MLIMAWANYOKA
JF-Expert Member
- Oct 25, 2019
- 690
- 2,409
π΅π. π±πππ-π©ππππππ π΄. π΅πππππππ
____________________________
Kanisa Katoliki, tofauti na Taasis au Mamlaka nyingi, ambazo Maagizo na maelekezo mengi yanatoka Juu kwenda chini. Mfumo wa Kanisa Katoliki kwa kiwango kikubwa sana kiutendaji Maagizo mengi huanzia Chini kwenda Juu. Kanisa Katoliki halina Mfumo wala utaratibu wa, "Maagizo kutoka JUU." Bali linafuata zaidi "Maagizo kutoka CHINI".
Iko hivi, Familia ni Msingi wa Kanisa Katoliki na ni Kanisa Ndogo. Baada ya Familia, zinafuata Jumuiya Ndogo Ndogo, Kigango, Parokia, Dekania, Jimbo, Kanda na Baraza la Maaskofu Katolii Tanzania (TEC).
Viongozi wa Jumuiya wanatoka kwenye Familia. Viongozi wa Kigango wanatokana na Viongozi wanaochaguliwa kwenye Jumuiya Ndogo Ndogo. Viongozi wa Halmashauri ya Walei Parokia wanatokana na Viongozi wa Halmashauri ya Walei Vigango hadi tunafika Jimboni.
Katekista hafanyi chochote bila kuwasikiliza Viongozi wa Jumuiya. Paroko anamsikiliza Katekista na Viongozi wa Halmashauri ya Walei Kigango na Parokia. Askofu anamsikiliza Paroko. Askofu Mkuu anamsikiliza Askofu wa Jimbo husika maana yeye ndiye Mwenye Maamuzi ya Mwisho katika Jimbo lake.
Kwa Kanisa Katoliki, kama Mtu hauna Mtu haushiriki kwenye Jumuiya Ndogo Ndogo, halafu uombe Huduma za Kiroho au Sakramenti kama vile: Ubatizo wa Mtoto, Komunyo Takatifu, Kipamara, Ndoa, Mpako wa Wagonjwa au uwe Umekufa, hauwezi kupata Huduma hizo bila kupata Kibali toka kwenyeJumuiya. Yaani hapo hata kama wewe ni Mdogo wa Paroko, Askofu, Kardinali au Papa.
Mnakumbuka wale 'Wakatoliki Feki wa Crushprogram' walioenda Ubalozi wa Vatican ambao Jambo lao lilionekana Kituko kwa Jamii? Yaani wale walikuwa wanachekesha tu pale. Hata kama wangebahatika kuonana na Papa, bado wangeambiwa walipaswa kuanzia kwenye Jumuiya Ndogo Ndogo, Kigango, Parokia, Jimbo, Kanda, kisha wapate 'GO AHEAD' ya TEC ndipo waende au wapelekwe na TEC kwa Apoatolic Nuncio (Balozi wa Papa). Kila Mkatoliki anayelijua Kanisa Katoliki anaujua huo Mfumo wa Kimawasiliano na Utendaji.
Kwenda kumuomba Papa atuombee kama Taifa bila 'Kumalizana' kwanza na Baraza la Maaskofu, ni kuruka Ngazi kwa Taratibu za Kanisa. Na Papa atawasikiliza na atatuombea kwasababu ni wajibu wake wa Kiroho kiwasikiliza wanaohitaji kusikilizwa na Kuombewa. Lakini, maombi yake kwetu yanaweza yakawa hayahusiani na Utengamano, Upatanisho, Maridhiano na Muafaka wa Kitaifa.
Iko hivi tena, Papa hawezi kumsikiliza Mtu mwingine yeyote au Mamlaka yoyote nje ya Utaratibu wa kutoka kwa Apostolic Nuncio (Balozi wake) ambaye naye anakuwa na Mawasiliano ya karibu sana na Baraza la Maaskofu la Nchi husika.
Kumbukeni huyo Papa Leo XIV, Balozi wake (Apostolic Nuncio) yuko Tanzania na anajua kila kitu kinachoendelea Tanzania na hali ilivyo kati ya Kanisa Katoliki na Mamlaka zingine. Na huyo Balozi anafanya kazi kwa karibu mno na Rais wa TEC (Mhashamu Baba Askofu Wolfgang Pisa), Katibu wa TEC (Rev. Fr. Dr. Charles Kitima) na TEC nzima kwa ujumla wake.
Papa anajua kila kinachoendelea Tanzania. Ndio maana aliwahi kuomba tuiombee Tanzania. Sitaki kuamini kuwa Papa hajui Mivutano iliyopo kwa sasa kati ya Kanisa Katoliki (TEC) na Mamlaka nyingine nchini.
Na niseme tu ukweli kutoka Moyoni kwamba kwa ninavyolijua Kanisa Katoliki hili la Roma, suala lolote linalohusu UHAI wa Watu, UTU wa Mtu, HAKI za Watu, USALAMA wa Watu, AMANI ya Watu, UHURU wa Watu, nk; halitayumbishwa na yeyote, popote, wakati wowote kwa namna yoyote.
Kanisa Katoliki linafundisha kuwa, "Uhai ni Mali ya Mungu na ni Zawadi toka kwa Mungu kwetu Wanadamu. Hakuna Mtu yeyote Mwenye Mamlaka juu ya Uhai wake au Uhai wa Mtu mwingine yeyote." Ni kutokana na Fundisho hili la Kanisa Katoliki la Miaka mingi, Azimio la Haki za Binadamu (Declaration of Human Rights) la Mwaka 1948, liliiweka HAKI YAKUISHI (Right to Life) kama Haki ya Kwanza.
Kwahiyo, tunapoliona Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) linatoa Matamko, Tafakari, Misimamo, Ujumbe, Nyaraka mbalimba kuhusu kukemea Mauaji na kutetea Uhai, tujue kuwa Msingi wake ni huo. Na katika hili, nina uhakika litapambana na kupigania Haki ya Kuishi kwa gharama yoyote ile hata ikiwezekana kwa kumwagika Damu kwa Viongozi hao wa Kanisa. Ila hawataacha kukemea.
Bila kuwa na Muafaka na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC); kutangulia kwenda Vatican wakati mambo bado hayajakaa sawa huku na Kanisa Katoliki, binafsi napata kigugumizi sana kuelewa. Na naamini katika hao walioenda huko Vatican kuna Mmoja namheshimu sana na ninaamini anajua vitu vingi sana vinavyouhusu Utaratibu wa Kanisa Katoliki na analijua sana hili ninalolisema.
πππππππ: Moja, Msilichukulie POA sana Baraza la Maaskofu (TEC). Bila kufikia Muafaka wa kweli na TEC, huko Vatican kwa Papa Leo XIV badala ya kuwa Suluhisho la kudumu, kunaweza kukawa ni Utalii. Mbili, Msamaha wa kweli huja tu pale Mkosaji anapokiri kwa Moyo na kutamka kwa uwazi kuwa amekosea hiki na anaomba kusamehewa.
Hata Mungu ili atusaheme ni lazima tutamke kwa Kichwa Makosa yetu japo yeye anayajua Makosa yetu kabla hata hatujayatamka ila anatutaka tuseme tulipokosea. Kukiri ulipokosea sio udhaifu ila ni uungwana na ni njia ya kuomba nafasi ya kujisahihisha kwani hakuna Binadamu ambaye hakosei kama Malaika. Na kukosea kwa Binadamu ndiko kunakompa Mungu Utukufu kuwa Yeye pekee ni Mtakatifu. Watanzania wanapaswa kuombwa Radhi hadharani, moja kwa moja na bila kona kona au mizunguko.
Tatu, Propaganda haziwezi kufanya kazi yake ipasavyo kwenye Jamii inayoujua ukweli wa kile kinachofanyiwa Propaganda. Tukubali kuwa wa kweli na tuusema ukweli ili 'Matanga' yaishe mapema. Nne, tunapoamua kusuluhishana kama 'Wanakaya', tukubali kusemwa tulipokosea kwa kukosolewa na sisi tuseme kwa uwazi tulipokosewa ili tuyatoe madukuduku yetu yote, tuanze upya kulirudisha Taifa letu kwenye Reli yake.
Tano, watu wanatakiwa kuwajibika, kuwajibishwa, kuwajibishana na kujiwajibisha. Hata kama Mila zetu, kama Mwanajamii amefanya Makosa Makubwa anawajibishwa ili iwe Fundisho kwake na kwa wengine pia. Watu wanatakiwa kiwajibishwa na kuwajibika kwa namna ambayo itaonesha kwa maneno na Matendo kuwa watu kweli wamewajibika.
Sita, kumwomba Papa atuombee katika Jambo ambalo linahitaji kwanza Mazungumzo ya Ndugu waliokosana ni kuruka hatua ya Msingi ya "Patana kwanza na Ndugu yako kabla ya kwenda kumuomba Mungu." Msamaha wa kweli unakuja pale ambapo aliyekosewa ametoa Msamaha kabla ya Msamaha wa Mumgu.
Anyway, nimesema tu kiutani; ila sio kila utani ni wa kuuchukulia kiutani.