kuwa ipo updated or no? Halafu ai-update saa ngapi? Ile barua yako uliyotuma eti unasubiri majibu, saa ngapi itasomwa halafu bosi apelekewe atoe ushauri halafu uandikiwe majibu, yapelekwe posta ili uyapate??

Mtazamo wangu.
 
Back
Top Bottom