Maadui wa umma.

Maadui wa umma.

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,932
Reaction score
11,849
Wafuatao ndo maadui wanaolitafuna Taifa hili
1.CCM chama hiki pamoja na kuwa madarakani miaka 53 kimeshindwa kumuinua mtanzania toka katika hali duni na ugumu wa maisha kwani pamoja na kile kidogo ambacho wamefanya ni kutokana misaada na mikopo toka nje(rejeani deni la Taifa) jambo la kujiuliza rasilimali zetu zinazoteketea zimeleta faida gani?
2. Walimu hawa wanaingia kwenye kundi hili kwani wamekuwa wakituhujumu sisi wapiga kura katika masanduku ya kura pili, pamoja na serikali kuwatenga kimaslahi baadala ya kuonesha hasira zao kwa serikali wameelekeza hasira kwa watoto wetu wasiokuwa na hatia kwa kutowafundisha vizuri hivyo kupelekea wanafunzi wengi kufeli,
3.Waislamu na waakristo hawa nawaingiza kwenye kundi kutokana na viongozi wao kuacha neno la Mungu na kuhubiri siasa makanisani na misikitini mwaka 2005 wakristo walitumika kuhujumu uchaguzi ule baada ya kuaminisha kuwa CUF ni chama cha waislamu vivyo hivyo mwaka 2010 waislamu waliaminisha kuwa chadema ni chama cha wakristo hivyo wasimpigie kura mgombea wake hivyo kupelekea kuchelewesha mabadiliko wito wangu kwenu wekeni itikadi zenu pembeni nchi inaliwa hii,
4.Wachina, hawa wamekuwa wakiiba mali za umma waziwazi huku serikali ikiwachekea pili watu hawa wametuingiza kwenye mikataba mibovu ambayo itazidi kulinyonya Taifa.
5,Jeshi la polisi, jeshi hili limekosa weledi linafanya kazi kimazoea limeshindwa kulinda na raia na mali zao limekuwa linabambakizia raia kesi, rushwa imeshamiri katika jeshi huku likiwa linaonyesha upendeleo wa wazi kwa chama tawala huku likivionea vyama vya upinzani, jeshi hili unaweza kuua,kuiba,kubaka usifanywe chochote hasa kama una pesa.

Tata Molembe.
 
Last edited by a moderator:
6.Wasomi kwa kutokupiga kura na pia kutojitokeza kwa wingi kugombea nyadhifa mbali mbali na kuwaachia wasiosoma kutuongoza
 
Wenye chama chao watakuja humu kusema unamtukana na kumdharirisha mwenyekiti wao, Jiandae kwa vyoto (Hoja na matusi)
 
1 na 4 zimenikolea sana ! Hao ni maadui kwelikweli wa taifa hili .
 
Kwa upande wa walimu utakuwa umewaonea!

Kwani karibia wote ni wanachadema.
 
Wafuatao ndo maadui wanaolitafuna Taifa hili
1.CCM chama hiki pamoja na kuwa madarakani miaka 53 kimeshindwa kumuinua mtanzania toka katika hali duni na ugumu wa maisha kwani pamoja na kile kidogo ambacho wamefanya ni kutokana misaada na mikopo toka nje(rejeani deni la Taifa) jambo la kujiuliza rasilimali zetu zinazoteketea zimeleta faida gani?
2. Walimu hawa wanaingia kwenye kundi hili kwani wamekuwa wakituhujumu sisi wapiga kura katika masanduku ya kura pili, pamoja na serikali kuwatenga kimaslahi baadala ya kuonesha hasira zao kwa serikali wameelekeza hasira kwa watoto wetu wasiokuwa na hatia kwa kutowafundisha vizuri hivyo kupelekea wanafunzi wengi kufeli,
3.Waislamu na waakristo hawa nawaingiza kwenye kundi kutokana na viongozi wao kuacha neno la Mungu na kuhubiri siasa makanisani na misikitini mwaka 2005 wakristo walitumika kuhujumu uchaguzi ule baada ya kuaminisha kuwa CUF ni chama cha waislamu vivyo hivyo mwaka 2010 waislamu waliaminisha kuwa chadema ni chama cha wakristo hivyo wasimpigie kura mgombea wake hivyo kupelekea kuchelewesha mabadiliko wito wangu kwenu wekeni itikadi zenu pembeni nchi inaliwa hii,
4.Wachina, hawa wamekuwa wakiiba mali za umma waziwazi huku serikali ikiwachekea pili watu hawa wametuingiza kwenye mikataba mibovu ambayo itazidi kulinyonya Taifa.
5,Jeshi la polisi, jeshi hili limekosa weledi linafanya kazi kimazoea limeshindwa kulinda na raia na mali zao limekuwa linabambakizia raia kesi, rushwa imeshamiri katika jeshi huku likiwa linaonyesha upendeleo wa wazi kwa chama tawala huku likivionea vyama vya upinzani, jeshi hili unaweza kuua,kuiba,kubaka usifanywe chochote hasa kama una pesa.

Tata Molembe.

7. CHADEMA; hawa walijifanya kuwa ni wana demokrasia wa kweli, wenye maadili na wapambanaji wa ufisadi kiasi watz wakaanza kuweka matumaini kwao, kumbe lah! hakuna lolote ni wizi mtupu na unafiki wa hali ya juu!!!! ubabe, uimla, udini, ukanda na kashfa za ngono huko ndo zimejaa!!!
 
Back
Top Bottom