Maafisa wetu wa misitu jipangeni upya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maafisa wetu wa misitu jipangeni upya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MUNYAMAKWA, Jul 16, 2012.

 1. M

  MUNYAMAKWA Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni jambo jema sana kwa wataalamu wetu wanapokuwa wanaweka msisitizo juu ya kupanda miti ili kupunguza kasi ya uharibifu wa Misitu unaofanyika hapa nchini hasa kwenye Misitu yetu ya asili.Lakini msisistizo huu unakosa nguvu pale wataalamu wetu hawa wanaposisitza tupande miti ya aina mbalimbali bila kutilia mkazo kupanda aina ya miti inayokabili vyanzo vinavyopelekea uharibifu huu kufanyika kwa kasi sana, mfano matumizi ya kuni na mkaa.Wataalamu,Njooni na mkakati wa kitaifa wa kupanda miti ya kuni na mkaa maana hiyo miti ya mbao mnayotuhamasisha kupanda itatupatia kuni na mkaa si chini ya miaka 8 hata zaidi ya miaka10 ijayo, sasa je kabla ya kufika huko nishati ya mkaa na kuni ambayo ndo watanzania tuliowengi tunaitegemea tutaipata wapi kama sio kuendelea kufanya uharibifu huko Misituni.
  Naomba muwe creative,na muamini juu ya hili: kwamba tukiweza kupunguza utegemezi wa nishati ya kuni na mkaa toka Misituni(Misitu ya asili) tutanusuru misitu yetu ya asili na kutunza mazingira.Fikeni pahali ambapo uvunaji haramu wa Misitu kwa ajili ya nishati ya kuni na mkaa muufanye iwe historia katika nchi hii, na hapa tutawa 'credit positive' maana hata maboss wanatumia mkaa huu huu kwa matumizi mbalimbali.
  Source:Munyamakwa
   
Loading...