Maagizo ya Rais kuwafukuza watumishi 9937 dhidi ya sheria za utumishi kifungu 22-23.

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939
Kwa mujibu wa Sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2002 kifungu 22, na 23 kifungu kidogo cha 1 na kifungu kidogo cha 2 a b na c imetoa muongozo wa taratibu za kufuatwa kabla mtumishi wa umma hajafukuzwa kazi
MOJA: iandaliwe hati ya mashtaka charge(mashitaka),kwa muktadha wa hawa wanaodaiwa wana vyeti feki,basi mamlaka yao ya nidhamu kwa maana maafisa utumishi/ tawala wao, baada ya kuchunguza na kuona wanatuhumiwa,basi wangeandaa hati ya mashtaka dhidi yake na kumkabidhi

Katika tukio la jana, bwana mkubwa alikabidhiwa ripoti na akawafukuza kazi mara moja bila kuwaandalia mashtaka ya kiutumishi(sio yakimahakama),

MBILI: wahusika,kwa mujibu wa sheria hiyo walitakiwa wapewe haki ya kusikilizwa baada ya kushtakiwa kiutumishi,hii ni haki ya kujitetea na kuelezea upande wao wa story ......lakini kwenye hili,hawajapata hii fursa,fursa hii huja baada ya kukabidhiwa hati ya mashitaka,na ushahidi wao,na wewe unaambiwa u-show cause kwa nini sasa usifukuzwe kazi kwa mujibu wa ushahidi unaokutuhumu kwamba umeghushi vyeti

TATU: Inquiry,ambayo sasa ndio uendeshaji wa kesi yenyewe,huyu kamuhoji yule na mengineyo

Hapa naongelea "mahakama zilizo ndani ya utumishi wa umma" ambazo ngazi yake ya mwisho ya rufaa ni Rais/Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais,tatizo linakuja pale Mamlaka ya mwisho ya rufaa,Taasisi ya urais inapoonekana tayari imefanya maamuzi kabla ya mamlaka za chini hazijakaa na kuandaa utaratibu wa mashtaka!

Ni sawa na kumsikia jaji anakutaja kwamba wewe ni "mwizi na jambazi" na unajua kesho unaenda katika mahakama yake ili akusikilize

Kitu ambacho angefanya bwana mkubwa ni kuzitaka mamlaka zichukue hatua kwa mujibu wa sheria,mara moja taratibu hizi zingekuwa activated na maafisa utumishi kwa kufungua mashtaka rasmi,na mwanasheria mkuu wa serikali naye kuitisha jopo lake
 
hao sio watumishi wa umma ila ni matapeli na wezi wa utumishi, kwa hiyo hakuna haja ya kufuata taratibu za kiutumishi wakati sio watumishi!!
 
Ila wakati wanaajiriwa waliajiriwa kwa kufuata taratibu za utumishi wa Umma....I wish kama Rais angeenda mbali zaidi kwa kuangalia wakati wanaajiriwa nani alihusika na kuwaingiza kazini maana taratibu zilzopo mtu akileta cheti lazima kifanyiwe verification
 
Acheni bla bla kama mtu kaonewa aende mahakamani
Kuna watu hata hamjulikani hua mnatete wizi au mnatetea haki
 
Sheria ya utumishi wa umma (soma kifungu cha 23 imetoa muongozo wa taratibu za kufuatwa kabla mtumishi wa umma hajafukuzwa kazi
MOJA: iandaliwe hati ya mashtaka charge(mashitaka),kwa muktadha wa hawa wanaodaiwa wana vyeti feki,basi mamlaka yao ya nidhamu kwa maana maafisa utumishi/ tawala wao, baada ya kuchunguza na kuona wanatuhumiwa,basi wangeandaa hati ya mashtaka dhidi yake na kumkabidhi

Katika tukio la jana, bwana mkubwa alikabidhiwa ripoti na akawafukuza kazi mara moja bila kuwaandalia mashtaka ya kiutumishi(sio yakimahakama),

MBILI: wahusika,kwa mujibu wa sheria hiyo walitakiwa wapewe haki ya kusikilizwa baada ya kushtakiwa kiutumishi,hii ni haki ya kujitetea na kuelezea upande wao wa story ......lakini kwenye hili,hawajapata hii fursa,fursa hii huja baada ya kukabidhiwa hati ya mashitaka,na ushahidi wao,na wewe unaambiwa u-show cause kwa nini sasa usifukuzwe kazi kwa mujibu wa ushahidi unaokutuhumu kwamba umeghushi vyeti

TATU: Inquiry,ambayo sasa ndio uendeshaji wa kesi yenyewe,huyu kamuhoji yule na mengineyo

Hapa naongelea "mahakama zilizo ndani ya utumishi wa umma" ambazo ngazi yake ya mwisho ya rufaa ni Rais/Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais,tatizo linakuja pale Mamlaka ya mwisho ya rufaa,Taasisi ya urais inapoonekana tayari imefanya maamuzi kabla ya mamlaka za chini hazijakaa na kuandaa utaratibu wa mashtaka!

Ni sawa na kumsikia jaji anakutaja kwamba wewe ni "mwizi na jambazi" na unajua kesho unaenda katika mahakama yake ili akusikilize

Kitu ambacho angefanya bwana mkubwa ni kuzitaka mamlaka zichukue hatua kwa mujibu wa sheria,mara moja taratibu hizi zingekuwa activated na maafisa utumishi kwa kufungua mashtaka rasmi,na mwanasheria mkuu wa serikali naye kuitisha jopo lake
.........kuajiriwa kwao kulikuwa hakupo kuanzia siku ile walipowasilisha vyeti feki (null and void from beginning !) Yaani mkataba waajiria ulivunjika mara tu, waliponuia kuwasilisha vyeti feki, kisha wakawasilisha kwa nia ya kumdanganya muajiri.
Muda wote wamekula mshahara isivyo halali !
Hayo maelezo yako ni mbwembwe tu za mtu asielewa. Wapo watumishi ambao walioambiwa walete vyeti original, wakaamua kusepa moja kwa moja !
 
Japo sijasoma ulichoandika, kifupi ni, ambaye hataki, asubiri mpaka trh 15, apelekwe mahakamani, na akajitetee kwa kutoa ivo vifungu. Nyie okoteni tu wapiga kura.
 
Ila wakati wanaajiriwa waliajiriwa kwa kufuata taratibu za utumishi wa Umma....I wish kama Rais angeenda mbali zaidi kwa kuangalia wakati wanaajiriwa nani alihusika na kuwaingiza kazini maana taratibu zilzopo mtu akileta cheti lazima kifanyiwe verification
.........verification hufanyika ya kawaida kwa kuangalia kwa macho cheti/vyeti vilivyo wasilishwa. What if 'Kurwa' ambaye kamaliza form six, akaamua kuwasilisha degree ya Dotto aliyemaliza chuo kikuu !? ....bado hujadanganywa !?
Otherwise detail verification hufanyika na vyombo maalum vya kiserikali.
Kuna wakati CRDB, katika miaka ambayo Kimeo anashika madaraka walifukuza 'kimya kimya' form Four fake/form six wengi sana !
Police ni eneo moja wapo la vyeti fake vingi !
 
Kwa iyo na wale watumishi hewa, wanaotumia cheti kimoja na wao wasubiri kubembelezwa! najuta kuwapigia kura.
 
Mahakama za Marekani bana ziko bomba sana ukitoa kauli kesho wanatengua duuh Trump anajuta
 
Back
Top Bottom