Tunakushukuru sana Spika Ndugai kwa ujumbe wako huo murua kabisa.
Mbali ya mhimili wa Mahakama, pia kuna haja hata maeneo mengine ya utoaji haki uzingatie huo ushauli uliotolewa na Mh. Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbali ya Mahakama kuna maeneo mengine kama TUME YA UTUMISHI WA UMMA ambapo mojawapo ya kazi zake ni kusikiliza na kutatua migogoro ya kazini, kati ya mwajiri na mwajiriwa.
Ni muhimu sana TUME YA UTUMISHI WA UMMA walijue hilo kwasababu ni mojawapo ya taasisi zinazosimamia na kutoa haki.
Kama ilivyoelezwa, TUME ijikite kutoa haki kwa kumtanguliza Mungu bila ya upendeleo wowote, maana inaaminika kuwa kumekuwa na kawaida ya waajiri kuirubuni au kushinikiza TUME ili kuwakandamiza watumishi walioko kwenye mgogoro na mwajiri wao.
Inasemekana kuwa kuna baadhi ya wajumbe wa TUME wamekuwa wakiwa-influence wajumbe wenzao ili kutoa uamuzi ambao ni biased kwa kumkandamiza mtumishi, na kuwa slow kushughulikia matatizo ya watumishi.
Asante,