Wakuu, kwa kuwa viongozi wetu wamekiri hadharani kuwa hawajui sababu ya umaskini wetu, naona itakuwa vema, pamoja na kuwa tumechelewa na kimsingi walitakiwa kujua, kuandika kidogo kupitia humu Jamvini.
Miaka kadhaa nyuma, kama Taifa, tulisema ili tuendelee tunahitaji WATU, ARDHI, SIASA SAFI na UONGOZI BORA. Yawezekana sababu zimepungua au kuongezeka, ni uzi wa siku nyingine.
UONGOZI BORA, naanza na huyu, cz huyu amekuwa sugu kwa kuwa hakuwekewa vigezo na mikakati makini ya kupambana nae, hasa kwa wanasiasa.
Watendaji wakawekewa sifa na vigezo kwa ngazi mbalimbali. Elimu na uzoefu; Elimu ya sekondari na vyuo;
Wanasiasa, wakaachwa, wakajiwekea vigezo laini na vyepesi ambavyo haviumizi ubongo; KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA!.
Hili ni kosa kubwa tunaloendelea kulilipia, na ndio maana hawajui wanachofanya, hawawezi kufikiria vizuri, hawaumizi vichwa, tafsiri ya cheo kwao ni ulaji, wanatoana macho na kutumia rushwa za kutisha!
Iwapo kweli tunataka kupambana na adui huyu, ni lazima wanasiasa nao wawekewe vigezo vya elimu na uzoefu katika ngazi zote.
Hii ni muhimu sana kwani tunashuhudia wanasiasa wetu wasivyo na upeo, hawana maono, hawafikirii mambo makubwa, hawana mikakati, wanarubuniwa kwa urahisi, ulimbukeni na mengi mengine, yet hawa ndio final decision makers! Lazima kujipanga kumuondoa adui huyu ili tuendelee kama wengine.