Malaika Mkuu
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 902
- 909
Siasa pia inaweza kuwa na maajabu yake. Uko msemo ukiyashangaa ya Musa utayaona ya Firauni. Tuliyashangaa sana ya Dr. Slaa sasa tunaanza yaona ya Freeman Mbowe,Mwenyekiti .Wakati wa Uchaguzi tulishuhudia mengi ikiwemo kufanya kosa la kuchagua Mgombea Fisadi, Mwizi na matokeo yake tukatumia kampeni yote kumsafisha. Leo hii tumekuja na kubwa lenyewe.
Chadema tumechagua mtaalamu wa Nusu kaputi yaani Dawa ya Usingizi kabla ya operesheni kuwa Katibu mkuu. Tumemchagua Dr. Kashinji .Hii ina maana kubwa kuwa tumechagua mtu atakayekuja kuipiga dawa ya Usingizi Demokrasia kama ilivyo katika utaratibu wa uendeshaji wa Chama wa Mwenyekiti Mbowe na Wapambe wake.
Swali kubwa ni hivi huyu Vicent Kishinji ndiyo nani? Ametoka wapi au amewahi kuwa nani?
Bwana Vicent ni mtaalamu wa Nusu kaputi kazi ambayo ameifanya kwa kipindi kirefu.Pamoja na hilo huyu ndiye aliyeandaa na kuratibu Mgomo wa Madaktari uliopelekea kuumizwa kwa Daktari Ulimboka. Ukiachilia Utaalamu wake wa Kuzima watu wakielekezwa kwenye Chumba cha Operesheni na kuanzisha Migogoro hana jengine analolijua kwenye siasa.
Hakika hakuna shaka juu ya uzoefu wake. Swali la msingi ni kuwa mtaalamu huyu ambaye hana kauli na hajui taasisi anayoiongoz anaweza vp kuvaa viatu vya Dr.Slaa. Sina hakika kama anaweza kuzungumza na kujenga hoja. Ma-CCM yaliwahi fanya kosa kama hilo kwa kumchagua Msomi mmoja anaitwa Mkama ambaye alikuwa ni Mshauri tu wa Chama Kuwa Katibu Mkuu. Yaliyowakuta ni Kumshukuru Mungu kwa kuwapa maono ya Kumchagua Ndg Kinana baadae maana Chama kilishatoka mstarini. Leo hii mwaka 2016 nasi tunafanya kosa hilo hilo.Mungu Tusaidie maana unaweza chukia Demokrasia kwa maamuzi ya Kidemokrasia.
Unaweza sema kuwa hakuna aliyezaliwa kuwa katibu mkuu lakini ukweli unabaki kuwa anayekuwa katibu mkuu ni muhimu sana akaielewa vizuri taasisi au chama anachokiongoza. Jambo la muhimu katika hili ni vile viatu vya aliyetangulia.Chama kinakwenda wapi? Leo amechaguliwa mtu ambaye kwanza hata Uanachama wake tunautilia Shaka. Kitu pekee nilichokisoma ni kwamba amependwa na Mwenyekiti Mbowe na Kundi lake.Nanukuu maneno yake" sikuamini nilipoitwa na Mwenyekiti Mbowe siku ya Jumanne na kuambiwa kuwa nitakuwa Katibu Mkuu".
Kweli wajinga ndiyo waliwao. Mbowe ameamua kugeuza Chama mtaji wake wa kujiwezesha kimaisha nasi tumebaki kuwa washabiki. Tunakushukuru sana.