Maajabu Jakaya Mrisho Kikwete Foundation inaanza ajira zilitoka Lini?

Good People

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
945
1,819
Aisee Nimeshangazwa sana na Jakaya Mrisho Kikwete Foundation imeanza Leo hata nafasi za wafagiaji hazijatoka Dah hii ndiyo Tanzania nimeona wejumbe wa Bodi yake Ina
-Ombeni Sefue
-Rwekaza Mukandara

Mi Mwenzenu nataka Kujimaliza Nimesha Give Up kitaa hata Kufanya Kazi bure mabosi hawataki nimeshaenda kama Halmashauri 4 nifanye kazi Bure imeshindikana.
 
Kwani lazima kutangaza?

Unajuaje kwamba ajira si za kazi ya kujitolea?
 
Wanaume wa kweli hawashobokei kuulizia ajira, ama wanauliziwa wao ajira, ama wanatengeneza ajira.

Jakaya mwanamme kapigana mpaka anatengeneza ajira kwa Foundation yake.

Mnataka kumpangia jinsi ya kuajiri watu?

Acheni kutolea macho vilivyoundwa na wengine. Tengenezeni vyenu.

Akiwaambia anaajiri watu aliosoma na kufanya kazi nao tu, mtasemaje?
 
Wewe Ni Kichaa na Kila atakayeangalia Mchango wako atagundua.
Sawa. Lakini wewe ni kichaa zaidi kwa sababu umeshindwa kueleza sababu za ukichaa wangu.

Hata hao madaktari bingwa huwa hawaagui ukichaa kwenye mtandao.

Na dalili moja kubwa ya ukichaa ni mtu kuona wenzake vichaa na yeye ndiye mzima.
 
Wanaume wa kweli hawashobokei kuulizia ajira, ama wanauliziwa wao ajira, ama wanatengeneza ajira.

Jakaya mwanamme kapigana mpaka anatengeneza ajira kwa Foundation yake...
Mbona inasemekana mwanaume wa kweli ni anayetumia Dume?

Halafu Jakaya si aliumwa na kutibiwa tezi dume, sasa kaangalie tezi dume inapimwaje halafu sema mwanaume gani angekubali.
 
Mbona inasemekana mwanaume wa kweli ni anayetumia Dume?

Halafu Jakaya si aliumwa na kutibiwa tezi dume, sasa kaangalie tezi dume inapimwaje halafu sema mwanaume gani angekubali.

Kwa hiyo na wewe unatumia dume?

Tezi dume unapima hata kwa damu, nenda Hospitali ya Mwananyamala ukaone.
 
Wanaume wa kweli hawashobokei kuulizia ajira, ama wanauliziwa wao ajira, ama wanatengeneza ajira.

Jakaya mwanamme kapigana mpaka anatengeneza ajira kwa Foundation yake.

Mnataka kumpangia jinsi ya kuajiri watu?

Acheni kutolea macho vilivyoundwa na wengine. Tengenezeni vyenu.

Akiwaambia anaajiri watu aliosoma na kufanya kazi nao tu, mtasemaje?

Kwani si hata hiyo Pesa aliyonayo inatokana na Jasho letu sisi Walipakodi na ambayo ndiyo inamtunza na Yeye? Muwe mnajifunza kufikiri sometimes siyo kuja na Utetezi wa hovyo hovyo humu Jamvini.
 
Kwa hiyo na wewe unatumia dume?

Tezi dume unapima hata kwa damu, nenda Hospitali ya Mwananyamala ukaone.
Tezi dume kwenye damu hiyo inakua ishaelekea kua kansa tena, chini ya hapo ni kuingizwa kidole tu mwanamme akaona asiingizwe kidole na mbongo mwenzake.

Alivyorudi akasema huu ugonjwa ni mdogo tu hata Muhimbili wanatibu maajabu yake hakuna aliyeuliza mbona hakwenda Muhimbili.
 
Nadhan baada ya kusimikwa rasmi kwa bodi kinachofuata sasa ni kuweka misingi ya ajira na kutangazwa kwa hizo nafasi za kazi.
Bodi ndio inaajiri...sasa ulitaka waajiriwe watu ndio bodi ianzishwe?
Tuliza kipago, kazi zitakuja.
 
Ajira bado na pia ile ni Private sio Government sasa sio lazima kira wakitangaza wew usikie
 
Tezi dume kwenye damu hiyo inakua ishaelekea kua kansa tena, chini ya hapo ni kuingizwa kidole tu mwanamme akaona asiingizwe kidole na mbongo mwenzake.

Alivyorudi akasema huu ugonjwa ni mdogo tu hata Muhimbili wanatibu maajabu yake hakuna aliyeuliza mbona hakwenda Muhimbili.
Wewe ushapima?
 
Kwani si hata hiyo Pesa aliyonayo inatokana na Jasho letu sisi Walipakodi na ambayo ndiyo inamtunza na Yeye? Muwe mnajifunza kufikiri sometimes siyo kuja na Utetezi wa hovyo hovyo humu Jamvini.
Hilo ulilofikiri nilishaliona na kulifikiri tangu mwanzo.

Kikwete alikuwa mfanyakazi wetu. Katufanyia kazi. Tumemlipa mshahara na masurufu kulingana na kazi yake.

Halafu tunataka kumpangia jinsi ya kuutumia mshahara wake tena?

Wewe muajiri wako anakupangia jinsi ya kutumia mshahara wako?

Ukistaafu kazi, ukaamua kutumia mshahara wako kuanzisha biashara, halafu uajiri rafiki zako tu uliosoma nao muajiri wako wa zamani ana haki ya kukukataza?

Acheni kutolea macho ajira kama vile mna haki nazo.

Fanyeni kazi. Gundueni vitu ambavyo vitawafanya muonekane mnahitajika na Kikwete mpaka Kikwete mwenyewe awatafute muende kumfanyia kazi.

Nina hakika mtu akigundua teknolojia ya kupata maji kirahisi sehemu zenye ukame, au kupata umeme kirahisi vijijini, Kikwete na watu wake watakuwa interested.

Wanaolilia ajira kwenye taasisi ya Kikwete wana kipi cha ajabu cha kumfanya awatake?

Msipende kulazimisha ajira kama haki zenu sehemu ambazo hata hamjui zinaendaje.

Hii ni taasisi ya rais mstaafu, si ya serikali. Kuna tofauti sana.

I am not even a Kiwete fan, but Waswahili walisema "Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni".
 
Back
Top Bottom