El'son
JF-Expert Member
- Jun 3, 2012
- 380
- 324
Ndugu zangu watanzania kwanza niwape pole kwa maafa yaliyotokea juma lililopita. Mungu awatie nguvu kwa kipindi hiki kigumu sana. Nimejaribu kuvumilia lakini nimeona isiwe tabu hebu tujadili hili kwa kirefu zaidi.
Binafsi nimekaa nikatafakari sana kuhusu hii ajali ya MV Nyerere kwa namna ilivyoleta maafa makubwa miongoni mwetu, lakini mpaka sasa bado sijapata jibu sahihi, japo siwezi kupingana hali halisi tayari vifo vimeshatokea kwa watanzania wenzetu.
Kikubwa kinachonishangaza ni ukaribu wa eneo la ajali ilipotokea na maafa yaliyotokea. Ni vitu ambavyo havioani kabisa. Kama ajali hii ingetokea zaidi ya kilomita kadhaaa basi hii hoja yangu isingekuwa na mashiko. Lakini ukiangalia picha ya mazingira ya ajali utaona ajali imetokea ndani ya mitaa kadhaa tu. Na ukilinganisha mita hizo na idadi ya watu waliokolewa unaweza pata kizunguzungu. Ajali hii imetokea karibu sana jamani mtu yupo ufukweni anaona kabisa kila kitu, sasa nini kimetokea mpaka idadi ya waliokufa iwe kubwa kiasi hicho. Kwa mazingira hayo nilitarajia watu wengi zaido ndio wangeokolewa.
Najaribu kutafakari tuu ila bado nashindwa amini. Niwatakie tafakuri njema ndugu zangu.